Marekebisho sera ya elimu(MUHIMU)

Mzee wa Gumzo

Senior Member
Apr 21, 2008
197
5
"SERIKALI ipo katika mchakato wa kuifanyia marekebisho makubwa sera ya elimu na mafunzo ya ufundi, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Gaudentia Kabaka, aliliambia Bunge jana.
Akijibu swali la nyongeza la Goerge Simbachawene (Kibakwe-CCM), Kabaka aliwataka wadau wote wa elimu ambao wana maoni kuhusu sera hiyo, wayapeleke wizarani ili yajumuishwe katika mchakato wa mabadiliko hayo.
Alitoa jibu hilo baada ya Simbachawene kuitaka serikali kuruhusu wanafunzi wanaofeli mitihani ya darasa la saba, wakariri darasa kwani elimu ni haki ya msingi ya kila Mtanzania kama inavyoelezwa katika katiba."


Haya jamani wadau wa elimu wakati ndio huu tuyapeleke maoni wizarani.
Tukumbuke kuwa kwa muda mrefu tumekuwa tukilalamikia sera mbovu ya elimu Tanzania ambayo hailengi kumsaidia mtoto wa kimasikini na aliyeko katika mazingira duni kufaidi elimu anayoipata.

Tunataka elimu ya msingi iwe inatoa stadi za ufundi kusudi mtoto anayekosa nafasi ya kuendelea na elimu ya sekondari kuweza kuyakabili mazingira yake kwa kutumia ujuzi atakao kuwa ameupata.

Kwa ujumla yapo mambo mengi kuhusu elimu tunayotakiwa kuyajadili na kupendekeza marekebisho kwenye sera ya elimu.

Tufungue mjadala hapa na tupeleke maoni wizarani kwa manufaa ya taifa letu!
 
Back
Top Bottom