Marekani yamuua Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Iran katika shambulio la roketi la uwanja wa ndege wa Baghdad

chizcom

JF-Expert Member
Jul 31, 2016
7,581
15,720
Qasem Soleimani, Jenerali wa vikosi vya kikurdi vinavyoungwa mkono na Iran, ameuawa na vikosi vya Marekani nchini Iraq. Pentagon imethibitisha kuwa aliuawa kufuatia "amri ya rais".




Hayo yamejiri kufuatia ripoti ya mashambulio katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Baghdad, ambayo ilisema watu kadhaa wameuawa.

Waziri wa mambo ya nje wa Iran, Javad Zarif, ametaja hatua hiyo kuwa "hatari na uchokozi wa kishenzi".

Gen. Soleimani alikuwa mtu mashuhuri kwa utawala wa Iran. Kikosi chake cha Kikurdi kilikuwa kinaripoti moja kwa moja kwa kiongozi mkuu wa kidini wa Iran Ayatollah Ali Khamenei na alisifiwa kama shujaa wa kitaifa.

Rais wa Marekani Donald Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter picha ya bendera ya Marekani baada ya kutangazwa kuuawa kwa jenerali hiyo.
IMG_6034.JPG

Ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinasema kuwa Jenerali Soleimani na maafisa wa waasi wanaoungwa mkono na Iran nwalikuwa wakiondoka katika uwanja wa ndege wa Baghdad kwa kutumia magari mawili wakati waliposhambuliwa na ndege za Marekani zisizokuwa na rubani karibu na eneo kuweka mizigo.

Kamanda huyo aliripotiwa kusafiri kutoka Lebanon au Syria. makombora kadhaa yaliripotiwa kushambulia msafara wao, ambapo karibu watu watano wanaaminiwa kuawa.

Taarifa iliyotolewa na Pentagon ilisema: "Kufuatia agizo la rais, vikosi vya jeshi la Marekani vilichukua hatua ya kuwalinda wafanyikazi wake nje ya nchi kwa kumuua Qasem Soleimani,"

"Hatua hii ililenga kudhibiti mipango ya Iran ya mashabulio ya siku zijazo. Marekani itaendelea kuchukua hatua madhubuti kuwalinda watu wetu na maslahi yetu kote duniani," ripoti hiyo iliendelea kusema.

Shambulio hilo la ndege zisizo na rubani linakuja baada ya siku kadhaa za maandamano ambapo waandamaanaji waliokuwa wakishambulia ubalozi wa Marekani mjini Baghdad kukabiliana na vikosi vya Marekani katika eneo hilo.

Pentagon inasema jenerali Soleimani aliidhinisha mashambulio dhidi ya ubalozi wa Marekani.


Qasem Soleimani ni nani?
  • Tangu mwaka Since 1998, Meja Jenerali Qasem Soleimani ameongoza vikosi vya kikurdi nchini Iran- kengo maalum cha jeshi la Iran (Revolutionary Guards) ambacho huendesha opareshani zake nje ya nchi.
  • Alikuwa kiungo muhimu katika mapambano ya kimkakati mashariki ya kati kupitia vikosi vya Kikurdi, ambavyo vinaendesha oparesheni yake kwa ushirikiano na jeshi la ulinzi la Iran.
  • Meja jenerali Qasem Soleimani, na vikosi vyake vinafanya kazi chini ya kiongozi mkuu wa kidini, Ayatollah Ali Khamanei, badala ya kufuata muundo wa kawaida wa kijeshi wa Iran.
  • Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alitaja jeshi la ulinzi la Iran Revolutionary Guards na washirika wake vikosi vua Kikurdi kama shirika la kigeni la ugaidi mwezi April mwaka jana.
 
Duuh, kwahiyo ili shambulizi nijipya?
Aisee inabidi dunia ifanye maombi kwaajili ya middle East.

