Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 414
Raia wa Marekani anayeshikiliwa nchini Venezuela kwa madai ya kufanya ujasusi nchini humo hakutumwa na serikali ya Marekani, taarifa ya kiongozi wa ngazi ya juu katika serikali ya Marekani imebainisha.
Mwendesha Mashtaka mkuu wa Venezuela, Tarek Wiliam Saab alitangaza siku ya Jumatatu kuwa jasusi huyo aliyekamatwa wiki iliyopita, Matthew John Heath, atafunguliwa mashtaka ya ugaidi pamoja na usafirishaji haramu wa silaha.
Uhusiano wa kidiplomasia kati ya Venezuela na Marekani unatajwa kuwa katika hali mbaya, huku Saab akieleza kuwa jasusi huyo wa Kimarekani akipanga kulipua viwanda vya OPEC na mifumo ya umeme ya nchi hiyo.
Lakini Mjumbe Maalum wa Marekani kwa Venezuela na Iran, Elliot Abrahams anaamini kuwa Heath hakutumwa na serikali ya Marekani, ingawa amesema kuwa hawezi kusema zaidi kwa sababu za kiusalama, na kwa kuwa Venezuela haina ubalozi wake mjini Caracas.
Awali Maduro alitangaza kukamatwa kwa jasusi huyo akiwa katika harakati za upelelezi wa kiwanda cha kusafisha mafuta katika eneo la Falcon Magharibi, akiwa na silaha maalum za upelelezi.
Afisa mmoja wa Serikali ya Marekani ambaye hakutaka jina lake kujulikana amesema kuwa inaendelea na uchunguzi kumhusu jasusi huyo. Saab, hata hivyo, amesema kuwa jasusi huyo aliingia Venezuela kupitia mpaka wa Colombia, na kwamba alikuwa amebeba "sarafu" iliyomuunganisha na Shirika la Upelelezi la Marekani, CIA, bila kutoa maelezo zaidi, huku akiongeza kuwa jasusi huyo alikuwa akifanya kazi pia na mkandarasi binafsi wa jeshi.
Saab ameongeza kuwa raia wengine watatu wa Venezuela wamekamatwa kuhusiana na tuhuma za kushiriki njama ya kulipua viwanda hivyo vya kuchakata mafuta.
Mwezi uliopita, wanajeshi wawili wa zamani wa Marekani walihukumiwa kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kuhusika na jaribio la mapinduzi lililoshindwa.
Chanzo: Al Jazeera