Marekani yaidhinisha kuanza kutumia dawa ya Ebola kuwatibu wenye CoronaVirus

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Picha

MAMLAKA ya Dawa na Chakula nchini Marekani (FDA) imetoa ruhusa ya dharura ya dawa ya ebola ‘remdesivir’ itumike kutibu wagonjwa wenye virusi vya corona.

Ruhusa ya kutumika kwa dawa hiyo kwa sasa imetolewa kwa watu waliolazwa hospitalini tu kwa ugonjwa wa homa ya mapafu Covid-19.

Jaribio la hivi karibuni la kitabibu linaonyesha kuwa dawa hiyo inasaidia watu mahututi wanaoumwa corona na inaaminiwa inaweza kuwasaidia kupona haraka. Hata hivyo, haijaonyesha inasaidia kupunguza idadi ya vifo.

Wataalamu wa dawa wametoa onyo kuhusu dawa hizo ambazo zilitengenezwa ili kutibu ebola na zilitengenezwa na kampuni ya Gilead pharmaceutical iliyopo mjini California.

Katika kikao na Rais wa Marekani Donald Trump Ikulu, Mkurugenzi Mkuu wa Gilead Daniel O’Day alisema Mamlaka ya dawa FDA ni hatua muhimu ya kwanza akisema kampuni hiyo itachangia chupa za dawa hiyo milioni 1.5. Kamishina wa FDA, Stephen Hahn alisema kwenye mkutano huo:
“Hii itakuwa tiba ya kwanza ya Covid-19 kupitishwa, tumefurahi sana kuwa sehemu ya uwezeshaji huo.” FDA si sawa na ile ambayo inatoa idhini rasmi ambayo inahitaji uangalizi wa hali ya juu zaidi.

“Remdesivir ni dawa ya majaribio ambayo haina ufanisi au usalama wa kutibu magonjwa yote.”

Gilead ilitoa angalizo la madhara makubwa ambayo yanayoweza kutokea. Pamoja na angalizo hilo, Trump amekuwa akiiunga mkono remdesivir kwa kuizungumzia kuwa ni dawa sahihi ya virusi vya corona.

Katika jaribio la kitabibu, taasisi ya taifa ya mzio na magonjwa yanayoambukiza Marekani (NIAID) imebaini remdesivir inapunguza muda wa dalili za ugonjwa huo kutoka siku 15 hadi 11.

Jaribio la dawa hilo lilifanyika kwa watu 1,063 hospitali mbalimbali duniani Marekani, Ufaransa, Italia, Uingereza, China na Korea kusini.

Baadhi ya wagonjwa walipewa dawa hiyo na wengine walipewa tiba ya ‘placebo’. Dk Anthony Fauci ambaye anaiongoza NIAID, alisema remdesivir imeonyesha wazi umuhimu wake kikubwa kuharakisha muda mtu kupona.

Hata hivyo, remdesivir inaweza kusaidia katika uponyaji na kuzuia watu kutibiwa chumba cha dharura. Majaribio ya dawa hiyo hayajaonyesha inaweza kuzuia watu kufa kutokana na corona.

Maswali mengi yakiwa hayana majibu kuhusu mwongozo wa tiba hiyo, Gilead ilishauri kuwa wagonjwa watumie dozi ya siku kwa wale wanaotumia mashine ya kupumulia na siku tano kwa wagonjwa ambao hawatumii mashine.

Gilead ilisema kwa sasa wanatumia dawa ambazo zilikuwepo kwenye hifadhi ya dawa zao na si rahisi kusafirisha maeneo mengine.

Serikali ya Marekani itaweza kupanga namna remdesivir itafikishwa kwenye hospitali za kwenye miji mbalimbali nchini Marekani imeathirika zaidi na ugonjwa huo wa Covid-19.

Haiko wazi kiasi cha dawa kitakachosambazwa duniani na gharama yake haijajulikana bado.

Gilead imesema inachangia dozi milioni 1.5 ya remdesivir zitakazokuwa na uwezo wa kutibu watu zaidi ya 140,000 bila gharama yoyote ile.
 
jamaa wanatapa tapa baada ya kusikia madagascar wana dawa
 
Tatizo la waswahili wanasoma tu kama kasuku lkn tayari wana "Prejudice" ndio maana mtu anatuma tu post ya kishabiki isiyo na mantiki yoyote.

Sijui walitaka wasikie dawa imegunduliwa Kasulu au labda Iran ndio wangefurahi lkn kwa bahati mbaya hivi ni vitu vinavyoenda na Intellect na sio uoteshwaji wala imani za dini.

All in all, rationale ni kusubiri tuone hatma yake itakavyokuwa na ikifaulu basi tuletewe tuweze kuitumia maanake mgonjwa ni mgonjwa hana jeuri, anacholilia ni kupona tu. That's all, mengine sasa ni umbeya tu.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom