Maridhiano ya kitaifa,vyama vya upinzani vinapaswa kubadili sera na mitazamo yao

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
MARIDHIANO YA KITAIFA,VYAMA VYA UPINZANI VINAPASWA KUBADILI SERA NA MITAZAMO YAO.

Leo 12:15pm,09/02/2020.

Wakati viongozi waandamizi wa vyama vya Upinzani nchini Tanzania wakipuyanga ughaibuni kutafuta pesa kwa njia ya kuichafua nchi kwa kila namna wanayoweza hata kwa kulamba miguu ya Wazungu ikiwezekana wazuie misaada ya benki ya dunia kwa Tanzania wapewe wao.

Wengine wanaendelea kujiuguza japo wamepona wakipiga bia baada ya kupanda kwenye mimbali ya television ya BBC katika kipindi cha Hard Talk wakiichafua Tanzania hata kusema haikaliki,

Ilihali Wananchi wengi wa Tanzania hawajui hata mlio wa bunduki ukoje,Njaa ya Madaraka na kukosa Uzalendo kunawafanya watu kukosa uaminifu kwa nchi yao waliyozaliwa,kukua hata kusomeshwa bure na kupata elimu ya sheria waliyonayo.

Wengine wamehojiwa kwa kukosa nidhamu mpaka wakapata njaa na kuahidi wakishiba watakuja kuongea kuhusu mahojiano yao,Utashangaa sana utapogundua mtu unayemlisha akikusaliti na kukutukana sirini,

Baada ya kuweka wazi meseji zake na sauti na kumuuliza,anajibu bila soni kuwa ni yeye na Sauti ni yake na kumalizia kwa kusema nichafue ninuke,utagundua watu awa wanashida pengine tonge lao walilozoea kulileta mdomoni limeshikwa na Mwanaume,sasa njaa kali wanaishia kusengenya.

Kitako cha andiko ili ni kuonyesha namna gani vyama vya Upinzani Tanzania vimebadilika na kuwa vyama vinavyopinga Maendeleo ya Tanzania hata ikiwezekana kuwa vibaraka wa Wazungu ili wasaidie na Wazungu kuutoa Uongozi madhubuti wa Rais Magufuli,

Uongozi ambao haupendi upumbavu,Uongozi ambao haupendi rushwa,Uongozi ambao haupendi rasilimali za Tanzania kuibiwa,Uongozi ambao unataka kuitoa Tanzania toka nchi masikini hadi kuwa nchi tajiri kama ilivyo China.

Sasa wakati umefika na Vyama vya Upinzani nchini Tanzania vitalazimika kubadili tabia zao mbaya ili kuwa vyama vya Upinzani badala ya vyama vinavyopinga kila jambo ndipo kufanyike maridhiano kuweza kuleta siasa safi katika Taifa letu.

Toka Chadema ishindwe uchaguzi 2015 kuna tabia ambazo imezijenga kama Chama kwa muda ambazo zimefanya chama cha Chadema kutoka katika misingi yake ya kupigania maslahi ya nchi,kupiga vita rushwa na kuwa chama kinachopinga Serikali ya Rais Magufuli inavyopigania maslahi ya nchi na kupiga vita rushwa.

Tabia za Chadema za sasa zinaweza kuwa zinakinzana na tabia au Sera iliyowahi kuwa nazo ili kuweza kujijenga kama chama kinachopigania maslahi ya Wananchi.

Sera ya Chadema ilikuwa nzuri sana kupigania maslahi ya Taifa la Tanzania lakini sasa Sera ya Chadema ni kuipinga Serikali ya CCM chini ya Rais Magufuli inayopigania maslahi ya Taifa la Tanzania na kupiga vita rushwa,ufisadi na unyonyaji uliokuwa ukifanywa na Mabepari katika sekta za Madini,Maliasili na Uwekezaji.

Je! Chadema iko tayari kuachana na tabia zao za sasa ili kujenga tabia nyingine ambazo zitasaidia Taifa la Tanzania kufanikiwa? Jambo hili huwa ni changamoto kwa Chama chenye watu kama Zitto Kabwe na Tundu Lissu ambao wanataka kupata kiki kwa namna yoyote ile ili wapate Uongozi wa juu katika nchi. Mtu kama Zitto Kabwe au Tundu Lissu anatamani kufanikiwa lakini hayuko tayari kubadili tabia zake.

