Marekani yaiondoa china kwenye viwango vya nchi wadhibiti wa ubadilishaji fedha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Marekani imeiondoa China kutoka kwenye orodha yake ya nchi zinazodhibiti kiwango cha ubadilishaji wa fedha.

Ripoti iliyotolewa jana na Wizara ya fedha ya Marekani inasema kwa sasa hakuna nchi mshirika wa kibiashara wa Marekani anayefikia vigezo vya kisheria vya kudhibiti thamani ya sarafu yake.

Waziri wa fedha wa Marekani Bw. Steven Mnuchin amesema kupitia taarifa kuwa wizara yake imetathmini maendeleo katika miezi kadhaa iliyopita na China na utendaji wake wa kifedha, na kuona kuwa China imetoa ahadi inayotekelezeka ya kutoshusha thamani ya sarafu yake ili kuongeza ushindani, huku ikiendelea kuhimiza uwazi na uwajibikaji.
 
Mchezo wao hua mtamu sana:

US inaongeza kodi kwenye bidhaa zinazotoka china nae China anaona sio inshu nashusha thamani ya pesa yangu.

Ngoma inogile.

dodge
 
Back
Top Bottom