Marekani yatuhumiwa kuchochea vita


jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Messages
295
Likes
12
Points
0
jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2010
295 12 0
Kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran Ayatollah Ali Khamanei hii leo akijibu shutuma za Marekani kuwa Iran inaelekea kwenye udikteta wa kijeshi,ameituhumu Marekani kuwa inachochea vita.
Matamshi ya Ayatollah Ali Khamenei ni ishara mpya ya mivutano inayozidi kuongezeka kati ya Tehran na Washington kuhusiana na mradi wa nyuklia wa Iran unaohofiwa na nchi za Magharibi kuwa unalenga kutengeneza silaha za nyuklia. Akiashiria ziara iliyofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton mapema juma hili katika Mashariki ya Kati, Khamenei amesema kuwa Marekani imemtuma wakala wake katika kanda hiyo kuishutumu serikali ya Iran iliyo na mfumo wa Kiislamu. Lakini hakuna anaeamini uongo unaoenezwa kwani wanafahamu kuwa Marekani ni mchochea vita na kuongezea kuwa eneo la Ghuba limefanywa ghala ya silaha. Wamezivamia Afghanistan na Iraq na sasa wanaituhumu Jamhuri ya Kiislamu amesema kiongozi mkuu wa kidini wa Iran.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton.
Lakini mapema wiki hii, Clinton alipokuwa ziarani nchini Qatar na Saudi Arabia alikanusha kuwa Marekani ina njama ya kuishambulia Iran. Amesema, Washington inataka kujadiliana na Tehran lakini haiwezi kubakia kimya wakati Iran ikiendelea na mpango unaoshukiwa kuhusika na silaha za nyuklia. Nchi za magharibi zinapaza sauti kuiwekea Iran vikwazo vipya hasa baada ya Rais Mahmoud Ahmedinejad juma lililopita kutoa amri ya kuanza kusafisha madini ya uranium kwa kiwango cha juu. Marekani inashika bendera katika kulihimiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liweke vikwazo ziada dhidi ya Iran. Lakini Iran inashikilia kuwa azma ya mradi wake wa nyuklia ni kupata umeme zaidi ili iweze kusafirisha mafuta na gesi zaidi kutoka nchi hiyo. Ikisisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya amani tu,vile vile imeonya kuwa itajibu shambulio lo lote litakalofanywa dhidi yake. Mwezi uliopita, maafisa wa Marekani walisema kuwa Washington imeimarisha mfumo wake wa ulinzi kwenye nchi kavu na baharini katika eneo la Ghuba ili iweze kukabiliana na kile kinachotazamwa kama kitisho kinachozidi kuwa kikubwa kuhusu makombora ya Iran. Eneo hilo la Ghuba ni muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani. Kwa upande mwingine, vyombo vya habari nchini Urusi vimemnukulu Mnadhimu Mkuu wa nchi hiyo, Jemadari Nikolai Makarov akidai kuwa Marekani inadhamiria kuishambulia Iran. Yeye amenukuliwa akisema kuwa mwenyekiti wa majeshi ya Marekani, Admeri Michael Mullen, hivi karibuni alizungumzia mpango huo. Mwandishi: Martin,Prema/ RTRE/APE Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed

http://www.dw-world.de/dw/article/0,,5259045,00.html
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Hivi lini wataanza vipi na iran hawa Americans? waanze tu waongeze idadi ya marehemu askari na askari wasio na akili maana statistics za askari matahira kwasababu ya vita huko iraq ni kubwa sana...
 
G

gudlack

Member
Joined
Oct 11, 2009
Messages
43
Likes
0
Points
0
G

gudlack

Member
Joined Oct 11, 2009
43 0 0
kwani ulitarajia aseme nini sasa??? nyie si wamoja na huyo Ayatollah???kila siku ananyonga watu yeye hajioni, wale walioandamana mbona walinjongwa mbaina hakuwatetea????
 
jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2010
Messages
295
Likes
12
Points
0
jamadari

jamadari

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2010
295 12 0
Iran na dimba la Ujerumani magazetini

Rais wa Iran achezea moto wasema wahariri wa Ujerumani

Mkutano wa usalama mjini Munich, na kinyang'anyiro cha madaraka katika shirika la kabumbu nchini Ujerumani DFB ni miongoni mwa mada zilizochamabuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo.