Ni lazima tuwe tayari kubadilika kama tunataka kufanikiwa zaidi. Ulivyo leo ni matokeo ya matendo yako ya kila siku ambayo mengine kwa kiasi fulani yamefanyika kuwa tabia yako,na kamwe hatuwezi kuruhusu kiongozi wa juu wa nchi mwenye tabia mbaya kama Zitto Kabwe na Tundu Lissu.

Kama Zitto Kabwe na Tundu Lissu wanautaka Urais wa Tanzania,wanapaswa kutoka katika hali zao za tabia mbaya za sasa na kwenda kwenda kwenye tabia za Uzalendo kwa Taifa na nchi yao,ni wazi kwamba kuna Mabadiliko ya baadhi ya tabia watapaswa kuyafanya.

Watu kama Zitto,Tundu Lissu,Fatma,Maria,Ansbert Ngulumo wanapaswa kupitia kwa makini tabia zao za sasa ili kubaini kama zina mchango wowote wa kulisaidia taifa kufikia malengo ambayo Serikali ya Awamu ya tano inatamani kuyakamilisha.

Kama tabia zao watu hao ambao ndio wasemaji na viongozi wa vyama vya upinzani kama tabia zao zina mchango kidogo au hazina kabisa basi zinapaswa kubadilishwa.

Yaweza ikawa ni vigumu kwao kuachilia tabia zako za awali lakini kwa kutazama umuhimu wa malengo ya Taifa na faida za kutimiza malengo hayo inakuwa rahisi kwako kufanya maamuzi ya kuachana na tabia zao mbaya ambazo hazisaidii Taifa la Tanzania kufikia malengo yake ya kuwa Taifa tajiri na lenye nguvu kiuchumi.

Sasa basi hata kama tabia fulani wao wanaona zinawafurahisha wao na jamaa zako lakini kama hazisaidii Taifa kufikia malengo yake ambayo ni muhimu zaidi wanapaswa wawe tayari kuibadilika la sivyo Taifa litawalaani na kuwakataa kama Wananchi wake kwa kuwa wamekosa Uzalendo.

Furaha wanayoipata kwa kulitukana Taifa nje ya nchi na kuzuia misaada kwa taifa la Tanzania ni furaha ya muda mfupi lakini hasara ya kushindwa kuishi ndoto zao katika Taifa la Tanzania ni kubwa zaidi.

Hatuwezi kufanikiwa kama Taifa kama hatuko tayari kubadili tabia zetu mbaya za kunyenyekea Wazungu hata pale wanapoiba na kupora Maliasili zetu,Tuliona makaburu yakiwachapa fimbo Wananchi na wananchi walibaki kusema "please Mr boer beat me again".

Tunapokumbuka uonevu mkubwa tuliofanyiwa na mabeberu hatuna budi kuacha tabia za kujipendekeza kwa mabeberu,tabia ambazo hazina mchango katika mafanikio ya Taifa letu la Tanzania. Mafanikio katika Taifa lolote lile yana gharama ya kuwa na Wananchi Wazalendo.

-Lugha mbaya za Upinzani zasababisha CCM kuwakataa Wapinzani.

Kwa mtiririko wa hapo juu kuhusu tabia mbaya za Vyama vya Upinzani,CCM inashindwa kuwakubali wapinzani tangu mwanzo mfano baada ya uchaguzi wa 2015 kwa kuwa Wapinzani wamekuwa na lugha kali na za vitisho haswa,Mfano Sauti za Freeman Mbowe na Halima Mdee kwenye mkutano wa Kinondoni uliosababisha Fujo.

Lugha kali majukwaani zimepelekea CCM kujihami na kuwaona Wapinzani kama maadui na sio wanaharakati au Wapinzani wenye sera mbadala,Lugha kali daima uwa ni kama mawe na mara nyingi yule unaemtusi huwa anajihami na kutokukushirikisha kwenye maongezi ya kujenga nchi kwa kuona wewe mpinzani ulianzishwa kwa sera za ushinikizwaji wa mabeberu.

Mfano mzuri kule Israel Hamas ilianzishwa na wayahudi ili kumvunja nguvu Arafat lakini leo hii Israel inapambana na Hamas kwa sababu wale wamekataa kuendelea kuigawanya palestina sasa kama kutakuwa na maridhiano ya kitaifa "national dialogue" tuanze na kubadilisha lugha zetu.

-Kama Upinzani utakataa kubadili tabia,Chama kimoja inawezekana.

China imetuonyesha mfano kuwa maendeleo ya Taifa yanaweza kuja na chama kimoja,China imefanikiwa,kwa nini Tanzania isifanikiwe,Kama wakati wa kujenga reli ya Tazara tulijifunza kutoka kwa Wachina kushona viraka katika nguo zetu kwa nini tusiige sasa namna walivyofanikiwa kuwa Taifa kubwa?.

Mfano mwingine China iko kwenye vita vya kiuchumi na Marekani, bidhaa za China zimewekewa kodi kubwa kuingia Marekani lakini wachina hadi leo wameungana na kupambana na Mmarekani bila woga wala kutetemeka,

Enyi Wapinzani wa Tanzania mlioangukia kuwa vibaraka wa Wazungu,Je hamuoni cha kujifunza hapo!!

Kama Magufuli angeanza kulia na kuomba maandamano kwa sababu bila makombo ya wazungu tutakufa njaa,Je ingeendelea kuwa sahihi kwa mustakabali wa nchi yetu? Tunae Rais Mwanaume kweli kweli ambae hateteleki sio watu kama Zitto Kabwe na Tundu Lissu ambao hata sasa wanalamba miguu ya Wazungu ughaibuni.

Hapo kabla Wachina walikuwa wametawaliwa na waingereza wajapani na mmarekani alijaribu kupeleka siasa yake ya kibepari wakitumia wachina walioishi Marekani.

Wachina hawakukubali,Mmarekani akaja na mapinduzi,bado china hawakukubali,Wakawafukuza na kuuwa vibaraka wote,Marekani alipoona hivyo akakimbilia Taiwan ndipo Mmarekani alipotimiza malengo yake,

Umoja na Uzalendo wa Wananchi wa China umewafikisha hapa walipo,kama wangalikubali propaganda na sera za democracy ya Marekani naamini hadi leo China ingekuwa Taifa masikini duniani.

Sasa sisi waafrika tumechukuliwa utumwa. Tukatawaliwa kimabavu na sasa kiuchumi kwanini tusiwe na moyo wa ujasiri tukaacha tofauti zetu na kujikomboa moja kwa moja? Zitto Kabwe na Tundu Lissu kwa nini ninyi mnakubali kuwa vibaraka wa Marekani?

-Chadema inapaswa kurudi katika Misingi yake.

Sasa basi kwa kuwa Chadema inawezekana kuna sehemu mmeteleza kwa mtazamo wa wengi ikiwezekana mliamini mmeshinda 2015 ikapelekea kuweka gubu mioyoni mwenu,

Gubu mliloliweka mioyoni mwenu lilisababisha mtoke katika misingi yenu,sasa basi rudini katika misingi yenu na sera zenu nzuri kama chama chenye Sera mbadala badala ya kupinga kila jambo liwe zuri au baya,Sisi CCM ni wazazi na kamwe mtoto akikunyea mgongoni hatumtupi chini,kazi kwenu Chadema.

Tumeona Ghana, Zambia, Malawi na hata Namibia ..wao wameamua kuongea ..wameanza kuaminiana ...shida kubwa Chadema wanapenda sana kusema wanaonewa ilihali mara nyingi ni propaganda zao wanazotengeneza ili ionekane wanaonewa.. huenda wanafanya hivyo kupata kuonewa huruma na Wananchi,

CCM inapowakumbusha upinzani kuiga mfano wa China wanasema si sahihi kusema hivyo,Wapinzani mfano wa Zitto Kabwe na Tundu Lissu wanataka kuiga Marekani.

Pengine ni sawa Wachina hawawezi kuwa mfano wa kuigwa hata kidogo lakini Marekani ndio kabisa hawawezi kuwa mfano wetu.

China waliamua wao kuungana kwa msaada mkubwa wa Kiongozi wao Mao Zedong

Wachina wana historia kubwa kwanza wote wanaongea lugha moja isipokuwa Wamongolia lakini kwa umoja wao wameshikamana sana.

