Marekani yasaini muswada kupinga vikwazo vya China dhidi ya waislamu

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,189
4,103
Bunge la Marekani limepitisha muswada ili kupambana na vile wanavyovisema kuwa ni vikwazo visivyo na mantiki, mateso na unyanyasaji kwa waislamu wa jamii ya Uighur nchini China.

Imelenga vile vikwazo vinavyowalenga wanachama wa serikali ya China na kumtaja kiongozi wa chama cha kikomunisti katika mkoa wa Xinjiang,Chen Quanguo.

Muswada huo bado unahitaji idhini kutoka kwa seneta na Rais Donald Trump.

Kwa upande wa China, Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo ameoneshwa kutofurahishwa na kusema hatua hiyo ni ya ''uovu''.
Muswada wa haki za kibinadamu za Uighur wa mwaka 2019 ulipitishwa bungeni na wabunge 407 kwa 1 usiku wa Jumanne.

Kupitishwa kwake kunakuja mara baada ya Rais Trump kutia saini sheria inayounga mkono maandamano ya demokrasia mjini Hong Kong pia kusababisha ukandamizaji kutoka kwa China.

Thomas Massie kutoka chama cha Republican kutoka Kentucky, amepiga kura kupinga muswada huo wa Uighur, vilevile hakuupigia kura muswada wa Hong Kong.

Mwandishi wa BBC nchini China John Sudworth amesema kama muswada huu utapitishwa basi ''itaashiria jaribio muhimu sana la kimataifa kushinikiza China kuhusu kuwaweka kizuizini waislamu wengi wa Uighur na wale kutoka makundi mengine ya kiislam.''

Marekani yasaini muswada kupinga vikwazo vya china dhidi ya waislamu wa Uighur
 
Ni kwa ajili ya hao waislamu au ni kwa chuki dhidi ya China? Au ni muendelezo wa uhasama kwenye vita vya kibiashara? kwani waislamu wanateseka huko China pekee? Wakati kundi la Ant-balaka linaua waislamu huko Central African Republic alichukua hatua gani? Waislamu wanao uawa huku Palestina na kwingineko amechukua hatua gani?
 
Hizo zinaitwa politics, yaani ni kama babaishabwege, Marekani anafanya kila anachoona kina MASLAHI kwake na sio MASLAHI ya yyte, ata akiwekea vikwazo China dhidi ya hivyo haiondoi ukweli kuwa Us ndio alieuwa Waislam wengi sana duniani na ndie anaechukia Waislam,pia inawezekana anataka kaengeza ushawishi M/East kwa kuonekana eti anatetea Waislam kumbe ni politics ya vita ya kibiashara
Bado kuna waislamu watasema marekani wanawachukia waislamu
 
Ni kwa ajili ya hao waislamu au ni kwa chuki dhidi ya China? Au ni muendelezo wa uhasama kwenye vita vya kibiashara? kwani waislamu wanateseka huko China pekee? Wakati kundi la Ant-balaka linaua waislamu huko Central African Republic alichukua hatua gani? waislamu wanao uawa huku Palestina na kwingineko amechukua hatua gani?
Kwa hiyo Wakristo wa Ant-baraka wanauwa Waislamu ila wao hawauliwi sio?
Siku Hammas ikiweka silaha chini kutakuwa na amani eneo hilo, ila Israel ikiweka silaha chini unajua nini kitatokea?
.
Hii dunia bila America kama super power WW3 ingeshatokea
 
Ndio akili zako zinavyokufundisha, ccm itatawala daima kama kutakua na akili kama hizi
Kwa hiyo Wakristo wa Ant-baraka wanauwa Waislamu ila wao hawauliwi sio?
Siku Hammas ikiweka silaha chini kutakuwa na amani eneo hilo, ila Israel ikiweka silaha chini unajua nini kitatokea?
.
Hii dunia bila America kama super power WW3 ingeshatokea
 
Hizo zinaitwa politics, yaani ni kama babaishabwege, Marekani anafanya kila anachoona kina MASLAHI kwake na sio MASLAHI ya yyte, ata akiwekea vikwazo China dhidi ya hivyo haiondoi ukweli kuwa Us ndio alieuwa Waislam wengi sana duniani na ndie anaechukia Waislam,pia inawezekana anataka kaengeza ushawishi M/East kwa kuonekana eti anatetea Waislam kumbe ni politics ya vita ya kibiashara
China amefanya nini kuikemea marekani isiue waislam?

Mmeshtukizwa!!!
 
Kwa hiyo Wakristo wa Ant-baraka wanauwa Waislamu ila wao hawauliwi sio?
Siku Hammas ikiweka silaha chini kutakuwa na amani eneo hilo, ila Israel ikiweka silaha chini unajua nini kitatokea?
.
Hii dunia bila America kama super power WW3 ingeshatokea
Si kweli nani angeanzisha vita ya tatu ya dunia.
 
Back
Top Bottom