BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,086
Labda sasa usanii wa JK kuhusu mafisadi umefikia kikomo. Jamaa wakikaza uzi na nchi nyingine za magharibi basi labda yale tuliyokuwa tukiyapigia kelele kuhusu mafisadi yatatimia
Marekani yambana JK
na Kulwa Karedia
Tanzania Daima~Sauti ya Watu
SERIKALI ya Marekani, imemtaka Rais Jakaya Kikwete, kuwakamata na kuwafikisha mahakamani vigogo pamoja na watu wote wanaohusishwa na kashfa za ufisadi, bila kujali nyadhifa kubwa wanazoshika serikalini.
Imesema katika kupambana na mafisadi, Rais Kikwete hapaswi kuangalia wadhifa wa mtu, awachukulie hatua wote wanaotuhumiwa bila kujali kama ni mawaziri au watu wenye nyadhifa kubwa serikalini.
Msimamo huo wa Marekani kuhusu vita dhidi ya mafisadi,ulitolewa juzi jijini Dar es Salaam na Balozi wa Marekani hapa nchini, Mark Green alipokuwa akizungumza katika sherehe za maadhimisho ya miaka 232 ya uhuru wa taifa hilo.
Rais Kikwete anatakiwa kuchukua hatua za kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale wote watakaobainika kuhusika na wizi wa mamilioni ya fedha za wananchi tunataka kuona hilo linatakelezwa bila kujali ni nani na ana wadhifa gani, alisema Balozi Green.
Balozi huyo alisema iwapo Rais Kikwete atafanya kazi ya kuwafikisha mahakamani viongozi wanaotuhumiwa kwa ufisadi na tuhuma nyingine dhidi ya mali ya umma, atafanikiwa kurejesha imani kwa wananchi na mataifa ya nje yanayotoa misaada kwa Tanzania, ikiwemo Marekani yenyewe.
Rais aliagiza kufanyika uchunguzi kupitia tume yake aliyounda kwa kipindi cha miezi sita na majibu yako karibu kutoka tunategemea kupata majibu ya msingi na kuona nini kitafanyika kwa wale wote waliohusika, alisema Balozi Green.
Balozi Green hakusita kuonyesha hisia zake kwa vyombo vya habari vya hapa nchini, alipovimwagia sifa kwa kuongoza mapambano dhidi ya ufisadi.
Alisema vyombo vya habari vya Tanzania vinastahili sifa kutokana na kufichua vitendo vya ufisadi vinavyofanywa na baadhi ya viongozi waliopewa dhamana ya kuongoza taifa.
Tanzania ina vyombo vya habari imara, ambavyo vimekuwa vikiripoti habari muhimu na kutoa changamoto dhidi ya viongozi walioko madarakani, na matokeo yake sasa yanaonekana, alisema.
Akizungumzia tatizo la mpasuko wa kisiasa Zanzibar, alisema wakati Rais Kikwete anaingia madarakani mwaka 2005, aliahidi katika hotuba yake kumaliza tatizo hilo kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) jambo ambalo lilitia matumaini makubwa katika jumuia ya kimataifa.
Tulivutiwa na kauli yake pale aliposema suala hili atalipatia ufumbuzi haraka na analipa kipaumbele zaidi, nadhani sote tunapaswa kumsaidia katika hili ili kupata mafanikio, alisisitiza.
Alisema Marekani kama rafiki wa Tanzania na Zanzibar kwa miaka mingi, haioni sababu ya pande hizo mbili kuogopa kuzungumzia matatizo yanayozikabili.
Katika kufanya mazungumzo kila upande unatoa dukuduku lake, na wakati huo kila upande unapata kile ambacho ulikuwa unategemea na hatimaye kufikia makubaliano, alisema Balozi Green.
Akizungumzia uhuru wa taifa hilo, alisema mwasisi wake, Jenerali George Washington alifanya kazi kubwa ya kuikomboa Marekani kutoka kwenye makucha ya wakoloni na hatimaye kuwa taifa huru ambalo limekuwa mhimili wa demokrasia na maendeleo duniani.
Tamko hilo la Marekani liliifanya serikali kusisitiza kauli yake ambayo imekuwa ikiitoa kila mara kuwa, wale waliohusika na wizi wa fedha za umma watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Mwakilishi wa serikali katika sherehe hizo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, aliwaambia waandishi wa habari kuwa kinachotakiwa ni Watanzania kuwa na subira kwa vile baada ya ripoti ya timu ya rais ya kuchunguza wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), watakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Kweli Balozi Green kazungumzia suala hili, mimi napenda kuwaambia Watanzania kuwa wawe na subira, kwa hili tunaamini wale wote watakaobainika kuhusika, sheria itafuata mkondo wake tu, alisisitiza Waziri Masha.
Alisema serikali haiungi mkono vitendo vya ufisadi vinavyoendelea kutokea, na kwamba vyombo vya dola vinalishughulikia kwa nguvu zote tatizo hilo.
Kuhusu ushirikiano na Marekani, Waziri Masha alisema, Tanzania itaendelea kushirikiana na taifa hilo katika nyanja mbalimbali, na kuwataka Watanzania kujitolea kulitumikia taifa lao kama ilivyo kwa Wamarekani bila kujali itikadi za kisiasa.
Msimamo huu wa Marekani unaweza kumuweka Rais Kikwete katika wakati mgumu iwapo ripoti ya timu yake itawataja baadhi ya viongozi wa serikali na wafanyabiashara wakubwa wanaodaiwa kuchangia kampeni za CCM katika uchaguzi mkuu wa 2005, kuwa wahusika katika wizi wa fedha za EPA.
Sherehe hizo pia zilihudhuriwa na Mzee Rashid Kawawa, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, wasomi na mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.