Lugha yao imewasaidia sana na hawataki kabisa kujiingiza kwenye Migogoro ya kivita,Pia sera zao za kujifunza na utamaduni wao wa Kizalendo umewasaidia sana.

Waliamua kuitafuta elimu na technology kwa gharama kubwa na ndiyo maana wamefikia hapo walipo,Wachina na Watanzania tunafanana utamaduni,ni rahisi kwetu kuiga mfano wa China.

Sisi wanaccm kwa upande wetu tunawajibu mkubwa wa kuijenga nchi yetu mimi naamini kuwa na mitazamo tofauti ni jambo jema na tukubaliane hamna mwenye ukweli mfukoni wa kutatua kero zote za wanachi,

Sisi Wanaccm tungependa kuona zile sera za wapinzani hata wakishindwa uchaguzi wazitekeleze na sio kususia kila kitu mfano kuna huduma ya kijamii au kiuchumi waziendeleze

Sio kutumia nguvu nyingi ku crash na kuipinga CCM hata sasa CCM inapofanya mambo makubwa ya kujenga nchi ambayo hayakufanywa kwa miaka 50 lakini kwa awamu hii ya tano mambo yote muhimu yamefanyika ilihali yalikuwepo kwenye ilani ya CCM toka mwaka 1977.

CCM itaanza kuwaamini vyama vya upinzani vitakavyo badili lugha na mtazamo wao. Mh Rais ameteuwa viongozi mbali mbali kutoka vyama vya upinzani yupo mkuu wa mkoa. Katibu mkuu wizara ya maji wanafanya vizuri sana.

Mfano Zitto Kabwe yupo na madiwani wa ACT katika halmashauri ya Kigoma, kwa hiyo kwenye ule uchaguzi wa serikali za mitaa ACT na Chadema wakajitoa,hofu ya kujitoa ni nini ilihali tunataka wajumbe na wenyeviti wa vyama tofauti,

Kama mngeshiriki uchaguzi ingeongeza umaana na kuaminiana na kujenga mshikamano kitaifa na hata kuwa na nguvu zaidi za kupambana vita hii ya kiuchumi kwa pamoja.

Ni vyema pia Wananchi wakaitisha mkutano na Mbunge na kumhoji na kumueleza atakapokwenda bungeni akumbuke maslahi ya Jimbo kwanza na sio chama anachotoka.

Hapo tutajifunza kuwa baada ya uchaguzi lazima tuweke tofauti zetu pembeni na wawakilishi kwa pamoja wawakilishe jimbo kwa pamoja kwani wananchi wanahitaji maendeleo.

Kamwe mbunge wa Upinzani usikwamishwe na Chama chako eti kwa vile chama chako kitaifa hakitaki tushirikiane.

Chadema na ACT wamepinga miradi hii ya awamu ya tano mfano kurudisha usafiri wa treni Dar to Moshi,na baada ya kurudishwa wamepanda treni hiyo kwenda Moshi.

Naamini Wapinzani hao hao ndio watapanda treni ya Umeme kutoka Dar to Morogoro na hadi Dodoma,Sasa tabia hizi mbaya za kuipinga Serikali inayoleta Maendeleo kwa Taifa zinatoka wapi,

Kwa nini Wapinzani wasifanye Siasa za kueleza tulikotoka tulipo na tuendapo na hatua adimu tuliyofikia badala yake mnataka watu waache kazi wakakae na ninyi kuzungumza maridhiano ya nchi inayoendelea kwa Speed ya 4G,kwa siasa za hapa kazi tu na maendeleo ya Wananchi kwa speed ya 4G tunahitaji Maridhiano ya nini!?.

Tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie Madarakani,Chadema ilikuwa inajitenga na shughuli za kitaifa kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Kama Chadema,ACT na watu kama kina Zitto Kabwe na Tundu Lissu watakubali kubadili Tabia,Mitazamo na Sera zao ndipo nitakapounga mkono wito wa wadau wa Siasa,Viongozi wa dini na Wanaharakati wa kutaka kuwepo maridhiano ya kitaifa ya vyama vya Siasa nchini.

Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kuibariki Tanzania,Ahsante Mwenyezi Mungu kwa kumbariki Rais wetu,John Pombe Magufuli.

Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854
 
Back
Top Bottom