Marekani yakumbuka watu laki tano waliokufa kwa COVID-19. Tanzania tuna bahati sana, tumshukuru Mungu

Data zikitolewa mnapinga na kudai zimepikwa,hamjulikani kipi mnapenda ,jua au mnvua
Issue sio kupenda au kutopenda issue ni kujisifia kwamba Corona imeua sana kule kuliko huku.., (Hence Mungu anatupenda) Tunasahau kwamba Malaria Ukimwi, Vifo vya watoto wachanga ni vingi huku kuliko kule...

Na tunajua kabisa vulnerable people kule ni wengi kuliko huku (wa huku wengi walishakufa)..., Kwahio tujiandae likija gonjwa lenye mortality rate kubwa na llinaloambukiza sana... Sitaki kufikiri what will happen
 
Tukubaliiane madhara ya Corona kwa nchi yetu si makubwa ,tumeushinda ugonjwa huu,japo umechukua maisha ya baadhi ya ndugu zetu.
Ukiangalia hali ya huduma za kiafya za nchi kama Amerika (bora zaidi) kulinganisha na huduma za kiafya za nchi kama yetu (duni), mungu katufanyia huruma ya hali ya juu sana.tumsifu sana Mungu wetu,ugonjwa huu hauna mjinga wala mwerevu
Wao wanajua ni laki tano, sisi tunajua tumepoteza wangapi kwa ugonjwa huu?

Baada ya kujua tumepoteza ndugu zetu wangapi, hapo ndipo tunaweza kuangalia uwiano uliopo kati ya wao na sisi.

Sasa haya mambo ya kusema tu tuna mungu wetu anayetupenda kuliko wengine hasa yanatoka wapi kama sio propaganda tupu za kupotosha wasiojua mambo haya.

Lakini kwa nini ujilinganishe na wao huko mbali, kwa nini usiulize tu hapo Rwanda kama na wao Mungu, sijui kama wanaye (mungu) wa kwao pia, kawatelekeza, au na wao kawalinda kama huyu wa kwetu alivyotupendelea?
 
Kwahio tujiandae likija gonjwa lenye mortality rate kubwa na llinaloambukiza sana... Sitaki kufikiri what will happen
Likija gonjwa la namna hiyo, na kiongozi awe bado ni huyu huyu na hakubadilika kwa kuogopa aibu...

Lakini tunaweza pia kulinganisha na aina ya gonjwa la aina hiyo lililowahi kutokea miaka ya nyuma kidogo na bado lipo lakini limedhibitiwa kwa vile tulikuwa na viongozi wasiokuwa na kiburi kama huyu.

Hebu fikiria HIV/AIDS ndio ingeingia wakati huu imkute kiongozi huyu.

Akatae kutumia njia zote za kujikinga, kama mipira ambayo angesema imewekewa sumu kutuua waafrika.

Yeye angehimiza maombi kwa 'mungu' wake, na dawa za kienyeji, basi..., sijui wakati huu taifa letu lingekuwa na hali gani?

Maana watu wasingeacha kujamiiana, na jinsi ugonjwa huo unavyosambazwa kimyakimya; maabikizi yake hayaonekani kwa muda mfupi kabla haujajitokeza bayana, si watu wangepukutika kama nzige waliopuliziwa dawa?
 
Sasa data ama statistics mmeficha tutajuaje kuwa tulipukutika au maombi yenu yaliwasaidia.
KUNA MZUNGU ALINIAMBIA KUWA AFRIKA HAMUENDELEI KAMA SISI KWA SABABU MAMBO MENGI MMEMUCHIA MUNGU.
Ata kama data zimefichwa na haijalisha USA ina raia wangapi na pia ujue walichukua tahafhari zote za WHO pamoja na kujiweka Lockdown, barakoa mbilimbili, sanitizer, farmigation etc lakini watu laki 5 wameenda ila Tanzania hivyo vyote hatujafanya nilitegemea basi watu wasipungua milion 2 mpaka 5 wangeondoka maana hakuna lockdown, hakuna barakoa sie mwendo wa tangawizi na kujifukiza pamoja na macovido ambayo mnaona si ya maana ata robo ya hivyo vifo hatujafikia.
 