Tuanzie lakini Munich ambako wahariri wanahisi Iran imelitumia jukwaa la mkutano wa usalama wa kimataifa ili kuicheza shere jumuia ya kimataifa.Gazeti la " NORDWEST-ZEITUNG la mjini Oldenburg" linaandika:

"Lilikua pigo jengine hilo.Vuta nikuvute kuhusu mradi wa kinuklea wa Iran inaingia katika awamu nyengine.Hata kama watu walikua tayari kuziamini ahadi za utawala wa mjini Teheran za kushirikiana na jumuia ya kimataifa,utayarifu huo hivi sasa umechujuka kutokana na hotuba ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Iran katika mkutano wa usalama mjini Munich.Iran haijaachana na mipango yake ya kutaka kujitengenezea silaha za kinuklea.Kwa mara nyengine tena mvutano umezidi makali.Wakati umewadia sasa,sio kuzungumzia juu ya shambulio la kijeshi,bali hasa kusaka uungaji mkono wa walio wengi ili kuiwekea vikwazo zaidi serikali ya mjini Teheran.Jumuia ya kimataifa na jumuia ya kujihami ya Magharibi NATO zinajikuta njia panda hivi sasa.

Gazeti la NORDBAYERISCHER KURIER la mjini Bayreuth linahisi rais Ahmedinedjad anacheza na moto.Gazeti linaendelea kuandika:

Rais wa Iran anacheza mchezo mbaya sana:Kwanza anazusha matumaini na muda si muda anayamwagia mchanga.Anamtuma waziri wake wa mambo ya nchi za nje katika mkutano wa usalama mjini Munchen ili kuleta mfarakano ndani ya jumuia ya kujihami ya magharibi.Mara senetor wa Marekani Joe Liebermann akaishiwa na subira na kutishia Teheran itahujumiwa kijeshi.Ahmadinedjad anatanga tanga kwasababu nchini mwake kunatokota.Wananchi wa Iran na hasa wale ambao hawaungi mkono msimamo wa mayatollah,hawataki kufuata mkondo wa vita ,wakihofia usije ukawaangamiza.Ishara za kupalilia mivutano zimechomoza mwishoni mwa wiki.Wananchi wa Iran hawajui wafanye nini,wanataraji tuu kwamba wenye usemi wataepukana na balaa la mgogoro wa kijeshi.

Mada yetu ya pili magazetini inahusu mvutano ndani ya shirikisho la kabumbu la Ujerumani DFB.Gazeti la Stuttgarter Zeitung linaandika:

Kilichohanikiza magazetini mnamo siku za hivi karibuni,kuhusiana na madai ya kurefushwa mkataba wa kocha wa timu ya taifa Joachim Löw na meneja wa timu ya taifa ya kabumbu Oliver Bierhoff,kinabainisha ukosefu wa kutambua hali namna ilivyo,upotofu na kiu ya madaraka na mali.Pekee fedheha iliyosababishwa na pande zote mbili, ni sababu ya kutosha,kuwafukuza wote wahusika.Hata wakati wa enzi za mwenyekiti wa zamani wa shirikisho la kambumbu la Ujerumani DFB,Gerhard Mayer-Vorfelder ,habari za kuudhi zilikua zikivuja toka makao makuu ya soka la Ujerumani mjini Frankfurt-lakini katika enzi za sasa za aliyeshika nafasi yake Theo Zwanziger,jungu la njama na fitna laonyesha kuzidi kutokota.Mwandishi:Hamidou,Oummilkheir /Dt Presse

Mhariri:Abdul-Rahman

http://www.dw-world.de/dw/article/0,,5226032,00.html
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
kwani ulitarajia aseme nini sasa??? nyie si wamoja na huyo Ayatollah???kila siku ananyonga watu yeye hajioni, wale walioandamana mbona walinjongwa mbaina hakuwatetea????
Wanaoandamana ni vibaraka wa wamerakani, hata wamerakani wahalifu wanaohujumu nchi inawafunga au kuwanyonga so kila nchi kuna sheria zake inabidi wafuate au wakae kimya..
 
