Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 39,762
- 71,145
Kuna watu watasema suala liko Mahakamani hivyo lisubiri, lakini sio kweli.
Kesi iliyoko mahakamani ni kati ya wanachama 19 waliokuwa Chadema na chama chao cha zamani Chadema na haihusiani na Bunge kwani Bungeni wameshapewa taarifa kuwa hao wameshafukuzwa sio wanachama tena.
Kila mtu anajua kuwa wale wako bungeni kwa nguvu ya serikali ya CCM na sio nguvu ya katiba kwani hawana chama. Hivyo kulazimisha kuwa ni wabunge wa chama fulani kilichowakataa ni kunajisi hayo muitayo maridhiano na ni UKOROFI TUU.
Kamati kuu ya Chadema inayokutana leo ilijadili na hili kwani kesi ile wale wanapigania uanachama wao hivyo hawana haki kuwepo bungeni kama wawakilishi wa Chadema. Vinginevyo hayo MARIDHIANO YAMEJAA HADAA NA DHARAU . Serikali/Bunge watimize wajibu wao kuwaondoa kabla mambo hayajaharibika na Rais kuonekana muongo