Marekani yakumbuka watu laki tano waliokufa kwa COVID-19. Tanzania tuna bahati sana, tumshukuru Mungu

wakatanta

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
2,593
3,148
Tukubaliiane madhara ya Corona kwa nchi yetu si makubwa, tumeushinda ugonjwa huu, japo umechukua maisha ya baadhi ya ndugu zetu.

Ukiangalia hali ya huduma za kiafya za nchi kama Amerika (bora zaidi) kulinganisha na huduma za kiafya za nchi kama yetu (duni), mungu katufanyia huruma ya hali ya juu sana.

Tumsifu sana Mungu wetu,ugonjwa huu hauna mjinga wala mwerevu.
 
Unataka kusema ni zaidi ya Amerika?
Acheni ujinga nyie. Mnang'ang'ania namba tu kwa vile mnajua watanzania wengi hawataki kutafakari beyond namba. Umejiuliza Marekani ina watu wangapi?

Tanzaniua nayo ina watu wangapi? Umejiuliza Marekani ina watu wangapi ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60? Umejiuliza Tanzania ina watu wangapi ambao umri wao ni zaidi ya miaka 60? Umejiuliza Tanzania mapaka sasa wameshafariki watu wangapi kuanzia wale waliokuwa wanazikwa usiku kwa mafungu mwaka jana?

Umejiuliza Marekani ina watu wangapi walio kwenye risk group wakipata corona? Unajua Marekani kuna wagonjwa wengi wa magonjwa kama moyo, kansa, kisukari n.k. ambao bado wanaishi kwa sababu utaalam wa mbambo ya tiba yako juu na kama wangekuwa Tanzania wangeshafariki zamani sana?
 
Unaijua idadi ya waliokufa kwa Corona Tanzania ?
Bila hata ya kujua idadi ya vifo vya Tanzania. Ajiulize Marekani ina raia wangapi ambao umri wao ni zaidi ya miaka 65? Na Tanzania ina raia wangapi ambao umri wao ni zaidi ya mika 65?

Kwa kifupi idadi ya raia wa Marekani wenye miaka 65 na zaidi (ambao ni rahisi kufa kwa corona kulingana na utafiti) inazidi idadi ya raia wote wa Tanzania! Kwa kifupi ni kuwa Marekani wenye umri wa miaka 65 na zaidi ni around milioni 70 wakati Tanzania raia wenye miaka 65 na zaidi hawafiki milioni mbili!

Kwa hiyo tukichukuwa factor ya umri tu kama kigezo cha ''hatari ya kufa kwa covid'' utaona tunafananisha watu milioni 70 vs watu milioni 1.8! Hapo bado hujaweka kigezo kingine cha watu wenye magonjwa hatarishi kama moyo, kansa, kisukari n.k. ambao kule Marekani wako wengi sana kwa sababu wanaishi maisha marefu kutokana na huduma nzuri.

Hawa wajinga wanajua watanzania wengi hawawezi kutafakari vitu kama hivi, hivyo hukimbilia kutaja tu namba na kusema anagalieni wenzetu wanavyokufa.
 
Dah Mama Tanzania.

Hivi hizi maabara za mtaani zina vipimo vya covid 19 kweli,sample mpaka itoke kwa mkemia mkuu tayati ushachomoka.
 
H
Tukubaliiane madhara ya Corona kwa nchi yetu si makubwa ,tumeushinda ugonjwa huu,japo umechukua maisha ya baadhi ya ndugu zetu.
Ukiangalia hali ya huduma za kiafya za nchi kama Amerika (bora zaidi) kulinganisha na huduma za kiafya za nchi kama yetu (duni), mungu katufanyia huruma ya hali ya juu sana.tumsifu sana Mungu wetu,ugonjwa huu hauna mjinga wala mwerevu
Hivi ukikaa kimya hautatambulika mpaka na wewe uandike. Tuwe na busara tuikimbie aibu.
 
Bila hata ya kujua idadi ya vifo vya Tanzania. Ajiulize Marekani ina raia wangapi ambao umri wao ni zaidi ya miaka 65? Na Tanzania ina raia wangapi ambao umri wao ni zaidi ya mika 65?...
Utetezi mfu,lengo ni ku -under-rate utawala uliopo madarakani tu.
 
Kwa hesabu zangu waliokufa kwa Korona nao wajua ni 57 mpaka jana, ninao wajua kabisa,
Ugua pole Mpango
 
Hauna Data ni vigumu kuongea..., Tuongelee data ambazo tunazo.

Mortarity rate ya Malaria ni kubwa kuliko Corona (ni wangapi Tanzania wamekufa kwa Malaria) ofcource ni more than America (vipi hapo Mungu hakutuonea huruma)?

Malaria inaua kwetu kuliko hata Ukimwi na Ukimwi ulipiga zaidi Huku kuliko kule (tulimkosea nini Mungu)?

Corona inaua 5% na wengi wao umri umekwenda juu na wanamatatizo mengine, Bongo ungekuwa una matatizo mengi ungeshakufa hata kabla haujafikisha miaka mitano, na life expectancy ni 65 years. Je, wenzetu yao ni ngapi?

Pia huyu Mungu anayeua wengine na kusamehe wengine kutowaua (ingawa kifo ingekuwa ni adhabu wazuri wasingekufa)..., Kweli ndio tunaomba mwisho twende tukae nae milele na milele?
 
Sasa data ama statistics mmeficha tutajuaje kuwa tulipukutika au maombi yenu yaliwasaidia.
KUNA MZUNGU ALINIAMBIA KUWA AFRIKA HAMUENDELEI KAMA SISI KWA SABABU MAMBO MENGI MMEMUCHIA MUNGU.
Hapo kwa Mungu sasa unakosea jombaa
 
Acheni ujinga nyie. Mnang'ang'ania namba tu kwa vile mnajua watanzania wengi hawataki kutafakari beyond namba. Umejiuliza Marekani ina watu wangapi? Tanzaniua nayo ina watu wangapi...
Kwahiyo unachosema mkuu ni kwamba Tanzania watu wenye miaka kuanzia 65 ni wachache ukilinganisha na Marekani ambako wako na ndio wanaokufa sana na kwamba Tanzania watu wenye magonjwa kama ya kansa, moyo, kisukari n.k ni wachache kuliko Marekani hivyo ndio maana hatuoni wingi wa vifo kama Marekani?
 
Back
Top Bottom