Marekebisho ya kisheria yafanyike kulinda haki wakati wa uteuzi wa wagombea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekebisho ya kisheria yafanyike kulinda haki wakati wa uteuzi wa wagombea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by John Mnyika, Jan 23, 2010.

 1. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Uteuzi wa Wagombea upo katika ngazi mbili: Uteuzi wa Wagombea katika Vyama na Uteuzi wa Wagombea katika Tume ya Uchaguzi. Uteuzi wa ndani ya vyama unasimamia na katiba, kanuni na taratibu za vyama husika. Ni kawaida katika siasa za uteuzi ndani ya vyama kutawaliwa na ushindani mkubwa; lakini ieleweke kuwa kuna tofauti kati siasa chafu na siasa za ushindani. Siasa zenye ushindani chanya zinasababisha uteuzi wa wagombea ambao wenye uwezo kiuongozi mathalani elimu, uzoefu na dira. Siasa za ushindani hasi hupelekea kupatikana kwa wagombea ambao ushindi wao umetokana na rushwa, upendeleo, kupakana matope, udini, ukabila nk. Kwa mfano, uteuzi wa ndani ya CCM uligubikwa na ‘takrima’ na siasa za kupakana matope katika maeneo kadhaa ikiwemo kuanzia ngazi ya udiwani mpaka ya Urais. Mathalani inatajwa jinsi Salim Ahmed Salim (aliyekuwa Katibu Mkuu wa OAU) alivyopakwa matope (kwa mujibu wa Ripoti ya Uchaguzi Mkuu 2005 ya TEMCO). Ilifikia hatua Fredrick Sumaye, mmoja wa wagombea (ambaye pia alikuwa Waziri Mkuu wakati huo), akiwa analaani jinsi ambavyo anapakwa matope alitamka bayana kwamba “anayesafisha njia kwa kalamu, atatawala kwa risasi”.

  Makala inaendelea hapa: http://mnyika.blogspot.com/2010/01/marekebisho-ya-kisheria-yafanyike.html
   
 2. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  lakini bwana mnyika unaonaje? sheria hiyo hiyo unayozungumzia ikawa na uwakilishi wa makundi yote ndani ya jamii hususani katika uwakilishi wa bunge letu,hapa namanisha kila chama cha kisiasa kipewe idadi sawa ya viti kisha makundi ya kijamii,hivyo kazi ya kuomba kura irudi kwenye hayo makundi,hauoni tutapunguza pesa nyingi zinazopotea kwenye chaguzi huku watu wakifa na njaa?,labda nikuulize wewe mwenyewe ulitumia shilingi ngapi? ulipokuwa unataka ubunge wa ubungo?
   
 3. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  umenipata kaka
   
 4. k

  kimboka one JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2010
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 734
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  jamani watanzania nisadieni lipi? jana kuteuwa wabunge kutoka kwenye makundi ya kijamii au kuendelea kutumia mamilioni kwa kampeni za kura za pamoja,pesa tunazo ibiwa kutoka kwenye stahiki zetu za madawa hospitali na ujenzi wa mashule na kungine kwingi
   
 5. John Mnyika

  John Mnyika Verified User

  #5
  Jan 23, 2010
  Joined: Jun 16, 2006
  Messages: 715
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Kuhusu kiwango cha fedha, kampeni zangu zilitumia kiasi kisichozidi milioni 20. Suala unalolizungumzia ni tofauti kidogo. Unazungumzia mfumo wa uchaguzi. Kwa mawazo yako, wewe unaamini katika mfumo wa uwakilishi wa uwiano. Nchi yetu inatumia mfumo wa wengi wape(mshindi anachukua vyote) ndio maana kuna matatizo ambayo umeyadokeza hususani katika uchaguzi wa marudio. Kwa maoni yangu, tulipaswa kuwa na mfumo wa mchanganyiko wa uwakilishi wa uwiano lakini pia mfumo huu wa uchaguzi wa majimbo moja kwa moja.

  Kwa maoni yangu hili linaweza kutekelezeka bila kuongeza ukubwa wa bunge lakini wakati huo huo makundi ya kijamii yakawakilishwa bungeni. Mathalani, tunaweza kuamua kwenye sheria badala ya mfumo wa sasa wa mgawanyo wa majimbo- wilaya/halmashauri ndio ziwe majimbo pia. Kwa njia hii, tutakuwa na majimbo sawa na idadi ya wilaya(133-139), halafu nafasi zilizobaki zikagawanywa kwa kura za uwakilishi wa uwiano. Jambo hili la mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi hayajaguswa katika marekebisho ya sheria ya uchaguzi yaliyotolewa.

  Unaweza kupata majibu zaidi kwa swali uliloniuliza kwa kusoma makala hii:http://mnyika.blogspot.com/2008/11/tubadili-mfumo-wa-uchaguzi-kupata.html

  Hata hivyo, unapoisoma uzingatie kuwa kile ambacho CCM ilikiahidi kukitekeleza wakati huo kubadili sheria kupanua uwakilishi wa wanawake kufikia 50-50 haijakitelekeza na serikali imeonyesha wazi kuwa haitakitekeleza. Na hata ndani ya marekebisho ya sheria hakipo tofauti na kauli ya Rais Kikwete.

  JJ
   
Loading...