Marekani yafanya njama ya kutorosha tani 40 za dhahabu walizonazo ISIS huko Syria

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Marekani yafanya njama za kutorosha dhahabu ya tani 40 kutoka kwa ISIS huko Syria
Feb 14, 2019 02:43 UTC
Shirika moja la haki za binadamu la nchini Syria limefichua kwamba muungano unaoongozwa na Marekani unaofanya mashambulizi nchini Syria unafanya juhudi za kuwakinaisha viongozi na wanamgambo wa genge la kigaidi la Daesh (ISIS) waliozingirwa huko Deire Zor wajisalimishe ili muungano huo upate kuwapokonya dhahabu za tani 40 walizo nazo magaidi hao.
Mapigano baina ya wanamgambo wa Kikurdi wanaojiita "Vikosi vya Demokrasia vya Syria" na genge la kigaidi la Daesh huko mashariki mwa Mto Furat katika mkoa wa Deire Zor yangali yanaendelea.
Shirika hilo la haki za binadamu ambalo liko karibu na waasi nchini Syria limeripoti kuwa magaidi wa ISIS wanafanya juhudi za kubakia huko mashariki mwa Mto Furat kwa hali yoyote ile ingawa hivi sasa wamezingirwa katika eneo dogo lenye ukubwa usiofika kilomita mbili.
Shirika hilo limegusia jinsi Marekani na wavamizi wenzake wanavyoendelea kufanya mashambulizi nchini Syria kwa madai ya kupambana na magaidi wa Daesh na kusisitiza kuwa, lengo la mashambulizi hayo ni kuwalazimisha viongozi na wanamgambo wa ISIS wajisalimishe lakini hadi sasa wamegoma kujisalimisha wakitaka wapewe dhamana ya kuondoka salama kwenye eneo hilo.
Madai ya shirika hilo la haki za binadamu lililoko karibu na waasi huko Syria yametolewa katika hali ambayo siku ya Jumamosi wapinzani wa serikali ya Damascus walitangaza kuwa, Marekani na wanamgambo wa Kikurdi wameshafikia mwafaka na magaidi hao wa ISIS na tayari magaidi hao wameshakubali kuondoka katika ukingo wa mashariki mwa Mto Furat.
 
Kwa mimi siwezi kushangaa wala siwezi kutafuta habari
Naamini wizi wanaoufanya USA kwani nimeisha shuhudia jinsi walivyokuwa wanaiba Iraq na kupeleka Turkey mpaka Ulaya
Sio wao tu wazungu wote wapo kwa kuiba tu
Wamechukua kila kitu na wanasaidiwa na vikundi (locals) kufanikisha wizi wao kama kuvunja museums na kupora kila kitu
Vito vingi sana walivyoiba vinauzwa leo London, NYC mpaka Paris
Na kwa macho yangu nimeyaona yakiwa London yakiuzwa kwa bei mbaya
Jiwe dogo (ukubwa wa kidole gumba) ambalo limechongwa vizuri miaka 3000 zilizopita linauzwa kwa £4000-5000
Halafu wanafikiri ni hadithi za kutunga wakati nimeona live
I was there


Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 
Back
Top Bottom