Maridhiano ya kisiasa ya CCM na vyama vingine yasifanyiwe mzaha na upande wowote

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
5,159
5,399
Waswahili tunasema chanda chema huvikwa pete, lakini pia nyota njema huonekana asubuhi.

Nchi zote zilizofikia hatua ya kupatikana katiba na Tume Huru za Uchaguzi katika nchi zao, zilipitia katika magumu mengi. Si lazima magumu hayo yafanane lakini yanaweza kuwiana.

Kenya ni mojawapo ya nchi ya kutolea mfano. Rais Mama yetu ameamua kwa dhati kutengeneza Tanzania ya mfano, kwa kauli zake amejitanabaisha hivyo. Madhira ya Wanasiasa wa Tanzania wa Upinzani yamekuwa chachu ya msukumo wa maridhiano haya chini ya mwenyekiti Freeman Mbowe wa CHADEMA.

Watanzania tumekuwa na imani kubwa mno kufanikiwa kwa jambo hili zuri kama tulivyokuwa na imani kwa Rais Mstaafu J. Kikwete alipoanzisha uundwaji wa Katiba Mpya na kisha kutelekezwa.

Swali langu chokonozi kwa Watanzania wote ni je, kutelekezwa kwa Katiba ya Jaji Warioba ni kwa bahati mbaya ama kulipangwa na watu wasioonekana ama wanaoonekana?

Swali la nyongeza, Mchakato huu wa maridhiano ili kuleta Katiba na Tume Huru siyo mpango mficho mwingine tena ulioanzishwa na wahusika ili kurubuni akili za Watanzania kuwa wanafanya kumbe ni kuvuta hisia na kupata wafuasi wengi na kisha kuutelekeza tena?

Nikiwa Mtanzania napongeza kuanza kwa maridhiano haya na pia nampongeza Rais kwani mwisho ukiwa kama ulivyopangwa utampaisha mama huyu Duniani, atakuwa amefanya kitu ambacho Dunia nzima itajifunza kwake.

Lakini pia ikiwa mchakato huu utakuwa wa maigizo ili kuvuta muda na kisha kuutelekeza matokeo yake yatakuwa mabaya mno na yatazaa kitu kibaya ambacho itakuwa historia kwetu na Duniani.

Ni wazi Rais mstaafu J. Kikwete kwa nafasi yake bado ni mshauri wa Rais na ana nafasi yake kwa kufanikisha zoezi hili, hivyo Watanzania bado tuna kumbukumbu ya namna walivyoratibu vyema mchakato wa kutupumbaza kwenye Katiba ya Warioba ili muda uende.

Ni wazi pia Kinana naye ni mshauri wa Rais na alikuwepo na kushiriki katika uanzishwaji wa ile Katiba iliyotelekezwa na bado yupo katika hili kama mhusika wa kati ambaye ndani yake ni mhusika mkubwa pia. Uwezo wa kinana katika siasa upo bayana kama ilivyo kwa J. Kikwete. Watanzania tunajua na tunaelewa mambo mengi ya kweli na ya uongo.

Ikiwa tunamtakia Mama yetu mwisho mwema kwa Watanzania na mbele za Mungu wake basi tumsaidie na makundi yote yamsaidie kufikia upatikanaji wa Tanzania mpya kwani faida zake ni nyingi kuliko hasara zake.

Kwa kuwa Manju wa ngoma hii ni Rais mwenyewe na jopo lake ana wajibu wa kuamua ngoma hii ichezwe kwa muda gani ili isiwakinai wahusika hadhira.

Watanzania kwa wastani mkubwa tuna imani na Maridhiano haya. Chonde kusiwe na mzaha wa kisiasa na kitelekezwa kwa Maridhiano na kukosekana kwa Katiba Mpya yenye ulinzi na Tume Huru ya Uchaguzi kabla ya 2025.

Hongera Mama Samia, sasa Tanzania inaelekea kupata mtu, na iwe hivyo.
 
Dhana ya maridhiano ina presuppose kuwepo kwa conflict hapo awali. Nachokiona mimi ni abuse of power iliyofanywa na mtu mmoja, ambayo suluhisho lake ni kuziba gap za kisheria au kikatiba zinazompa mtu mmoja madaraka mengi ya kuchezea.

Lazima kuwe na legal interventions kwasababu tatizo liko kisheria. In as much as mama kaonesha political will, swali je yeye akiwa hayupo, atakuja mtu mwenye utashi wa kisiasa kama wake? Hivyo basi, suluhu ya kweli ni maboresho ya katiba na sheria.
 
Hakunaga maridhiano ya namna hii popote pale duniani , kilichopo ni matawi mawili ya CCM yaliyong'atwa pamoja sasa wanajipongeza , wakat mwingine mda ndo hujibu mambo yaliyojificha , tuuache mda useme Kwa uzuri
 
Kama CCM unafanya janja juu ya maridhiano basi itakuwa jambo baya sana maana kuaminiana Kwa jamii kutapungua sana matahlani ambavyo vyombo vya haki ambavyo haviaminiki hata kidogo hivyo watu wenye busara na hekima wawe chachu wa kuhimiza ukweli juu ya jambo hili.

Hadaa zote zile hazita zaa matumda hata kdogo maana wananchi wanaona na kusikia wanasubuli Nini kitatokea
 
Kama ccm unafanya janja juu ya maridhiano basi itakuwa jambo baya sana maana kuaminiana Kwa jamii kutapungua sana matahlani ambavyo vyombo vya haki ambavyo haviaminiki hata kidogo hivyo watu wenye busara na hekima wawe chachu wa kuhimiza ukweli juu ya jambo hili.
Hadaa zote zile hazita zaa matumda hata kdogo maana wananchi wanaona na kusikia wanasubuli Nini kitatokea .
Tunaandika haya ili wayasome na wajue kuwa ukweli tunaujua na tunatoa tahadhari hii ni last card kwao.
 
Back
Top Bottom