Marekani yazuia mali za Makamu wa Kwanza wa Rais wa Sudani Taban Deng Ga

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,811
4,533
1578554208851.png
Serikali ya Washington imeamua kumuadhibu Makamu wa Kwanza wa Rais, Taban Deng Gai. Marekani inaendelea kuiwekea shinikizo Juba wakati mchakato wa amani unaendelea kucheleweshwa.

Serikali ya Umoja imepangwa kuundwa hadi mwezi Februari.

Wizara ya Fedha imeamua kuzuia mali za Taban Deng Gai nchini Marekani. Pia imepiga imarufu Raia yeyote wa Marekani kufanya shughuli naye.

Marekani haijawahi kuchukulia hatua dhidi ya Afisa wa Ngazi ya Juu katika Serikali ya Sudani Kusini. Baada ya maafisa watano wa ngazi ya chini na mawaziri wawili, hatimaye Marekani imemchukulia vikwazo Taban Deng Gai, na hivyo viongozi wa juu katika serikali hiyo kuwa mashakani.

Makamu wa kwanza wa rais, 69, ni maarufu nchini Sudan Kusini na ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa nchini humo. Aliwahi kuhudumu kama mkuu wa Jimbo la mafuta la Unity, kisha waziri wa Madini, na alijiunga na waasi wa Riek Machar wakati vita vilipoanza.

Lakini wakati mzozo ulipoanza tena mnamo mwaka 2016, Taban Deng Gai alijitenga na Riek Machar na kuamua kujiunga na rais Kiir kabla ya kuteuliwa kwenye nafasi ya makamu wa kwanza wa rais. Hivi sasa ana kundi lake la wapiganaji na kambi ya Riek Machar inamwona kama msaliti.

Kwa mujibu wa Wizara ya fedha ya Marekani, Taban Deng Gai ana hatia ya ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu. Alihusika katika kisa cha kutoweka kwa na kifo cha wakili Samuel Dong Luak na mpinzani Aggrey Idry.

Washington imesema makamu wa kwanza wa rais anataka kuimarisha msimamo wake, kuchochea machafuko kati ya wapinzani kwa kuzuia Riek Machar kurudi nchini.


Chanzo:RFI
 
Back
Top Bottom