Sasa data ama statistics mmeficha tutajuaje kuwa tulipukutika au maombi yenu yaliwasaidia.
KUNA MZUNGU ALINIAMBIA KUWA AFRIKA HAMUENDELEI KAMA SISI KWA SABABU MAMBO MENGI MMEMUCHIA MUNGU.
Umeambiwa mficha maradhi kifo umuumbua, So hizo data ni USELESS. Inatakiwa useme ukoo wetu karibia wote wamekufa, majirani zangu wamebaki watatu.So hili linatakiwa lianze na wewe na sio story za kusikia
 
Pamoja na mibarakoa yote ile watu laki 5 wamekufa?

Wanasema hao laki 5 ni wengi kuliko wale waliokufa kwenye vita ya kwanza na ya pili ya dunia ukiunganisha kwa pamoja.
 
Wao wanajua ni laki tano, sisi tunajua tumepoteza wangapi kwa ugonjwa huu?....
Rwanda wamekufa wangapi?

Kiufupi Afrika nzima Mungu katupendelea,

Lakini kwa ishu ya tz ukuu wa Mungu unaonekana zaidi maana sisi hatujawahi kuchukua tahadhali zozote kwa hiyo tulitegemea kama kule wanakochukua tahadhali wanakufa laki 5, sisi tungekufa mara 10 yake au zaidi
 
Tukubaliiane madhara ya Corona kwa nchi yetu si makubwa ,tumeushinda ugonjwa huu,japo umechukua maisha ya baadhi ya ndugu zetu.
Ukiangalia hali ya huduma za kiafya za nchi kama Amerika (bora zaidi) kulinganisha na huduma za kiafya za nchi kama yetu (duni), mungu katufanyia huruma ya hali ya juu sana.tumsifu sana Mungu wetu,ugonjwa huu hauna mjinga wala mwerevu

si makubwa kwa sasa ni lazima ujue corona inabadilika na wimbi hili la pili limeua sana na tusikofanya chanjo litakuja la tatu. Tuliweza kukabili wimbi la kwanza mwaka jana sasa hivi watu wengi sana wamepata corona mimi nyumbani kwetu zaidi ya watu 10 wapata corona lakini wote wamepona. Hii iliyokuja mwezi wa kumi na mbili kutoka south ni kali sana.

Wengi hawafi kwasababu ya umri Tanzania kuna watu milioni 13 tu wenye umri zaidi ya miaka 35 ! Wenzetu wana watu milioni 350 na umri wa kati 39-40 wakati sisi 17-18 zaidi ya mara mbili!
 
Pia huyo MZUNGU aliongezea kusema sisi WAAFRIKA tumeletewa dini vitisho kuwa MUNGU hadiskasiwi kwa sababu tutapata zambi
Hapo kwa Mungu jombaa paache tu... We baki na mzungu wako ila ukianza kumuingiza Mungu kwa approach unayoifanya unakosea jombaa.
 
Tukubaliiane madhara ya Corona kwa nchi yetu si makubwa ,tumeushinda ugonjwa huu,japo umechukua maisha ya baadhi ya ndugu zetu.
Ukiangalia hali ya huduma za kiafya za nchi kama Amerika (bora zaidi) kulinganisha na huduma za kiafya za nchi kama yetu (duni), mungu katufanyia huruma ya hali ya juu sana.tumsifu sana Mungu wetu,ugonjwa huu hauna mjinga wala mwerevu
Msemo

Wajinga ndiwo waliwao.
Mimi narekebisha, wapumbavu ndiwo waliwao.

Chukua idadi ya marekani waliokufa kwa covid ni asilimia ngapi ya wamarekani wote

Alafu chukua idadi ya waliokufa kwa covid Tanzania ni asilimia ngapi ya watanzania wote

Utaona nchi gani wamekufa wengi
Msiropoke tu

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna cha kushukuru Mungu, uenda tukawazidi, na uwezi ficha takwimu halafu useme sisi tuna afadhali! Toa takwimu unaogopa nini?
 
Tukubaliiane madhara ya Corona kwa nchi yetu si makubwa ,tumeushinda ugonjwa huu,japo umechukua maisha ya baadhi ya ndugu zetu.
Ukiangalia hali ya huduma za kiafya za nchi kama Amerika (bora zaidi) kulinganisha na huduma za kiafya za nchi kama yetu (duni), mungu katufanyia huruma ya hali ya juu sana.tumsifu sana Mungu wetu,ugonjwa huu hauna mjinga wala mwerevu
Hamna hata takwimu, hamfanyi testing mnajuwaje kama hamkuwazidi hata hao laki tano? mbona mnapenda kudharau akili za wenzenu kiasi hiki?
 
Back
Top Bottom