MaxShimba

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Messages
35,816
Likes
139
Points
160
MaxShimba

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2008
35,816 139 160
Viongozi wa dini zingine bana. Badala yakufundisha watu deen, sasa ni wana siasa. Yaani nchi imesilimu na kuwa na deen.

Sasa sijui Muislamu ni mfuasi wa nani, allah, Muham-mad, Islam, au Koran?
 
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Messages
967
Likes
20
Points
0
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2009
967 20 0
Tumaini huko uliko usije ukajilipua kama suicide bomber maana utaharibu jina la Tanzania.Una chuki kali moyoni mwako.Usije ukawa kama Abdulmuttalb ,aliyeficha bomu kwenye underwear!Ameharibu sifa ya Nigeria zaidi na zaidi,sasa hata student hawapati visa kwenda kusoma nje.
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Tumaini huko uliko usije ukajilipua kama suicide bomber maana utaharibu jina la Tanzania.Una chuki kali moyoni mwako.Usije ukawa kama Abdulmuttalb ,aliyeficha bomu kwenye underwear!Ameharibu sifa ya Nigeria zaidi na zaidi,sasa hata student hawapati visa kwenda kusoma nje.
Sifa ya Tanzania? pole sana mimi ni Muislamu Tanzania comes second
 
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Messages
967
Likes
20
Points
0
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2009
967 20 0
Tumaini ukijilipua na kuua watu ,watu watakutambua umetoka wapi,utaharibu jina la Tanzania!Uislamu wako ni juu yako
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Tumaini ukijilipua na kuua watu ,watu watakutambua umetoka wapi,utaharibu jina la Tanzania!Uislamu wako ni juu yako
Pole sana ndugu siwezi kujilipua ila nitasema ukweli
 
MaxShimba

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2008
Messages
35,816
Likes
139
Points
160
MaxShimba

MaxShimba

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2008
35,816 139 160
Sifa ya Tanzania? pole sana mimi ni Muislamu Tanzania comes second
Naona uzalendo umekushinda. Deen kwanza! sasa wewe kama Muislamu ni mfuasi wa nani? Maana hata nchi kutokana na deen yako inaweza kuwa Islamu! Astakafulahi.

Wewe unafuata nani, allah? Marehemu Muham-mad? Koran ya Gibril? au Imani ya Islamu?
 
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2009
Messages
7,236
Likes
326
Points
180
Utingo

Utingo

JF-Expert Member
Joined Dec 15, 2009
7,236 326 180
Sasa sijui Muislamu ni mfuasi wa nani, allah, Muham-mad, Islam, au Koran?
Max tambua kuwa ni wafuasi na wana wa Baba wa Uongo ---jibu unalijua
ndiyo maana ni confusion on what to follow, allah, Muham-mad, Islam, Koran, au Ayatollas, the Mullas and their contemporary prophet Osama bin Laden.
Islam is a tradition but people have made it religion ndiyo maana wamechanganyikiwa hawajui wafuate nini. Hata ukiwaambia wavae mabomu wajilipue kwa kuua ng'ombe za wasio waislamu na wakifanya hivyo watakwenda akhera (maana wao paradiso ni ndoto) they will do it. It is a Middle Eastern New Age Movement- It has nothing to do with God, but what pleases your heart and feelings.

It is all Hoaxes
 
B

Bull

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2008
Messages
984
Likes
0
Points
0
B

Bull

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2008
984 0 0
Mbona mnashangaa shangaaa, Nani asiejua kuwa America na western coutries ndio wanao palilia vita africa na around the world?

