Marekani yaishtaki BP uvujaji mafuta Ghuba ya Mexico

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Marekani yaishtaki BP uvujaji mafuta Ghuba ya Mexico


NEW YORK,Marekani

SERIKALI ya Marekani kwa mara ya kwanza imewasilisha ombi la kuishtaki kampuni kubwa ya mafuta nchini Uingereza BP pamoja na kampuni nyingine nane, kuilipa fidia ya mabilioni ya dola kwa uharibifu kutokana na kuvuja kwa mafuta katika Ghuba ya
Mexico ambapo umwagikaji huo wa mafuta ndio lilikuwa tukio baya kabisa katika historia ya Marekani.

Ombi hilo liliwasilishwa juzi na Wizara ya Sheria katika Mahakama moja mjini New Orleans huku maelfu ya watu wengine wakiwemo wafanyabishara wakiishtaki kampuni hiyo kubwa ya mafuta katika mji huo.

Kulingana na Mwanasheria Mkuu wa Marekani, Eric Holder kampuni hiyo ya mafuta ya BP na kampuni hizo nane zinalaumiwa kwa kukiuka sheria za usalama, iliosababisha kutokea kwa ajali hiyo pale kisima cha Deepwater Horizon kilichopo chini ya bahari kilipolipuka Aprili 20 mwaka huu.
Matokeo yake ilikuwa ni kuvuja kwa mabilioni ya lita za mafuta yaliyosambaa kote katika Ghuba hiyo ya Mexico.

Bw.Holder alisema wana lenga kuthibitisha kuwa walalamikiwa katika kesi hiyo wana jukumu chini ya kifungu cha sheria kuhusiana na uharibifu wa mazingira kuifidia serikali kwa gharama zote za kusimamisha umwagikaji huo, hasara ya kiuchumi iliopatikana pamoja na uchafuzi wa mazingira.

Mwanasheria huyo mkuu aliongeza kuwa serikali ya Marekani katika kesi hiyo pia inataka kupiga marufuku uchimbaji wa mafuta chini ya bahari ambao haujaidhinishwa- hii ikiwa ni chini ya kifungo cha sheria kinachotaka kuwepo kwa maji safi.Katika malalamiko yao serikali ya Marekani ilisema BP hawakuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kisima hicho ni salama, na wala hawakutumia teknologia ya kisasa ya kuchunguza shughuli katika kisima hicho na kwamba vifaa vyake vya usalama vilikuwa na matatizo.

Katika taarifa yake BP ilisema itajibu madai hayo ya Marekani katika wakati ufaao na kwamba bado wataendelea kushirikiana na uchunguzi wote unaondeshwa kuhusiana na umwagikaji huo wa mafuta.

BP, kampuni ya tatu kubwa ya mafuta duniani imejitetea kuhusiana na namna ilivyokabiliana na janga hilo, ikiwemo kuuza mali zake katika maeneo mbali mbali duniani ili kukusanya kiasi ya dola bilioni 30 kuwalipa fidia waathirika na kusimamisha umwagikaji huo wa mafuta.
 
Back
Top Bottom