Marekani yasema itaendelea kutoa misaada kwa Tanzania

Kifaurongo

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
4,220
2,358
Akiongea Mbele ya Balozi Mahiga leo, Balozi wa Marekani akiwa ameongozana na maafisa wengine amesema Marekani itaendelea kuisaidia Tanzania katika miradi yake ya maendeleo pamoja na sintofahamu iliyotokea baada ya maamuzi ya MCC.

Amesema Marekeani inaiona Tanzania ni Muhimu sana katika kujenga mahusiano katika eneo hili la ukanda wa Afrika na kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuimarisha mahusiano hayo.
=================

View attachment 337916
Serikali ya Marekani imeihakikishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendeleza uhusiano uliopo baina ya nchi hizo mbili ikiwa ni pamoja na kutoa ufadhili na misaada mbalimbali ya miradi ya maendeleo hasa katika sekta za afya na Elimu.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari muda mfupi mara baada ya kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani hapa nchini aliyeongozana na Ujumbe wa watu 15 wanaoshughulikia miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani hapa nchini, Waziri wa Mambo ya Nje,Afrika Mashariki,Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa Dr Augustine Mahiga alisema kuwa licha ya kutokea kutoelewana kwa Serikali hiyo na Tanzania hivi karibuni lakini nchi hiyo imesema kuwa haitasitisha kuendeleza miradi muhimu kama vile miradi ya Elimu na Afya iliyoanzishwa hapa nchini na Seikali ya Marekani sambasamba na kuendeleza Ushirikiano huo katika nyanja zingine za kimaendeleo.

Aidha Waziri Dr Mahiga aliwatoa hofu watanzania na kusema kuwa miradi yote ambayo ilianzishwa hapa nchini kwa ufadhili wa Serikali ya Marekani itaendelezwa kama ilivyopangwa hapo awali na kuahidi miradi mingine zaidi itakayoleta tija kwa Taifa sambamba na kuleta ajira kwa Watanzania walio wengi.

Kwa Upande wake Balozi wa Tanzania Nchini Mark Childress alisema kuwa upo umuhimu wa kuendeleza mahusiano kati ya Tanzania na Marekani hasa katika utoaji wa misaada mbalimbali ya kimaendeleo hivyo Serikali ya nchi hiyo itaendeleza na kukuza mahusiano hayo licha ya changamoto mbalimbali za kisiasa zilipo nchini.

Nchi hiyo ya Marekani imeahidi kuongeza miradi mingi zaidi nchini itakayolenga kukuza uchumi wa Tanzania na kuitoa nchi hiyo katika hali ya umasikini iliyopo hivi sasa.

Katika mazungumzo hayo, pia walijadili jinsi ya kuimarisha masuala ya kidiplomasia na namna ya kuzidisa usalama wa kikanda kwa manufaa ya wote.
 
Sawa, Nadhani chadema watarudi na hoja yao kujitegemea.. hapa watadai marekani WaPo after uraniaum na gas watasahau ni hivi Pune wametoka kusikitishwa na kusitishwa wa pesa za mcc
 
Walikuwa wanamtingisha Rais Magufuli.

Huyu masikini jeuri hatingishiki wakati huo huo, mabeberu wana vingi vya kupoteza kama wataendelea na msimamo wao kuliko kupata wanachokitafuta.

Niliwahi kusema kwenye hii thread;

Usiwaamini sana hawa mabeberu wa Magharibi kwa sababu hata Muammar Gaddafi alifanya kosa la kukubali kukaa nao meza moja na kuruhusu makampuni yao kuingia Libya kumbe walikuwa majasusi ambao baadaye walifanikisha vikundi vya mapambano dhidi ya utawala wake. The rest is history!
 
Akiongea Mbele ya Balozi Mahiga leo, Balozi wa Marekani akiwa ameongozana na maafisa wengine amesema Marekani itaendelea kuisaidia Tanzania katika miradi yake ya maendeleo pamoja na sintofahamu iliyotokea baada ya maamuzi ya MCC. Amesema Marekeani inaiona Tanzania ni Muhimu sana katika kujenga mahusiano katika eneo hili la ukanda wa Afrika na kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuimarisha mahusiano hayo.

Chanzo: Ch10 Habari
Hii habari chungu kwa Maalimu a. k.a Mzee wa matamko,wajomba zake tena wanasema kinyume cha anavyotaka,na alivyo na husuda huyu mzee eti viongozi wa serikali ya mapinduzi wazuiliwe kwenda nje,kwani nje ndio kwao,wataenda Sheraton kupumzika nje sio lazima.
 
Akiongea Mbele ya Balozi Mahiga leo, Balozi wa Marekani akiwa ameongozana na maafisa wengine amesema Marekani itaendelea kuisaidia Tanzania katika miradi yake ya maendeleo pamoja na sintofahamu iliyotokea baada ya maamuzi ya MCC.

Amesema Marekeani inaiona Tanzania ni Muhimu sana katika kujenga mahusiano katika eneo hili la ukanda wa Afrika na kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuimarisha mahusiano hayo.

Chanzo: Chanel 10 Habari
Tulisema huko nyuma Magufuli is on the right track.
Marekani wameshapima interests zao, mizania imewangukia!
 
Akiongea Mbele ya Balozi Mahiga leo, Balozi wa Marekani akiwa ameongozana na maafisa wengine amesema Marekani itaendelea kuisaidia Tanzania katika miradi yake ya maendeleo pamoja na sintofahamu iliyotokea baada ya maamuzi ya MCC.

Amesema Marekeani inaiona Tanzania ni Muhimu sana katika kujenga mahusiano katika eneo hili la ukanda wa Afrika na kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuimarisha mahusiano hayo.

Chanzo: Chanel 10 Habari
wamejarib kumtiksa magufuli hatiksiki
 
Sawa, Nadhani chadema watarudi na hoja yao kujitegemea.. hapa watadai marekani WaPo after uraniaum na gas watasahau ni hivi Pune wametoka kusikitishwa na kusitishwa wa pesa za mcc
Walisema kwa nguvu kuhusu kujitegemea baada ya saga la MCC ni CDM? Au CCM?
 
Akiongea Mbele ya Balozi Mahiga leo, Balozi wa Marekani akiwa ameongozana na maafisa wengine amesema Marekani itaendelea kuisaidia Tanzania katika miradi yake ya maendeleo pamoja na sintofahamu iliyotokea baada ya maamuzi ya MCC.

Amesema Marekeani inaiona Tanzania ni Muhimu sana katika kujenga mahusiano katika eneo hili la ukanda wa Afrika na kuna umuhimu mkubwa wa kuendelea kuimarisha mahusiano hayo.

Chanzo: Chanel 10 Habari
Hawa walikuwa wanatikisa kibariti itabidi mikataba yao ichunguzwe kwa undani zaidi maana wapo kimasila tu hawa hawana mema sana kwetu.
 
Walikuwa wanamtingisha Rais Magufuli.

Niliwahi kusema kwenye hii thread;

Usiwaamini sana hawa mabeberu wa Magharibi kwa sababu hata Muammar Gaddafi alifanya kosa la kukubali kukaa nao meza moja na kuruhusu makampuni yao kuingia Libya kumbe walikuwa majasusi ambao walifanikisha vikundi vya mapambano. The rest is history!

Mkuu kwa mtizamo wangu kulingana na huo ushabiki wako, naomba niseme hujui kitu kuhusu hii Dunia sasa inaelekea wapi na kwanini inaelekea huko.

Utanisamehe kama nitakukwaza ila kwa hii issue kubali kataaa hujui lolote about this World na proof yake ni hiyo thread uliyoanzisha siku hiyo. Wewe kutoka katika hiyo minyororo hutaweza kamwe mpaka utapokuwa na fikra huru ambazo hazihitaji kuegemea popote.

Viongozi wa Africa wapo katika trap ambayo hawataweza kutoka kamwe kulingana na uroho wao wakujilimbikizia mali na anasa zisizo na msingi. Ila unafiki umewajaa sana. Mfano ni issue ya Gaddafi uliyotaja? Nikufunue zaidi hebu fuatilia kwa kina Blueprints za Hitler hope unamjua vizuri tuu na uweke kando media propaganda.

Nyerere na Sikoine walishindwa policies za WB na IMF itakuwa siye kwa sasa na ambavyo washapandikiza watu wao vya kutosha. Hatuwezi ku extract chochote siye mkuu , We need them.

Najua utakuja na hoja laini that Mchina yupo, sababu hujui ni kwanini China ipo hivyo mpaka sasa. Remember nchi zote za Asia na hizi zingine katika mabara zinazoibuka ni plan B ya hao wakubwa. China unapotegemea hakuna technolojia makini zaidi ya high end za copy and paste.
 
Back
Top Bottom