Marekebisho ya kiuchaguzi au shambulio kwa demokrasia?

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
Ujumbe toka kwa Tundu Lissu: "Muswada wa Matumizi ya Uchaguzi hauna malengo ya kuzuia fedha chafu katika uchaguzi na wala haujadaiwa hivyo na walioutunga. Hakuna kifungu hata kimoja kwenye Muswada wenyewe kinachokataza matumizi ya fedha za wizi au za madawa ya kulevya au za wakwepa kodi katika Uchaguzi. Wala haukatazi fedha za wageni. Hakuna kifungu hata kimoja kinachokataza fedha zinazotoka katika serikali au taasisi za kibeberu au mashirika yake au wananchi wa nchi hizo.

Lengo lake kuu ni kuzuia wapinzani - wawe wa vyama vya siasa au katika civil society - kupata fedha kutoka nje (hata kama ni kutoka kwa raia wa Tanzania walioko Kenya au Uganda!) au kutumia fedha zao wenyewe kama ziko ndani au nje ya nchi yetu. Huu ni Muswada hatari sana na kama kuna anayefikiri wanamtandao wameacha kuwa wanamtandao anaota ndoto au anataka na sisi tuote ndoto!

Naatambatanisha paper niliyoiwasilisha juzi katika Kongamano la DDC Mlimani Park. Nitafurahi kama nitathibitishwa kwamba nimekosea katika uchambuzi na conclusions zangu." Mwisho wa kunukuu

Ps: Nataka nianze kutafsiri uchambuzi husika kwenda kwenye lugha ya kiswahili. Ukiwa tayari nitawaletea. Au kama kuna ambaye unaweza kujitolea kutafsiri kwa haraka zaidi tafadhali anijulishe kupitia mnyika@yahoo.com au 0754694553.

Zingatieni kwamba vikao vya kamati za bunge vinaanza wiki hii, miswada hii nadhani itajadiliwa na kamati husika wiki ijayo. Hivyo, maoni na msukumo wa umma kuhusu suala hili ni jambo la dharura, na ni muhimu usambae kwa wadau wengi iwezekanavyo kwa haraka sana. Kwa jinsi serikali ilivyotangaza inaonyesha dhamira ni kupitisha katika kikao cha bunge kinachoanza karibuni.

Sambamba na muswada huu, pia kuna muswada mwingine wa sheria inayogusa masuala ya 'usalama wa taifa'.

Nawatakia mjadala mwema

JJ
 

Attachments

  • Assault%20on%20Democracy[1].doc
    100.5 KB · Views: 84
Nimeisoma hiyo paper, mapendekezo yaliyomo yanamnyima kabisa mgombea na chama chake haki ya msingi ya kushiriki katika uchaguzi hasa katika msingi wa kutoa na kupokea misaada iwe ya kifedha ama mali nk. Mgombea haruhusiwi kutumia fedha zake binafsi kupokea misaada toka nje miezi mitatu kabla ya uchaguzi isipokuwa toka kwa chama chake tu wala chama hakiruhusiwi kupokea msaada wowote miezi mitatu kabla ya uchaguzi.

Kama ndivyo hivyo naona muswada utainufaisha CCM kwa kiasi kikubwa kutokana na yenyewe kuwa na vyanzo vingi vya mapato, pia Katibu Mkuu wa chama amepewa uwezo wa kutengua jina lolote la mgombea kwenye chama chake hata kama jina litakuwa limeteuliwa kwenye kura za maoni.

Nionavyo mimi CCM imenusa na kuona kuwa kuna uwezekano wa kutokea mtafaruku mkubwa hasa wakati wa kura za maoni sasa inajihami ili iweze kuwadhibiti wale watakaopita kwa mzengwe ndiyo maana imeleta mswada huu. Lakini kwa kufanya hivyo watakaoumia zaidi ni wa vyama vya upinzani maana vinategemea misaada mingi zaidi toka kwa wahisani hasa wa nje.
 
Hivi ni "nani" anayeandika hii miswada "kama huo" inayopelekwa huko bungeni........?
 
Hivi ni "nani" anayeandika hii miswada "kama huo" inayopelekwa huko bungeni........?


Nafikiri serikali inatoa mapendekezo kwa njia ya muswada na kuupeleka bungeni kabla ya kupitishwa na kuwa sheria baada ya kuridhiwa na raisi.
 
Nafikiri serikali inatoa mapendekezo kwa njia ya muswada na kuupeleka bungeni kabla ya kupitishwa na kuwa sheria baada ya kuridhiwa na raisi.


Nadhani swali la Ogah lilikuwa satarical!

Tuendelee na mjadala

JJ
 
Kuna miswada mingi sana iliwahi kuletwa kama na kipindi kama hiki katika kuelekea uchanguzi mkuu, Miswada kama ya Takrima, Sheria ya kupinga matokeo ya uchaguzi na yule anatupasa kuweka kama milioni 5 hivi. Mimi naona mambo kama haya watu wote kwa pamoja inatupasa kukataa kufanya mambo ya ajabu. Na pia serikali kama ndio hivyo itoe fedha kwa wagombea wote kupitia vyama vyao na CCM iachane kutumia dola na kuwa chama dola ili kuwa na fair ground kwa vyama vyote, hali itakuwa mbaya sana kwa vyama vya upinzania
 
Mimi huwa najiuliza hivi kwa nini hii miswaada huwa inaletwa kipindi cha mwisho kabisa muda mfupi kabla ya uchaguzi wana ajenda gani walikuwa wapi kipindi cha miaka mitano? basi kama ndo mchezo wenyewe huu itakuwa kila kabla ya uchaguzi sheria zinabadilika kutokana una upepo wa kisiasa ndani ya CCM, huu mchezo wa kucheza na sheria si mzuri kabisa mwisho wataingilia katiba shame on you.
 
Jamani.let us discuss critically,this is a very serious issue.Tusipojadili kwa mapana haki ya nani CCM watatawala milele.Huu mswada ni mgumu sana kwa vyama vya upinzani,ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano kuliko kwa vyama vya upinzani kushinda uchaguzi huu kama mswada huu utakuwa sheria.mwenye masikio na asikie.
 
Back
Top Bottom