Marekani yalalamika baada ya Uganda kuwanyima idhini wakaguzi wake wa uchaguzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,426
2,000
Balozi wa Marekani nchini Uganda ameeleza kukatishwa tamaa na hatua ya serikali ya kukataa kuwapatia wasimamizi wao idhini ya kusimamia uchaguzi.

Balozi Natalie Brown amesema kuwa zaidi ya asilimia 75 ya maombi ya idhini za ujumbe wa wakaguzi wa Marekani yalikataliwa.

Ni watu 15 pekee ndio waliopewa idhini hiyo, lakini ubalozi huo unasema idadi hii haitoshi kufuatilia uchaguzi.

Bi Brown ameongeza kuwa Tume ya uchaguzi haikutoa maelezo yoyote juu ya ni kwanini maombi yao yalikataliwa, ingawa ubalozi huo uliwasilisha nyaraka zote zinazohitajika.

Kupitia ujumbe wa Twitter Balozi Natalie E. Brown alisema kuwa anasikitika kutangaza uamuzi wa Marekani wa kutosimamia uchaguzi wa Uganda baada ya asilimia 75 ya maombi ya idhini ya kusimamia uchaguzi kukataliwa:

Social embed from twitter​

RipotiReport this social embed, make a complaint

Mwaka 2016, Marekani ilikuwa na wakaguzi wa uchaguzi zaidi ya 80 kote nchini Uganda.

Jumuia ya Afrika Mashariki na Muungano wa (IGAD), ndio waliothibitisha kupata idhini ya kufuatilia uchaguzi mkuu wa Uganda unaotarajiwa kufanyika Alhamisi wiki hii.
 

May Day

JF-Expert Member
May 18, 2018
4,253
2,000
Hivi mara zote wanaposimamia na kutoa ripoti kuna maboresho yoyote hufanyika au ni format tu?....nadhani hata Babu kaona wataenda kupoteza muda tu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom