Marekani yalaani Mauwaji ya Arusha

mchonga

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,233
247
U.S condemns Arusha bombing.

Last edited by a moderator:
Aache kuja rais wao maana hakuna usalama. Tukio linatokea na polis wapo palepale halaf mharifu anasepa bila polisi kumkamata! Kunasiku jk atapigwa grunade na aliyempiga hataonekana maana hatuna polisi bali vikaragosi 2
 
Inakuwaje kama hao polisi ndo wametumwa na na huyo unaedhani atapigwa grenade?
Mhalifu wala hajakimbia
alikuwepo all the time akiwitness kazi ya mikono yake akiwa ndani ya gwanda.
Video clip ipo! You'll be suprised.
Time...
 
JUMANNE, JUNI 18, 2013 01:20 NA BAKARI KIMWANGA

*Yataka waliohusika wasakwe kwa nguvu zote
*Yawataka Watanzania kufuata misingi ya Nyerere

SERIKALI ya Marekani, imesema watu wote waliohusika na mlipuko wa bomu mjini Arusha, wapaswa kukasakwa kwa udi na uvumba ili wafikishwe mbele ya vyombo vya dola.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam na kusaini na Balozi wa Marekani hapa nchini,Alfonso Lenhardt ilisema Serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua kali dhidi ya wahusika.

Taarifa hiyo, imekuja siku chache kabla ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama ambaye anatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao.

“Tunataka kuona watu wote, waliohusika na tukio hili wanasakwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya dola,

“Marekani inatoa wito wa kukamatwa, kushitakiwa na kutiwa hatiani kwa waliohusika,”ilisema taarifa ya Balozi Lenhardt.

Taarifa hiyo,ilisema kitendo hicho ni cha woga mno kwani kinafanana na ulipuaji wa bomu ulitokea Mei5, mwaka huu katika Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph mjini humo.

“Marekani inalaani vikali mlipuko wa bomu uliotokea Juni 15, mwaka huu katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),tunasikitika kuona watu watatu wamepoteza maisha na kujeruhi wengine zaidi ya 40.

“Tunatoa salamu zetu za rambirambi kwa familia ambazo zilipoteza wapendwa wao na waliojeruhiwa katika uhalifu huu wa kutisha.

“Tunatoa wito wa kukamatwa, kushitakiwa na kutiwa hatiani kwa waliohusika na vitendo hivyo. Tanzania ni nchi inayojulikana kwa utajiri wake wa kiutamaduni, uvumilivu na mchanganyiko wa watu.

“Vitendo vya vurugu za namna hii,aina yoyote, vinatishia kuipaka matope na kudhoofisha amani na usalama wa nchi hii ya aina yake.

“Marekani itaendelea kujenga ushirika na Watanzania wote na tunawataka waendelee kulaani machafuko yanayofanywa na wale wanaotishia usalama wa raia wenzao,” alisema Lenhardt

Taarifa hiyo, ilisema Marekani inatoa wito kwa raia wote kujikita juu ya maadili na misingi ya hekima, umoja na amani ambayo yaliwekwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Misingi hiyo imeelezwa katika wimbo wa taifa wa Tanzania ambayo yameenziwa na kuheshimiwa na Watanzania wote na wapenda amani duniani kote.

Aaaah... Amani ililetwa na Mababu ZETU!!!!

Oh... Rais wa kwanza alitunyima ELIMU... tulibaguliwa (kivipi) Wengine pia tulibaguliwa - Mnataka kusikia Malalamiko ya kila MTU??? then kutakuwa hakuna Tanganyika...
 
wamarekani waache unafiki,vujo kwao ndiyo neema,silaha zote zina anza kutengenezwa kwao!wengine kama wachina wanaiga tuu!Hizo innovation wanazofanya kila siku za silaha kwa manufaa ya nani kama siyo kuua?
 
Wasiishie kulaani tu, wao si ndio polisi wa dunia bana, walete makachero wao (FBI et al) wafanye kazi independently maana kina kagonja hawaaminiki wale
 
Kumbe nao wanajua kuwa kuna watu wanatishia usalama wa taifa???? Poleni CHADEMA kumbe hata dunia inawatambua kwa makeke ujinga wenu!!!
 
Nyerere Alikuwa na misingi ya kikomunist hao wamarekani wanaropoka tu.. hawajui nyerere vizuri
 
Kumbe nao wanajua kuwa kuna watu wanatishia usalama wa taifa???? Poleni CHADEMA kumbe hata dunia inawatambua kwa makeke ujinga wenu!!!

Samahani,cdm wanatishia usalama wa taifa au wanawatisha ccm inayounda serikali iliyomadarakani? yani unaamini washington ndo habari za kijasusi walizonazo! na wewe unafarijika unapost jf atleast lumumba waone umepost kitu! poor minded person,coward n traitor,this is our country!
 
JUMANNE, JUNI 18, 2013 01:20 NA BAKARI KIMWANGA

*Yataka waliohusika wasakwe kwa nguvu zote
*Yawataka Watanzania kufuata misingi ya Nyerere

SERIKALI ya Marekani, imesema watu wote waliohusika na mlipuko wa bomu mjini Arusha, wapaswa kukasakwa kwa udi na uvumba ili wafikishwe mbele ya vyombo vya dola.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mjini Dar es Salaam na kusaini na Balozi wa Marekani hapa nchini,Alfonso Lenhardt ilisema Serikali ya Tanzania inapaswa kuchukua kali dhidi ya wahusika.

Taarifa hiyo, imekuja siku chache kabla ya ujio wa Rais wa Marekani, Barack Obama ambaye anatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao.

"Tunataka kuona watu wote, waliohusika na tukio hili wanasakwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya dola,

"Marekani inatoa wito wa kukamatwa, kushitakiwa na kutiwa hatiani kwa waliohusika,"ilisema taarifa ya Balozi Lenhardt.

Taarifa hiyo,ilisema kitendo hicho ni cha woga mno kwani kinafanana na ulipuaji wa bomu ulitokea Mei5, mwaka huu katika Kanisa la Katoliki la Mtakatifu Joseph mjini humo.

"Marekani inalaani vikali mlipuko wa bomu uliotokea Juni 15, mwaka huu katika mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),tunasikitika kuona watu watatu wamepoteza maisha na kujeruhi wengine zaidi ya 40.

"Tunatoa salamu zetu za rambirambi kwa familia ambazo zilipoteza wapendwa wao na waliojeruhiwa katika uhalifu huu wa kutisha.

"Tunatoa wito wa kukamatwa, kushitakiwa na kutiwa hatiani kwa waliohusika na vitendo hivyo. Tanzania ni nchi inayojulikana kwa utajiri wake wa kiutamaduni, uvumilivu na mchanganyiko wa watu.

"Vitendo vya vurugu za namna hii,aina yoyote, vinatishia kuipaka matope na kudhoofisha amani na usalama wa nchi hii ya aina yake.

"Marekani itaendelea kujenga ushirika na Watanzania wote na tunawataka waendelee kulaani machafuko yanayofanywa na wale wanaotishia usalama wa raia wenzao," alisema Lenhardt

Taarifa hiyo, ilisema Marekani inatoa wito kwa raia wote kujikita juu ya maadili na misingi ya hekima, umoja na amani ambayo yaliwekwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Misingi hiyo imeelezwa katika wimbo wa taifa wa Tanzania ambayo yameenziwa na kuheshimiwa na Watanzania wote na wapenda amani duniani kote.

Laana imeanziwa kwa Rais aka Fast jet Marekani mnayemthamini! Hamtambui Nyerere wala mazuri ya Nyerere amekuja kutengeneza TZ yake ya UFITINI wa KIDINI na KISIASA!!
 
Sema tuu tamko zito lna kilo ngapi?
Au kwa sababu limetoka kwa WAUS?
 
Aache kuja rais wao maana hakuna usalama. Tukio linatokea na polis wapo palepale halaf mharifu anasepa bila polisi kumkamata! Kunasiku jk atapigwa grunade na aliyempiga hataonekana maana hatuna polisi bali vikaragosi 2

Hapa ni kweli mkuu,ipo siku rais atabtuliwa na ----- atakayembutua atasepa bila kukamatwa kama askari wenyewe ndio askari shati,wanajua kujilinda wenyewe tu.
Ila kwa hili la arusha wanaonekana kupanga kabisa
 
Inakuwaje kama hao polisi ndo wametumwa na na huyo unaedhani atapigwa grenade?
Mhalifu wala hajakimbia
alikuwepo all the time akiwitness kazi ya mikono yake akiwa ndani ya gwanda.
Video clip ipo! You'll be suprised.
Time...

Wakuu hebu tupieni hiyo clip mapema, wasije kusema imetengenezwa, tupia clip mbaya ajulikane mapema, SUPU YA MBWA HULIWA INGALI MOTO!
 
2livyo wepec kupepetwa km mahindi tena kwenye cnia, bac overseas wanapata raha kwel, hahahahahaha
 
Kumbe nao wanajua kuwa kuna watu wanatishia usalama wa taifa???? Poleni CHADEMA kumbe hata dunia inawatambua kwa makeke ujinga wenu!!!
Jasho inawatoka hadi mmepoteza akili. Sasa si muwakamate kama wamevunja sheria badala ya dola kufanya ugaidi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom