Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,671
- 8,237
Wakuu Moja ya marekebisho muhimu sana ya Sheria ya Mwenendo wa Mashitaka ya Jinai, Sura ya 20, (CPA) ya Sheria za Tanzania, yaliyomo katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa Mwaka 2021 ni Kifungu cha 91 (1) ambacho kinampa Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai (DPP) mamlaka ya kumuondolea mashitaka mshitakiwa mahakamani kwa lugha kisheria "nolle prosequi" na kuweza kumkamata tena na kumshitaki kwa mashitaka yale yale yaliyoondolewa na kuyaanzisha upya bila kujali alishakaa mahabusu jela muda mrefu.
Mamlaka hayo ya DPP yalikuwa yanaleta kadhia kubwa sana kwa washitakiwa.
Muswada huo ambao sasa upo mikononi mwa Kamati ya Sheria na Katiba ya Bunge ikipokea na kusikiliza maoni ya wadau, unamlinda mshitakiwa kutokamatwa tena na kushitakiwa kwa makosa yale yale ya awali.
Isipokuwa kuwe na sababu za kuridhisha kwa mahakama na kesi ianze kusikilizwa mara moja bila kucheleweshwa kwa mujibu wa Kifungu cha 131A (1) cha CPA ambacho nacho ni kipya kinachopendekezwa ndani ya Muswada huo, kinachotaka upelelezi uwe umekamilika ndipo mtuhumiwa ashitakiwe.
Hivyo kukomesha kauli zilizozoeleka za waendesha mashitaka (ma-PP) kwamba "upelelezi bado kukamilika" na kutaka kesi kuahirishwa kwa tarehe nyingine za kutajwa na mshitakiwa kurudishwa mahabusu jela.
MAREKEBISHO HAYA YATALETA MANUFAA YAFUATAYO KATIKA HAKI JINAI NCHINI:
1. Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai (DPP) kuhakikisha anafungua mashitaka yenye ukamilifu wa upelelezi.
2. Mahakama itaweza kukataa mashitaka yanayorudishwa tena na waendesha mashitaka kutoka ofisi ya DPP baada ya awali kuyaondoa.
3. Mashitaka hayatachelewa kusikilizwa mahakamani kwa sababu ya upelelezi kutokamilika kwani hati ya mashitaka haitapokelewa na mahakama iwapo upelelezi haujakamilika.
4. Itapunguza msongamano wa mahabusu magerezani kwani wengi husubiri kukamilika kwa upelelezi wa kesi zao.
5. Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kutoka Jeshi la Polisi itabidi awe makini katika ukamataji na upelelezi wa watuhumiwa ikiwemo suala la kubambikia watu kesi ambazo DPP atakosa ushahidi na kumfanya asifungue mashitaka au ayaondoe bila ya kuyarudisha tena.
I Humbly Submit Guys