Marekani yatuma salamu za muungano kwa Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekani yatuma salamu za muungano kwa Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Apr 26, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Tafakari yangu:

  Zipo changamoto nyingi za muungano ambazo mara zote zinapozungumzwa tu zinatafsiriwa kama "kero za Muungano". Muungano wetu daima umeonekana kama ni "ndoa" iliyounganisha nchi mbili yaani Tanganyika na Zanzibar iliyozaa mtoto aitwae "Tanzania" na wakati huo huo akiwepo mtoto mwingine aitwaye "Zanzibar".

  Kwa kutambua dosari za kiutawala ndani ya muungano, waasisi wa Muungano pia walionelea pia kuunganisha vyama vya siasa kwa wakati huo yaani TANU na ASP ambavyo vilizaa mtoto " Chama cha Mapinduzi (CCM). Ni mwaka hu huo 1977, Katiba ya Jamhuri ya Muungano ilipitishwa ikiwa imebeba pamoja na mambo mengine yale yaliyofikiwa katika Makubaliano ya Muungano ya Mwaka 1964 "Articles of Union".

  CCM alishika hatamu ya uongozi wa Serikali mpaka aliporuhusu kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa mwaka 1992 na kwa nia ya kulinda Muungano, miongoni mwa masharti kwa vyama vyote vya siasa kwa mujibu wa Sheria ya Vyama vya Siass ni kuhakikisha Muungano unadumu kwa kuwa na itikadi isiyopingana na Muungano na kukubalika zinazokubalika na wananchi wa pande zote mbili za muungano (Tanzania Bara na Visiwani).

  Hata hivyo, ndani ya Katiba yetu na pia mfumo mzima wa uongozi na utawala, bado zipo dosari nyingi sana ambazo zinafanya muungano wetu kuonekana una mapungufu na hatua za lazima za kushughulikia dosari hzo si kupuuza au kuhairisha yale ambayo wanasemwa na wananchi kuwa ni mapungufu...au pengine, si kujaribu kutegeneza mazingira ya kuwatishia na kuwakemea vikali wale ambao wanajaribu kubainisha mapungufu hayo na kuwaona kama wao ni "wahaini, wapotoshaji au wasioutakia mema muungano au kutozienzi fikra sahihi za viongozi wetu na waasisi wa Muungano".

  Mungu ibariki Tanzania,

  Mungu ibariki Zanzibar,

  MUngu Ubariki Muungano.
   
 2. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,359
  Likes Received: 3,124
  Trophy Points: 280
  haya bana............ngoja tuendelee kusaidiana!!!!!!!!!!!
   
 3. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mkuu kwa mtazamo wangu binafsi huu muungano ulibidi uwe hivyo au uundwe ulivyo kipindi kile na namna ya kuuboresha siyo kuunda serikali tatu wala kuendelea kuuzunguka ukweli. Kinachotakiwa kwa kizazi kijacho ni kuamua kuunganisha nchi iwe na Raisi mmoja, serikali moja, bendera moja, mawaziri wa serikali moja, sheria moja nchi nzima na bunge moja tuuu! Kila Mkoa uwe na haki ya kuchagua viongozi wake na wawakilishi ndani ya serikali kuu-bungeni, Zanzibar, Pemba zikiwakilishwa kama mikoa. Tuunde Shirikisho in other words. Hapo ndipo tutakuwa tumewaenzi waasisi wa Muungano na ndipo tutakuwa imara kama URT.

  Bila busara zetu kutufikisha hapo huu muungano ni wa kujadili 24/7 na hakuna kitakachoeleweka.
  I SEE THAT AS A SOLUTION!!
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Apr 27, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Ngoshwe usiwe naive kiasi hicho. Hizi ambazo zinaitwa kero zilianza kidogo kidogo, zimekuzwa kijanja janja mpaka watu wamefikia kuhoji uhalali wa Muungano wenyewe! Lengo hasa ni kuingia IKULU si vinginevyo! Kusaini mkataba wa Muungano wazanzibari walikubali, mabadiliko yote ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano tangu mwaka 1977 hadi leo yaliridhiwa na wazanzibari na Watanzania Bara, sasa iweje Wazanzibari wanalalamika kama vile hawakuwepo miaka yote hiyo? Usichukuliwe na upepo wa wanasiasa ndugu yangu, tafakari kwa kina kama msomi, utaelewa!
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  MODs, ondoa hii thread. haina umuhimu wowote kujadiiliwa humu JF.
   
Loading...