Marekani yahimizwa kubadilisha sera yake ngumu dhidi ya China

ldleo

Senior Member
Jan 9, 2010
181
250
中美角力.jpg
Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Marekani imetekeleza sera ngumu dhidi ya China, na kusababisha kuzorota kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Jarida la kisiasa na kidiplomasia la Marekani “Maslahi ya Kitaifa” limetoa makala, inayosema serikali ya Marekani inapaswa kuzingatia zaidi “kujizuia na kutafuta maafikiano” badala ya “kupingana”, wakati wa kutunga mkakati mpya kuhusu China.

Makala hiyo iliyoandikwa na mchambuzi wa sera za kigeni wa Marekani Brian Clark imesema, maendeleo ya China yanashangaza sana. Tangu nchi hiyo ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango zaidi ya miaka 40 iliyopita, wastani wa ukuaji wa uchumi wake kwa mwaka umefikia karibu asilimia 10, na watu milioni 800 nchini humo wamefanikiwa kuondokana na umaskini. Maendeleo ya uchumi pia yameleta ongezeko la nguvu za kijeshi. Wachambuzi wengi wanaona kuwa, kama Marekani ikifanya vita na China barani Asia, China itapata ushindi. Clark anaamini kuwa, kufuatia ongezeko la uwezo wa kitaifa, China inajaribu kurekebisha utaratibu wa kimataifa, ikiwemo mfumo wa kiuchumi duniani. Kwa mfano, China imetoa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kuanzisha Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia, na Benki mpya ya Maendeleo ya BRICS. Zaidi ya hayo, China pia inataka kurekebisha mfumo wa usalama duniani.

Ili kukabiliana na maendeleo ya China, Marekani imechukua hatua mbalimbali ngumu dhidi ya China, ikiwemo vizuizi dhidi ya makampuni ya teknolojia ya juu ya China, haswa Huawei, vita ya kibiashara, kupinga China katika masuala mengi yakiwemo Bahari ya Kusini, Taiwan, Hong Kong, Xinjiang, na utafutaji wa chanzo cha virusi vya Corona. Licha ya hayo, Marekani pia inajitahidi sana kuchochea nchi nyingine kupinga China kwa visingizio vya haki za binadamu, usalama, makabila madogo, na mfumo wa kisiasa.

Ingawa wanasiasa wengi wa Marekani wanatetea sera ngumu dhidi ya China, lakini Clark anaona kuwa, sera hizo ni mbaya, na hazinufaishi upande wowote. Kwenye makala yake, amesema ukweli kuwa, Marekani haijawahi kuwa nchi yenye nia njema ya kulinda utaratibu wa kimataifa, badala yake, mara kwa mara inakwenda kinyume na utaratibu wa kimataifa na hata kukiuka sheria za kimataifa. Ameongeza kuwa “unafiki” wa Marekani pia unaonekana katika matumizi ya nguvu. Ametolea mfano wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Colin Powell, mwaka 2003, ambaye anadaiwa kuwa alichukua unga wa poda ya kufua nguo kama ushahidi wa Iraq kuwa na silaha za kikemikali, na Marekani kuanzisha vita dhidi ya Iraq bila ya kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Clark amesema, ni lazima Marekani itafakari kwa makini jinsi ya kukabiliana na maendeleo ya China, na mkakati wake mpya unapaswa kuzingatia zaidi “kujizuia na kutafuta maafikiano” badala ya “kupingana”. Hii ina maana kuwa, Marekani inatakiwa kukubali kwamba utaratibu wa kimataifa unaonesha mabadiliko ya nguvu duniani, na zaidi ya hayo, Marekani pia inapaswa kuheshimu kwa dhati sheria za kimataifa, na kutotumia nguvu ovyo, ili kupata uaminifu wa nchi nyingine.
 
Muuza viatu

JF-Expert Member
May 14, 2020
2,318
2,000
View attachment 1941585 Katika miaka ya hivi karibuni, serikali ya Marekani imetekeleza sera ngumu dhidi ya China, na kusababisha kuzorota kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili. Jarida la kisiasa na kidiplomasia la Marekani “Maslahi ya Kitaifa” limetoa makala, inayosema serikali ya Marekani inapaswa kuzingatia zaidi “kujizuia na kutafuta maafikiano” badala ya “kupingana”, wakati wa kutunga mkakati mpya kuhusu China.

Makala hiyo iliyoandikwa na mchambuzi wa sera za kigeni wa Marekani Brian Clark imesema, maendeleo ya China yanashangaza sana. Tangu nchi hiyo ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango zaidi ya miaka 40 iliyopita, wastani wa ukuaji wa uchumi wake kwa mwaka umefikia karibu asilimia 10, na watu milioni 800 nchini humo wamefanikiwa kuondokana na umaskini. Maendeleo ya uchumi pia yameleta ongezeko la nguvu za kijeshi. Wachambuzi wengi wanaona kuwa, kama Marekani ikifanya vita na China barani Asia, China itapata ushindi. Clark anaamini kuwa, kufuatia ongezeko la uwezo wa kitaifa, China inajaribu kurekebisha utaratibu wa kimataifa, ikiwemo mfumo wa kiuchumi duniani. Kwa mfano, China imetoa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, kuanzisha Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia, na Benki mpya ya Maendeleo ya BRICS. Zaidi ya hayo, China pia inataka kurekebisha mfumo wa usalama duniani.

Ili kukabiliana na maendeleo ya China, Marekani imechukua hatua mbalimbali ngumu dhidi ya China, ikiwemo vizuizi dhidi ya makampuni ya teknolojia ya juu ya China, haswa Huawei, vita ya kibiashara, kupinga China katika masuala mengi yakiwemo Bahari ya Kusini, Taiwan, Hong Kong, Xinjiang, na utafutaji wa chanzo cha virusi vya Corona. Licha ya hayo, Marekani pia inajitahidi sana kuchochea nchi nyingine kupinga China kwa visingizio vya haki za binadamu, usalama, makabila madogo, na mfumo wa kisiasa.

Ingawa wanasiasa wengi wa Marekani wanatetea sera ngumu dhidi ya China, lakini Clark anaona kuwa, sera hizo ni mbaya, na hazinufaishi upande wowote. Kwenye makala yake, amesema ukweli kuwa, Marekani haijawahi kuwa nchi yenye nia njema ya kulinda utaratibu wa kimataifa, badala yake, mara kwa mara inakwenda kinyume na utaratibu wa kimataifa na hata kukiuka sheria za kimataifa. Ameongeza kuwa “unafiki” wa Marekani pia unaonekana katika matumizi ya nguvu. Ametolea mfano wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Colin Powell, mwaka 2003, ambaye anadaiwa kuwa alichukua unga wa poda ya kufua nguo kama ushahidi wa Iraq kuwa na silaha za kikemikali, na Marekani kuanzisha vita dhidi ya Iraq bila ya kuidhinishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Clark amesema, ni lazima Marekani itafakari kwa makini jinsi ya kukabiliana na maendeleo ya China, na mkakati wake mpya unapaswa kuzingatia zaidi “kujizuia na kutafuta maafikiano” badala ya “kupingana”. Hii ina maana kuwa, Marekani inatakiwa kukubali kwamba utaratibu wa kimataifa unaonesha mabadiliko ya nguvu duniani, na zaidi ya hayo, Marekani pia inapaswa kuheshimu kwa dhati sheria za kimataifa, na kutotumia nguvu ovyo, ili kupata uaminifu wa nchi nyingine.
US anapaswa kujitafakar
 
Tuna

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
841
1,000
Mmarekani hana njia yoyote anayoijua zaidi ya Nguvu,Sumtime inabidi utumie busara kuliko nguvu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom