Maria Sarungi, umefanya mapinduzi. CCM wanalilia mic kwenye space waongee

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
499
1,000
Vyombo vyote vya habari vipo mikononi mwa CCM, ana mamlaka yakusema na kufanya atakavyo. Baada ya kubana vyombo hivyo visiwe na mdahalo huru Maria Sarungi amenzisha mdahalo kupitia mtandao 'space'. Huu umekuwa zaidi ya mkutano wa adhara kwa sababu watu zaidi ya elfu tano wanakusanyika kusikiliza hoja na majibu au ufafanuzi.

Baada ya mashambulizi kuwa makubwa WanaCCM wakiwemo Mawaziri wameanza kulalamika kwanini awqpati nafasi yakuchangia mada hii ikiwa ni yakutafuta wasaa wakujieleza wanakosa wakuwasikiliza kwenye vyombo rasmi.

Kama Mawaziri na wanachama wa CCM pamoja na watu wa dola wanatamani malumbano ya hoja Kama yanayoendelea huko space kwanini wasimweleze Rais akatoa Uhuru wa majadiliano ili vyama na asasi za kiraia watumie vyombo vyetu kueleza na kufafanua mambo Kama ilivyo space? Kibaya zaidi huko lazima tutumie VPN, je kwanini waziri akajiunge VPN kujadili issues ambazo angeweza kujadili public na watu wakasikia?

Maria hongera Sana, umetufumbua macho kwamba hata wao wangependa waongee ila walipowanyamazisha walisau hata wana wangenyamaza maana wangekosa wakuongea naye.
 

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
13,285
2,000
Space wamefanya mapinduzi, maana CCM wamevikaba media zote za kizamani za maandishi, magazeti, radio, televisheni na mitandao-uchwara.

Bora sasa mbali ya Jamiiforums kuna Space ili Bongo zetu huru ziweze kutumika vizuri kama watu huru.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom