Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,499
- 9,279
Marekani imesema inawawekea vikwazo vya viza watu wanaoaminika kuhusika au kushirikia katika kudhoofisha mchakato wa demokrasia nchini Uganda, ikiwemo wakati wa uchaguzi wa Januari na kipindi cha kampeni.
Waziri wa mambo ya nje Antony Blinken amesema katika taarifa kuwa vitendo vya serikali ya Uganda vinawakilisha kuporomoka kwa demokrasia nchini humo na kuheshimiwa kwa haki za binadamu.
Blinken amema uchaguzi ambamo rais mkongwe Yoweri Musevni alishinda muhula wa sita haukuwa huru wala wa haki. Taarifa hiyo hata hivyo haikuwataja waathirika wa vikwazo vya viza.
Uchaguzi huo ulishuhudia mchuano mkali katika Museveni mwenye umri wa miaka 76 na mwanamuziki maarufu ambaye pia ni mwanasiasa wa upinzani Bobi Wine mwenye umri wa miaka 39 aliekamatwa na kunyanyaswa mara kadhaa kabla ya uchaguzi huo. Wine baadae alidai kuwepo na udanganyifu mkubwa katika uchaguzi.