Mariam Ditopile: Tegeni sikio Jumapili Rais Samia ana jambo zito sana

Mkoa wa chato utatangazwa siku kuzima mwenge.....J2 ana propaganda yake tu.....miradi maji ...miundombinu etc
 
Mliitengeneza "MOVIE" ya kura feki nchi nzima.....nani asiyejua?!!!

Mliuratibu mtandao koko nchi nzima.....nani asiyejua?!!!

Una matatizo ya KISAIKOLOJIA wewe......
Kuchapisha kura fake na kutamba nazo mitaani tena kwenye vituo vya kupigia kura tena kwenye siku ya kupiga kura ni very serious crime,ni kosa la jinai ambalo ni serious sana!

Sasa kama upinzani walichapisha kura fake kwa nini hawajakamatwa na kushtakiwa kwa kutenda kosa hilo ambalo ni very serious crime?
109_20210724_194836.jpg
109_20210724_194739.jpg
109_20210724_194857.jpg
 
Kutakuwa na mtifuano ccm.
Mitifuano akaongee wana ccm wenzake huko ndani vikao akiongea taifa aongee yahusuyo maendeleo sio vijembe.....kuna suala kujenga madarasa na madawati nchi nzima nchi imefunguka.....196bil
 
Ndio nchi yetu ilipofikia hapa, cha msingi ni kila mtu akomae apambane na hali yake asife njaa maana hamna wa kumtegemea
Bila siasa safi ukipambana na hali yako hutoweza kufua dafu:

1.Wanaodhulumiwa haki zao za kidemokrasia wakaamua kuingia mstuni ili kudai haki zao kwa nguvu maana yake amani inatoweka na hutaweza tena kupambana ili mkono uingie kinywani.

2.Viongozi waliokosa kibali cha wananchi wanapoingia madarakani kwa wizi wa kura wanakuwa hawana skills na maarifa ya kuongoza matokeo yake wanakuwa wanapitisha sera zisizosahihi na matokeo yake uchumi unakufa na wewe hutaweza tena kupata kipato katika shughuli zako za uchumi.Imagine Babu Tale ndiye mtunga sheria za nchi.

3.Serikali inayoongozwa na viongozi ambao hawana kibali cha wananchi inakuwa imejaa rushwa na ufisadi kwa hiyo inakuwa ngumu kwa mwananchi wa kawaida kama wewe kupata huduma za kijamii kwa wakati.

4.Ni ngumu sana kuishi bila haki.Haki hutoweka serikali inapokuwa na viongozi ambao hawana kibali cha wananchi.Polisi wakitumwa waje kukukagua kwa mujibu wa sheria wakifika wanakupora badala ya kukukagua.
 
Kwani Biashara Ya Kununua Wabunge Bado Ipo
Huenda Hicho Wanachosisitiza Labda, Membe,Cheyo, Lipumba, Na Wengine Wanarudi Ccm !!

Kila Mtu Anasisitiza Tegeni Sikio, Tutasikiliza Tokea Wapi
Au mbowe anapewa unaibu waziri nini?
 
Aongee jambo lolote lile, lakini ikikosekana kauli ya kumwachia huru Freeman Mbowe basi hataweza kuzikonga roho za wapenda mabadiliko walioukuwa wengi. Pengine amekwisha kutambua ukweli uliopo nyuma ya kesi ile ya ugaidi wa laki sita.

Kupandishwa ghafla cheo kwa jaji anayelisikiiliza shauri hilo la kisheria inaweza kuwa kiashiria kimojawapo. Lakini nchi wahisani, ambazo kupitia balozi zao walidhihirisha wazi kuwa na shahuku juu ya shauri hili, baadhi yao tayari zimeanza kumimina misaada iliyokuwa imekoma katika kipindi cha utawala wa JPM.

Madam President SSH do it now before it becomes too late. Siro na Diwani tupa kule kwa kuwa walikushauri na kukuaminisha vibaya katika suala hili.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Rais sio hakimu wala judge, hana mamlaka hayo, labda sheria zibadilike,
 
Aongee jambo lolote lile, lakini ikikosekana kauli ya kumwachia huru Freeman Mbowe basi hataweza kuzikonga roho za wapenda mabadiliko walioukuwa wengi. Pengine amekwisha kutambua ukweli uliopo nyuma ya kesi ile ya ugaidi wa laki sita.

Kupandishwa ghafla cheo kwa jaji anayelisikiiliza shauri hilo la kisheria inaweza kuwa kiashiria kimojawapo. Lakini nchi wahisani, ambazo kupitia balozi zao walidhihirisha wazi kuwa na shahuku juu ya shauri hili, baadhi yao tayari zimeanza kumimina misaada iliyokuwa imekoma katika kipindi cha utawala wa JPM.

Madam President SSH do it now before it becomes too late. Siro na Diwani tupa kule kwa kuwa walikushauri na kukuaminisha vibaya katika suala hili.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
Unasahau baada ya diwani kuingia, tatizo la watu kwenye sandalusi likaisha?, muwage na kumbukumbu basi
 
TEGENI SIKIO JUMAPILI RAIS SAMIA ANA JAMBO ZITO SANA-MBUNGE DITOPILE

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile leo amejumuika na wanaCCM wenzake katika Kata ya Bulungwa kumuombea kura Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Ushetu Mkoani Shinyanga, Emmanuel Cherehani huku akiwataka watanzania kutega sikio siku ya Jumapili kumsikiliza Rais Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, Ditopile amesema Cherehani ambaye alipitishwa na Chama Cha Mapinduzi kuwa mgombea Ubunge wa Ushetu anatosha na ana sifa zote za kuwa muakilishi wao bungeni.

"Jumapili Mama Samia ana jambo Kubwa na Zito kweli kweli nawaomba wana Ushetu na watanzania kwa ujumla Nchi nzima Mtege Sikio, Mama huyu yupo kazini anahangaika na shida za watanzania, tukae kwenye redio, na TV tumskilize, na tukitoka tukawasimulie wengine.

Tunaye Rais mahiri na shupavu na nyie mmeona anafaa mmempa Uchifu leo kwenye historia ya nchi yetu pamoja na kwamba tuna Rais wa kwanza mwanamke tuna Chifu Mwanamke Chifu Hangaya Samia Nyota inayong’aa "
Mbunge Mariam Ditopile, Ufungaji Kampeni Jimbo la Ushetu,

Nawaomba wana Ushetu watuletee Cherehani kule bungeni nimelelewa na wasukuma najua ukarimu wenu, nitashirikiana naye kule Bungeni hatokuwa mgeni atawapambania kuwaletea maendeleo"
Amesema Ditopile Akimuombea Kura Mgombea Ubunge Kwa Tiketi Ya Ccm Jimbo la Ushetu Leo.

Jimbo la Ushetu limeingia kwenye Uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo na aliyekua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kuandikwa.View attachment 1968598View attachment 1968599View attachment 1968600
Hv kwa tume hii bado mnatumia kodi zetu kuandaa uchaguzi kwa nn msingemutangaz mshindi huyo wa kijan tukoe kodi zetu zikafanya mambo mengine
 
Unasahau baada ya diwani kuingia, tatizo la watu kwenye sandalusi likaisha?, muwage na kumbukumbu basi
Mkuu Elungata utendaji mzuri wa mtu hauangaliwi kupitia kitu kimoja tu, bali kwa kujali miiko ya kazi zake, weledi unaothibika, maadili mema awapo kazini, kutoa ushauri mzuri na awe na hofu kwa Mola wake.
 
Back
Top Bottom