Marekani yafuta safari za ndege kwenda Cuba

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,521
9,325
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo ametoa taarifa kuwa wameiagiza wizara ya usafirishaji ya nchi hiyo kusimamisha safari zote za kuelekea Cuba isipokuwa zile za kuelekea uwanja wa ndege wa Jose Marti uliopo Havana.

Pompeo amesema uamuzi huo umechukuliwa kama muendelezo wa vikwazo dhidi ya utawala wa huo kufuatia utawala huo kukandamiza raia wake na kuunga mkono utawala wa Rais Nicolas Maduro nchini Venezuela

Pamoja na hayo mashirika ya kimarekani yanayofanya safari zake kuelekea Cuba, kama American airline na JetBlue nayo yamejumuihswa katika marufuku hiyo, kuanzia sasa ni safari za kuelekea Jose Marti pekee ndio zitakazoruhusiwa
 
Kumbe marekani siku hizi ni hakimu wa nchi zingine
Hawa viongozi wa marekani kuwaelewa ni vigumu! Suala la ukiukwaji wa haki na ukandamizaji wa Demokrasia wana lazimisha kwa Maifa yenye rasilimali za asili ambazo hawajazifikia. Au kwa Viongozi wanao tishia Maslahi ya Mabeberu! Mfano rahisi ni Saudi Arabia ambapo America ana Maslahi yake. huko ndo kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za Binaadamu na Democracy hakuna hata harufu yake huwezi sikia lakini America wajifanya hawaoni wala kusikia
 
Back
Top Bottom