Mambo ni magumusana huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu alikuwa ndio mchora ramani wa Iran kwa shughuli zao zote nje ya Iran, kuanzia kushambuliwa kwa Visima vya Mafuta vya Saudi Arabia mpaka kuteka meli na bila kusahau kashikashi la Ubalozi wa Marekani. Tungoje tuone Iran atafanya nini,sasa hivi kichapo kwake kipo wazi wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BREAKING: #Iran vows retaliation following death of IRGC commander #Soleimani - senior military officer Iran Vows Retaliation Following Death of IRGC Commander Soleimani - Senior Military Officer Sputnik on Twitter
Huyu alikuwa ndio mchora ramani wa Iran kwa shughuli zao zote nje ya Iran, kuanzia kushambuliwa kwa Visima vya Mafuta vya Saudi Arabia mpaka kuteka meli na bila kusahau kashikashi la Ubalozi wa Marekani. Tungoje tuone Iran atafanya nini,sasa hivi kichapo kwake kipo wazi wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
JITAARISHENI KIPIGO CHAJA

IMG_20200103_024536.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
BREAKING: #Iran vows retaliation following death of IRGC commander #Soleimani - senior military officer Iran Vows Retaliation Following Death of IRGC Commander Soleimani - Senior Military Officer Sputnik on TwitterJITAARISHENI KIPIGO CHAJA View attachment 1310666

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahaha hawatathubutu,njoo tubeti kama Iran atafanya kitu. Kipindi ndio atajua Marekani ni nani,maana walikuwa wanamchekea mpaka ikafikia hatua ya kumshika Simba sharubu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
#Breaking #Iran military forces command: “we will be delivering a seismic response to the #US assassination of General #Soleimani in #Iraq, and the crossing of all the red-lines.”
Nakwambia hivi,kama Iran anajipenda hataweza kujaribu huo ujinga sababu anajua Safari hii US hatamuacha salama

Sent using Jamii Forums mobile app
Mm sie niliesema, Wairan wakisema wanafanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
#Breaking #Iran military forces command: “we will be delivering a seismic response to the #US assassination of General #Soleimani in #Iraq, and the crossing of all the red-lines.”Mm sie niliesema, Wairan wakisema wanafanya

Sent using Jamii Forums mobile app
Hayo ni maneno ya kujifariji na kuwapa matumaini nyie wafuasi wake. Mpaka sasa US 3 na Iran 0

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu alikuwa ndio mchora ramani wa Iran kwa shughuli zao zote nje ya Iran, kuanzia kushambuliwa kwa Visima vya Mafuta vya Saudi Arabia mpaka kuteka meli na bila kusahau kashikashi la Ubalozi wa Marekani. Tungoje tuone Iran atafanya nini,sasa hivi kichapo kwake kipo wazi wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi US waliwapa taarifa Iraq kwenye hilo shambulizi?.

Maana Iraq juzi walisema US wana kosa adabu kwa kufanya mashambulizi kwenye ardhi ya nchi yao bila ya wao kupewa taarifa.
Sasa kama hawakuwataarifu Iraq tena kwenye hilo shambulizi, Iraq wanaweza kuwaruhusu raiya kuingia tena kwenye ubalozi na kufanya uharibifu zaidi.

I just guess.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
2 Jan 2020

BAGHDAD (AP) — An airstrike killed Gen. Qassem Soleimani, head of Iran’s elite Quds Force and architect of its regional security apparatus, at Baghdad’s international airport Friday, Iranian state television and three Iraqi officials said, an attack that's expected to draw severe Iranian retaliation against Israel and American interests.

The strike also killed Abu Mahdi al-Muhandis, deputy commander of Iran-backed militias in Iraq known as the Popular Mobilization Forces, or PMF, the officials said. The PMF media arm said the two were killed in an American airstrike that targeted their vehicle on the way to airport

8844434e-ad43-4b4d-b646-b7a9c25db3c2.jpg



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom