Marekani yaidhinisha Dawa ya VVU ya kutumika mara 1 kwa mwezi badala ya vidonge vya kila siku

Hivi kweli mkuu leo hii itokee hicho unachokiwaza kuwa pasiwe na muingiliano wowote ule na mabara mengine?nakuhakikishia sisi wafrika ndani ya muda mfupi tu, tutaangamia !!hadi wao waanze kuyaona madhara sisi huku, tumekwishaaaa!!!kwa akili hizi za viongozi wetu wa kiafrika?!!kama unasema chanjo za polio ni majanga si tutengeneze zetu?!!kwani tumezuiwa?kwa wasomi wetu hawa?Africa hatuna wasomi bwana!!sisi bila wazungu maisha yetu yapo rehani!!
Inaweza kuchukua muda na kugharimu maisha ya wengi ila mwisho wa siku tutasimama tena, tutajifunza kuishi kwenye mazingira yanayotuzunguka.

Nephiles wale ni special case. Kama wa Khushi walijenga Pyramids n.k na wako Africa, tungetoboa na si weupe wale, moto, chuma, zama za mawe, matumizi ya ngozi za wanyama, dawa za mitishamba n.k Misri haikuwahi kuwa ya waarabu, tungetoboa tu mwisho wa siku.

Muingereza wa kwanza kuiona Africa, aliliambia bunge lao, ustaarabu, uelewa na ujamii wa wale watu, ni lazima tuwape elimu yetu tukitaka kuwatawala, kule hakuna wizi wala omba omba n.k

Kilwa ilitengeneza sarafu yake na umeme kabla mreno hajaichoma moto kwa wivu.
 
Nchi inayoilaribia america kwa population ni nigeria. With 206mil.. while US wakiwa na 331mil.
US ni super power kwa dunia na Amerika yote, Nigeria ndio super power wa Africa.

India naye anakuja juu haswa. Ajabu hao wote wana population kubwa. Mbona wasiwe maskini wa kutupwa kabisaaa kwasababu ya wingi wa watu?
 
ARVs ziko za aina nyingi sana na za gharama kubwa kadiri unavoweza afford uko Marekani. Cha ajabu wabongo wanaamini hizi ARVs za mtumba tunazopewa huku ni za sawa na wanazopata uko duniani.

Kuna dawa za zaidi ya dola 300 nani akulipie, tutaishia kupata hizi cheap ambazo patents zake ni rahisi na zina miaka kibao sokoni, wafadhiri wanalipia dozi mamilioni ya Waafrika hawawezi leta dawa advanced wataishiwa hela mapema. Unaona kama hao J&J (Johnson&Johnson) hawawezi toa ruhusa utumie tech yao wakati hawajapiga faida na kurejesha research & development cost.

Ni kama kwenda Kidimbwi kwa ofa ukataka ununuliwe Hennessy kisa haina hangover, utaishia kupata Serengeti Lite. Hizo dawa zisizo na side effects kubwa tutazisikiliza ukouko. Kwetu kuna mama mmoja anafanya kazi NGO moja anachukua dawa US hatumii hizi za Buguruni unazoenda umevaa sunglasses na ushungi.
Unataka kusema paracetamol ya bongo na USA ni tafauti?
 
What do say .? Wakifa hauta enea? Or hawa deserve kuishi?
Nikisema waathirika hawatakiwi kuishi itakua nakosea na si ubinaadamu kabisa, ila wakiishi wasiathiri na wengine, point yngu ni kuwa kama watatumia dawa hizo kuna uwezekano waathirika wakazidi zaidi
 
Wachache tu watakuelewa. Huwa nashangaa sana watu wanavyopapatikia vitu vya weupe hali ya kuwa hao weupe kila kukicha wanaplan kutumaliza kwa style mbali mbali. Mzungu katengeneza virusi ili afanye business Africa ndio maana kujifanya umegundua dawa ya UKIMWI watafanya kila njia kuhakikisha unanyamazishwa kwa kila namna.

Amaka Africa.
Kwani huko marekani na ulaya hakuna ukimwi? Kwanini useme hili gonjwa tumeletewa huku na wao while sisi wa africa mda wote tunawaza ngono zaidi ya kazi na research
 
Idara ya Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA), imeidhinisha dawa aina ya "Cabenuva" iliyoundwa dhidi ya virusi vya Ukosefu wa kinga ya mwili (VVU) kutumika mara moja kwa mwezi.

Maafisa wa Marekani walitangaza kwamba idara hiyo ya FDA imeidhinisha dawa inayoitwa "Cabenuva", ambayo inaingizwa mwilini kwa sindano mara moja kwa mwezi na ina athari ya muda mrefu zaidi kama kinga mbadala kuliko vidonge vya kila siku vinavyotumiwa na watu wenye VVU.

"Cabenuva" imeboreshwa kutokana na ujumuishaji wa "Rilpivirine" iliyozalishwa na kampuni ya Johnson & Johnson na "Cabotegravir" iliyozalishwa na ViiV Healthcare.

Ilielezwa kuwa FDA ilitoa idhini ya matumizi ya dawa hiyo mahsusi kwa kwa watu wazima wenye VVU na wagonjwa wasiokuwa na kinga ya kutosha ya kudhibiti virusi.

Cabenuva inatarajiwa kurahisisha ufuatiliaji wa maisha binafsi ya wagonjwa na kulinda faragha zao.

Mtaalamu wa VVU kutoka chuo kikuu cha California Dr. Steven Deeks, alisema dawa hiyo ya "Cabenuva" itaboresha hali ya maisha ya wagonjwa walioambukizwa VVU.
wanatudanganya hawa, tayari wanatumia dawa ya once per year, leo ndo wanatutanganzia dawa ya montly iliyokwisha achwa miongo kadhaa
 
Back
Top Bottom