42774277
JF-Expert Member
- Aug 24, 2018
- 6,833
- 8,811
Kesho kukikucha US atakuwa ashagongwa cases 100k
Wakati China imekuwa ikishika namba 1 bila mpinzani kwa miezi kadhaa, huku ikinuswa nuswa na Italy, watu wengi tulidhani kuwa Italy ndiyo itashika nafasi ya China siku chache zijazo. Lakini mambo yamekuwa tofauti mno.
Kwa ghafla Marekani imempita Italy na hapo hapo ikampiku China. Kwa sasa Marekani imefikisha zaidi ya visa vya corona 83,000, ikifuatiwa na China yenye visa takriban 81,000 huku Itali ikishika nafasi ya tatu kwa kuwa na visa takriban 80,500.
Hata hivyo kasi ya maambukizi nchini Italy ni kubwa mno, huwenda ikaipiku China ndani ya siku mbili tatu.
Update 27 March.
Visa vya corona nchini US vimefikia zaidi ya 96,000 huku zaidi ya vifo 1450 vikiripotiwa.
Italy imeipiku China, ikirikodi visa takriban 86,000 wakati china ikiwa na visa karibu 81,000. Kwa hiyo Italy imekuwa namba 2.
Kwa mujibu wa Utafiti uliofanyika University of Washington, inakadiriwa kuwa mpaka July (ndani ya miezi minne hivi) vifo vya corona nchini US vitakuwa wastani wa 91,000.
Katika uchambuzi wa data, utafiti huo umeainisha kuwa vifo hivyo vyaweza kufikia hadi 162,000.
View attachment 1401241
View attachment 1401246