Marekani yaiwekea Uganda vikwazo vya kusafiri, yasema uchaguzi ulichakachuliwa

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,655
2,000
Marekani imesema inawawekea vikwazo vya viza watu wanaoaminika kuhusika au kushirikia katika kudhoofisha mchakato wa demokrasia nchini Uganda, ikiwemo wakati wa uchaguzi wa Januari na kipindi cha kampeni.

Waziri wa mambo ya nje Antony Blinken amesema katika taarifa kuwa vitendo vya serikali ya Uganda vinawakilisha kuporomoka kwa demokrasia nchini humo na kuheshimiwa kwa haki za binadamu.

Blinken amema uchaguzi ambamo rais mkongwe Yoweri Musevni alishinda muhula wa sita haukuwa huru wala wa haki. Taarifa hiyo hata hivyo haikuwataja waathirika wa vikwazo vya viza.

Uchaguzi huo ulishuhudia mchuano mkali katika Museveni mwenye umri wa miaka 76 na mwanamuziki maarufu ambaye pia ni mwanasiasa wa upinzani Bobi Wine mwenye umri wa miaka 39 aliekamatwa na kunyanyaswa mara kadhaa kabla ya uchaguzi huo. Wine baadae alidai kuwepo na udanganyifu mkubwa katika uchaguzi.
 

Liwagu

JF-Expert Member
Jan 25, 2017
2,563
2,000
Wao mbona wameibiana kura na Trump nani alie wawekea vikwazo au sababu ya power yao, muda utaongetu.
 

Tuna

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
691
1,000
Wamarekani kweli Kidonda Ndugu,Wao wanafikiri Marekani ndiyo nchi bora sana Duniani.Pumbavu zao
 

UHURU JR

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
11,511
2,000
Huko kwenyewe siku hizi shaba nje nje hakuna amani kabisa kwa mtu mweusi.
 

Ausar

JF-Expert Member
Mar 19, 2021
299
500
Kwenda Marekani ilikua dili enzi hizo........sahivi watu ni China
 

huska

JF-Expert Member
May 1, 2019
269
500
ila m7 amezidi bana sio ajabu wanawake wajawazito wa uganda wakijifungua watoto wanao fanana na m7 jamaa amekaa madarakani sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom