Marekani yaikamata meli ya Korea Kaskazini, yadaiwa kuhusika kusafirisha makaa ya mawe

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
4,448
16,311
Marekani imeikamata meli ya Korea Kaskazini ikiilaumu kwa kukiuka vikwazo vya kimataifa. Idara ya haki imesema kuwa meli hiyo ilitumika kusafirisha makaa ya mawe ambayo ndio biashara kubwa ya taifa hilo licha ya kupigwa marufuku na Umoja wa mataifa kuendelea kuyauza nje.

NK.jpg



Meli hiyo ilikuwa imekamatwa nchini Indonesia mnamo mwezi Aprili 2018.Ni mara ya kwanza Marekani imeikamata meli ya Korea Kaskazini kwa kukiuka vikwazo na hatua hiyo inajairi wakati ambapo uhusiano kati ya mataifa hayo mawili umedorora.

Mkutano kati ya kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un na rais wa Marekani Donald Trump uliisha bila makubaliano mnamo mwezi Februari huku Marekani ikiisisitizia Korea Kaskazini kusitisha mpango wake wa kinyuklia huku nayo Pyongyang ikisisitiza kuondolewa vikwazo.

Korea Kaskazini imetekeleza majaribio mawili ya makombora yake angani katika kipindi cha wiki moja katika kile kinachoonekana kuwa jaribio la kuishinikiza Marekani kufanya makubaliano.

Je tunajua nini kuhusu meli hiyo?

Meli hiyo , kwa Jina the Wise Honest , ilikamatwa mara ya kwanza mwaka uliopita na Marekani ilitoa kibali cha kuikamata mnamo mwezi Julai 2018. Indonesia imeikabidhi Marekani meli hiyo na sasa inaelekea Marekani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Maafisa wa Marekani wamesema kuwa tangazo hilo halitokani na majaribio ya makombora yaliofanywa na Korea Kaskazini.

”Ofisi yetu iligundua mbinu ya Korea Kaskazini kuuza nje tani za makaa ya mawe ya kiwango cha juu kwa wanunuzi wa kigeni kwa kuficha asili ya meli , The Wise Honest ,” amesema mwendesha mashtaka wa Marekani, Goeffrey S Berman.


TR.jpg


“Mbinu hiyo iliifanya Korea Kaskazini kukwepa vikwazo mbali na kwamba meli hiyo ilitumika kuingiza mashine nzito nchini Korea kaskazini. ikiisaidia uwezo wa taifa hilo na kuendeleza msururu wa ukiukaji wa vikwazo.

Malipo ya utunzaji wa Wise Honest yalidaiwa kufanywa nchini Marekani kupitia benki zisizojulikana -hivyobasi kuipatia mamlaka ya Marekani fursa ya kuchukua hatua hiyo.

Korea Kaskazini imekumbwa na msururu wa viwakzo vya Marekani na vile vya kimataifa kutokana na hatua ya pyongyang kutengeneza silaha za kinyuklia pamoja na majaribio ya silaha.

Je Marekani na Korea Kaskazini zinaweza kurudi katika meza ya majadiliano?

Hatua zilizochukuliwa na mataifa hayo mawili yanaelekeza kurudi kwa uhasama, lakini mjumbe maalum wa Marekani kuhusu maswala ya Korea Kaskazini Stephen Biegun kwa sasa yuko Korea Kusini kujadiliana kuhusu njia za kuanza upya mazungumzo ya usitishwaji wa mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini.

Rais Trump amenukuliwa akisema kuwa ”hakuna mtu anayefurahia majaribio ya hivi karibuni ya Korea Kaskazini.

”Najua wanataka kujadiliana , wanazungumzia kuhusu majadiliano lakini sidhani kwamba wako tayari kujadiliana”, alisema.

Alikuwa rais wa kwanza aliye madarakani kukutana na mwenzake wa Korea Kaskazini wakati walipokutana mwaka uliopita lakini licha ya hayo na mkutano uliofuatia kumekuwa na hatua chache sana zilizopigwa katika kuhakikisha kuwa rasi hiyo ya Korea inaangamiza mipango ya kinyuklia.

Mwaka uliopita bwana Kim alisema kuwa atasitisha majaribio ya silaha za kinyuklia na kwamba hatofanya tena majaribio ya makombora ya masafa marefu yanayoweza kufika katika bara jingine lakini mipango yake ya kinyuklia inaonekana ikiendelea.

Mojawapo ya matokeo ya mazungumzo yao – juhudi za pamoja za kutoa mabaki ya wanajeshi wa Marekani waliouawa wakati wa vita vya Korea zimesitishwa.

BONGO5.
 
Da hawa jamaa wana hela sana sisi hata meli moja ya hivi hatuna tunaishia kununua ma pantoni tu
 
Back
Top Bottom