Mariam Ditopile: Rais Samia anazidi kuwafunga midomo waliombeza uendelezaji wa miradi Dodoma

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
867
947
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile amesema Rais Samia ndani ya muda mfupi madarakani anazidi kuwaumbua wale wote waliombeza kuhusu uendelezaji wa miradi ya kimkakati Jiji la Dodoma iliyo asisiwa na Mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Mbunge Ditopile ameyasema hayo leo baada ya Hafla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuweka Jiwe la Msingi mradi wa Ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje katika mji wa Dodoma, Barabara hiyo itatoka Ihumwa-Matumbulu-Nala-Veyula-Ihumwa Kilometa 112.3. Hafla hiyo imefanyika kwenye Sherehe zilizofanyika leo tarehe 09 Februari, 2022 katika eneo la Veyula Jijini Dodoma

"Nampongeza kidhati Rais Samia kwa kuendelea kutimiza ahadi zake kwa vitendo za kuendeleza miradi yote ya kimkakati iliyoasisiwa na Hayati Dkt. John Magufuli Jijini Dodoma, wote ni mashahidi miradi inaendelezwa kwa kasi kubwa sana"

"Yalikuwepo Maneno kwamba Hayati ameondoka na miradi itasimama au haitafanyika lakini sasa ni tofauti, miradi yote inaendelezwa. Mradi huu wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje wa Jiji la Dodoma ni mradi ulisubiriwa kwa Hamu na wana Dodoma utalibadilisha hili jiji letu"

"mradi mwingine unaendelezwa na Rais Samia Jijini Dodoma ni ujenzi wa Hospitali Mpya ya Jiji la Dodoma na tayari Rais Samia ametoa zaidi ya Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wake kuanza, sisi wana Dodoma tunamshukuru na kumpongeza Sana"

"Rais Samia anaonyesha kwa Vitendo anayo nia ya dhati ya kuendeleza miradi yote ya mtangulizi wake, nawasihi watanzania tupuuze maneno ya watu wachache wasioitakia mema Nchi yetu, Rais Samia atatekeleza miradi yote aliachiwa tena kwa kasi kubwa na ufanisi"

"Hii Miradi Mfano Njia mchepuo Kusini Jiji la Arusha 42.4KM
  • Barabara ya Mbinga-Mbamba Bay 66KM
  • Barabara ya Singida-Babati-Minjingu 223.5KM
  • Barabara ya Arusha-Namanga 105KM
  • Iringa- Dodoma 260KM
  • Namtumbo-Tunduru 190KM
  • Mayamaya-Bonga 188KM
  • Tunduru - Mangaka Mtambaswala 202.5KM yote inaendelea kutekelezwa na itakamilika kwa wakati, huyu ndo Rais Samia wa Vitendo sio Maneno"
 
Hio barabara ya dodoma-iringa si ilikamilika muda sana kwani bado inajengwa tena?
 
Tatizo ni hiyo mipasho mipasho utafikiri wanatoa fedha mifukoni mwao,Kumbe kodi za Wananchi.

Wasi wasi Wangu ni kuwa huyu Rais sidhani kama ana MODICUM ya financial intelligence kwani namuona kama anakazana kutumia tu na kugawa mabilioni ya shillings; sijui hata kama ana uhakika hizo fedha anazoahidi kama ziko au haziko!

Mnakumbuka hapa juzi imebidi wachukue fedha za mkopo wa UVIKO kwenda kulipia madeni yaliyoiva!! Hii inaonesha kuwa hawana mipango mizuri ya kuratibu mapato na matumizi ya serikali!!!
 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile amesema Rais Samia ndani ya muda mfupi madarakani anazidi kuwaumbua wale wote waliombeza kuhusu uendelezaji wa miradi ya kimkakati Jiji la Dodoma iliyo asisiwa na Mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli
 
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mhe. Mariam Ditopile amesema Rais Samia ndani ya muda mfupi madarakani anazidi kuwaumbua wale wote waliombeza kuhusu uendelezaji wa miradi ya kimkakati Jiji la Dodoma iliyo asisiwa na Mtangulizi wake Hayati Dkt. John Pombe Magufuli...
Miradi yote uliyotaja ilikamilika kabla Samia hajawa Raisi kuna mingine kabla ya Magufuli. Sijui unatoka nchi gani wewe
 
..kuhamia dodoma ni matumizi mabaya ya kodi zetu.

..fedha zingeelekezwa kwenye miradi ya kilimo, ufugaji, uvuvi, badala ya kujenga ikulu, maofisi, na majumba ya kifahari, kwa ajili ya viongozi wanaohamia Dodoma.
 
..kuhamia dodoma ni matumizi mabaya ya kodi zetu.

..fedha zingeelekezwa kwenye miradi ya kilimo, ufugaji, uvuvi, badala ya kujenga ikulu, maofisi, na majumba ya kifahari, kwa ajili ya viongozi wanaohamia Dodoma.
Dar, kila tumebabana sana. Soon or later ni lazima tuutatue mji. Tuukuze. Watu walikuwa Laku tano, sasa wako milioni tatu.
 
Back
Top Bottom