Mbona mnaishushia hadhi jf? anayosema Ayatollah sio kigeni, dunia nzima wanaelewa hili, hivi nyie vipi?
Wamarikani ku-support vita duniani haliitaji kuwa muislam kulitambua, hata wakiristo wengi wanalijua haliitaji uwe na dini

America is biggest terror in the world!! hivi kuna kunguwani hapa jf asie jua hili ?
 
Kubwajinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2008
Messages
2,190
Likes
21
Points
135
Kubwajinga

Kubwajinga

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2008
2,190 21 135
Sifa ya Tanzania? pole sana mimi ni Muislamu Tanzania comes second
Wewe kijana itabidi Usalama wa Taifa wakutembelee. Kama loyalty yako iko kwa Ayatolah n.k. kuliko nchi yako, ni wazi kuwa u-mtu hatari sana kwa Taifa. Nawasilisha hoja kwa Usalama wa Taifa ili watumie njia yoyote ile kupata IP Address ya Tumain na kumtambua, kabla hajatulipua.
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Wewe kijana itabidi Usalama wa Taifa wakutembelee. Kama loyalty yako iko kwa Ayatolah n.k. kuliko nchi yako, ni wazi kuwa u-mtu hatari sana kwa Taifa. Nawasilisha hoja kwa Usalama wa Taifa ili watumie njia yoyote ile kupata IP Address ya Tumain na kumtambua, kabla hajatulipua.
Mhh! Mmeshaanza kutishia watu hampendi kusikia other view, uislamu siyo ayatolla ndugu...pole sana kwa kuwa uko terrified!
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Naona uzalendo umekushinda. Deen kwanza! sasa wewe kama Muislamu ni mfuasi wa nani? Maana hata nchi kutokana na deen yako inaweza kuwa Islamu! Astakafulahi.

Wewe unafuata nani, allah? Marehemu Muham-mad? Koran ya Gibril? au Imani ya Islamu?
Nafuata uislamu period!
 
X-PASTER

X-PASTER

Moderator
Joined
Feb 12, 2007
Messages
11,649
Likes
134
Points
160
X-PASTER

X-PASTER

Moderator
Joined Feb 12, 2007
11,649 134 160
Nchi za kimagharibi zikiongozwa na Marekani hazinabudi kuukubali ukweli kwamba Iran sasa ni nchi yenye teknolojia ya nyuklia.
Hizi sera za sasa kutoka Washington dhidi ya Iran, pamoja na juhudi za kulazimisha Iran kuwekewa vikwazo zaidi vya kiuchumi ni kwa faida ya Marekani tu. Na baadhi ya nchi zimeshashtukia.
 
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2009
Messages
967
Likes
20
Points
0
M

mmakonde

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2009
967 20 0
Kubwajinga,Bull na mwenzake Tumaini ni Islamists.tatizo Ulaya imekaribisha watu kama hawa wengi sana,wengi ni scum bags,they dont work na kuchuka benefits tu.
Ukiangalia posts za Tumaini unajua hate aliyonayo.Uzuri amesema yeye ni mwislamu zaidi kuliko Mtanzania.tatizo ni kwamba akijilipua kwa bomu na kuua watu ,watamtambua kuwa ni Mtanzania!Atazibia watu wengi ambao wanataka kutafuta maisha mazuri na familia zao nchi za magharibi!
 
M

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2008
Messages
241
Likes
0
Points
0
M

Mzee Kibiongo

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2008
241 0 0
Hebu niulize.......Ina maana Marekani hawana silaha za nuclea ??? Mbona wameshupalia wenzao. Tatizo ni kwamba ulimwengu mzima unawaogopa. Tangu walipotafuta silaha za maangamizi Iraq mpaka leo hazijapatikana halaru UN na dunia nzima kiiiiiiiiiiiiiiiiiiiimyaaaaaaaaa.

Ila mwenzetu Tumain alikwisha sema huko nyuma kwamba yeye ni Mwajemi na kwamba anaogopa kurudi kwao kwa kuwa hakukaliki. Hivyo msimshangae siku moja akileta maafa ya kujilipua. Achunguzwe huyo.
 

Forum statistics

Threads 1,238,902
Members 476,226
Posts 29,336,151