Marekani yasisitiza kuiadhibu Korea Kaskazini Muda wowote kabla ya 2018

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,635
29,967
_98994816_ac1fc16b-56bf-4cbb-a8ce-2225f32c2e4f.jpg

Marekani imeyataka mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la masafa marefu.

Akizungumza katika baraza la usalama la umoja wa kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo Nikki Haley amesema kuwa rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa mafuta kwa Pyongyang.

Amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea Kaskazini itaangamizwa iwapo vita vitazuka.

Onyo hilo linajiri baada ya Pyonyang kufanyia majaribio kombora lake la kwanza katika kipindi cha miezi miwili.

Marekani: Korea Kaskazini ilikusudia uchokozi

Marekani yailalamikia Korea Kaskazini

Marekani yatishia kuiadhibu Korea Kaskazini

Korea Kaskazini imesema kuwa kombora hilo lililorushwa siku ya Jumatano ambalo inasema liliruka kimo cha kilomita 4,475, ikiwa ni mara kumi zaidi ya kimo cha kituo cha angani.

Madai hayo hayakuthibitishwa na wataalam wametiliashaka uwezo wa taifa hilo kuwa na teknolojia kama hiyo.

Hatahivyo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uzinduzi wa kombora hilo ulikuwa wa kufana.

Jaribio hilo likiwa mojawapo ya majaribio yaliofanywa na taifa hilo limeshutumiwa na jamii ya kimataifa na tayari baraza la usalama la umoja wa kimataifa limeitisha kikao cha dharura.

Bi Haley alionya kuwa kuendelea kwa uchokozi kunalenga kuliyumbisha eneo hilo.

''Tunahitaji China kuchukua hatua zaidi'', alisema.

Rais Trump alimpigia simu rais Xi Jinping mapema siku ya Jumatano , Ikulu ya Whitehouse ilisema kuwa rais Trump alizungumza na Xi Jinping kwa simu akimtaka kuchukua hatua zozote kuishawishi Korea Kaskazini kusitisha uchokozi na kusitisha mpango wake wa kinyuklia.
 
Kuna siku hapa ndani wengi wataukana upande wa Pyongyang........kwenye kumbukumbu zangu hakuna siku hata moja hawa jamaa marekani wamekurupuka kwenye vita...muda woote wanajivuta lakini wakiamka wameamka
Anasema hawataki kumwaga damu
 
Kuna siku hapa ndani wengi wataukana upande wa Pyongyang........kwenye kumbukumbu zangu hakuna siku hata moja hawa jamaa marekani wamekurupuka kwenye vita...muda woote wanajivuta lakini wakiamka wameamka
Watageuza tena maneno; watapiga mayowe anaonewa! Team Kiduku ni wa ajabu kidogo. Mkuu wewe unaielewa vizuri Amerika; namwona Secretary of Defense na timu yake wakipiga kazi 18 hours a day to explore "different options" kabla ya kuzifikisha mezani pa Commander-in-Chief kwa ajili ya maamuzi ya mwisho. Sasa wanywa viroba humu wasiojua hata mkuki unashikwaje kelele tupu; wanadhani vita ni sawa na mdundiko.

Jambo lisilo na shaka ndani yake ni kwamba Kim anaenda kufanyiwa kitu mbaya no matter what; ni suala la muda tu; kwamba Kim atapigwa sio suala la mjadala.
 
Iraq ilikua namna hii hii....watu wakasema aaah hamna kitu..mara hiki na kile..filimbi ilivyopulizwa tu jumba jeupe pale.....7days watu washakimbilia kwenye mashimo kama bata bukin
 
hio vita ikipigwa ndo itakuwa vita ya 3 ya dunia na ikimalizika dunia itayumba kiuchumi na hapo ndo lengo la kuwa na dini moja, chama kimoja, siku moja ya kuabudu na utawala mmoja utatangazwa na hapo ndo shetani ataanza kutawala
 
Akili za kuaminibushirikina zikiathiriwa na ushrikina uwa taabu sana
 
Kuna siku hapa ndani wengi wataukana upande wa Pyongyang........kwenye kumbukumbu zangu hakuna siku hata moja hawa jamaa marekani wamekurupuka kwenye vita...muda woote wanajivuta lakini wakiamka wameamka
Ataamkaje kwa mtu ambaye ana nuclear weapons anahesubili kadi ya mwaliko tu ili atambulike rasmi kwenye ligi......
 
Kuna siku hapa ndani wengi wataukana upande wa Pyongyang........kwenye kumbukumbu zangu hakuna siku hata moja hawa jamaa marekani wamekurupuka kwenye vita...muda woote wanajivuta lakini wakiamka wameamka
Marekani hupima kina cha maji kwanza kabla ya kujitosa! Tangu enzi za bush walishapima maji ya korea kaskazini wakaona ni maji marefu yasiyoogeleka! saa hii inawabembeleza china na urusi waunge mkono kuwatenga korea ya kusini lakini wamewatolea nje! Baada ya kuithibitishia dunia pasipo shaka kuwa korea ya kaskazini ina uwezo wa kutuma kitu kikatua popote pale duniani, wamehaha na wameshaanza kufufua alarm za kushtua watu dhidi ya shambulizi la nyuklia.
Marekani kajaribu mikwala na vitisho vyote vimegonga mwamba. Mara tu baada ya ziara ya Trump huko Asia iliyojaa vitisho na mikwara ya midege lukuki ya kivita ndo jamaa akarusha missile ya masafa marefu ambapo mpaka sasa Trump hajairopokea huko twitter kama alivyokuwa anafanya hapo mwanzo. Ulimi wake umeshafugwa tayari, chezea kuduku wewe!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom