Tetesi: Marekani yafanya mazoezi Korea kusini hali ya wasiwasi imetanda

Jeshi
la Marekani limerusha ndege yake aina ya B-1B bomber. katika anga ya Korea Kusini kama sehemu ya mazoezi ya pamoja ya angani katika hatua inayoonekana kama onyo kwa Korea Kaskazini.
Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora ililodai kuwa ni la masafa marefu ambalo linaloweza kushambulia nchini Marekani.
Marekani awali imerusha ndege hizo zenye uwezo wa juu kuonyesha ubabe baada ya majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini au majaribio ya mabomu ya nyuklia.
Zaidi ya ndege 200 na maelfu ya wanajeshi wanashirikia katika mazoezi hayo ya kijeshi ambayo yatakamilika siku ya Ijumaa.
Pyongynag ambayo mara nyini hukashifu mazoezi ya pamoja ya Marekania na Korea Kusini, imeyataja mazoezi ya sasa kuwa uchokozi wa vita vya nyuklia.
Misukosuko imekuwa ikiongezeka tangu lifanyike jaribio la kombora mwezi uliopita lililosababisha lawama za kimataifa na onyo kutoka Marekani kuwa Korea Kaskazini itaharibiwa aabisa ikiwa vita vitatokea.
Kumbe mazoezi yanafanyikia kusini hiyo B_1B itie pua mpakani ijifanye imesahau mpaka new York iwe tunaenda na kupeleka watoto kujifunza historia
 
Hayo "mazoezi" hayana jipya! Hayajaanza leo na yataendelea! Lakini jipya ni kiduku kuwa na makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia na kupiga sehemu yoyote marekani!
 
Hayo "mazoezi" hayana jipya! Hayajaanza leo na yataendelea! Lakini jipya ni kiduku kuwa na makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kubeba vichwa vya nyuklia na kupiga sehemu yoyote marekani!
du kweli mkuu
 
Kama US hawamwogopi NK, kwa nini wasijifanye wamekosea wakapitisha hizo ndege katika anga la NK?
Hata kwa tathmini ya haraka kabisa utajua anayeweweseka zaidi katika mgogoro huu ni US.
KIM akirusha DUDE moja tu, matokeo yake ni:-
(1)US wanachanganyikiwa.
(2)Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wanahaha.
(3)JAPAN wanalala kwenye mahandaki.
(4)SK wanachuchumaa. NB:-Mpaka sasa mazoezi yanayoendelea SK ni ishara tosha kwamba KIM anawaendesha NK na US, yeye mwenyewe akiwa ametulia kimya hana papara anaangalia tu jinsi anavyowahenyesha MAZUZU.
Kwa kifupi huyo ndiye KIM JONG UN, the Panky man.
Umri umekusukuma uandike hivi
 
Anaharibu vipi amani ya dunia??
Anazuia waislamu wasitumie upanga kueneza dini yao na hivyo kusababisha wasikitike sababu ahadi za kitabu chao na maamrisho ya kuneza dini kwa upanga yanaonekana kushindwa
 
kwangu mimi nasali usiku na mchana Kim aendelee kuporomosha makombora yake. Siwezi kuwaombea wamarekani na washirika wake kwa sababu ni wanafiki na hao ndo chanzo cha machafuko katika uso wa dunia hii. Longlive Kim Maste of the Jungle
Naamini utakuwa made ina arabuni,au mwili made in afrika akili na fikra made in utumwani arabuni
 
Kama Kim kweli anaweza kupiga mtu basi ujue huo ndo utakuwa mwisho wa ulimwengu.Ka inchi kadogo kama wilaya ya Bagamoyo kupambana na nchi iliosheheni zana za kisasa za maangamizi ni kutaka ka inchi hako kukaondoa kwenye ramani au uso wa dunia.Zana zote alizonazo Korea ni zana zilizobuniwa na kutumiwa na Marekani muda mrefu uliopita.Kelele na bange za Kim sio kigezo cha ujemadari.
 
Umri umekusukuma uandike hivi
Naona hata wewe utakuwa mhanga wa bange kama Kim.Madude yote ya kivita alionayo Korea Kaskazini ni zana zilizobuniwa na kutumiwa na Marekani tangu 1947 katika kuhitimisha vita ya pili ya dunia.Wakati huo Korea hata kuvaa kaptura alikuwa hajui.Korea ambae amezingirwa na Marekani pande zote tena akina umbali maili sifuri amwache Korea anamwangalia tu arushe madude yake ya masafa marefu kwenda kuangamiza huko mbali kabisa.Mimi naona upeo wa watu wengine wa kufikiri hua unaambatana na kutumia makamasi badala ya ubongo.Nchi ilivyo ndogo kama wilaya ya Bagamoyo inaweza kutoweka kwenye uso wa ramani duniani ndani ya siku moja tu.
 
Hii imekaa vizuri mno. Kim must go; wakorea waondokane na dikteta na dunia iwe mahali salama zaidi pa kuishi. Sote tuiombee Marekani na washirika wake dhidi ya dikteta katili Kim.
Acha ugoro mkuu haukufai....ustaarabu wa Marekani Ni upi kuuwa watu Iraq Afghanistan Syria Libya na kwingineko, ndo ustaarabu na Kim amemuuwa raia wa nchi gani!!!?
 
Marekani ni jogoo wa dunia ni lazima asimamie amani ya ulimwengu.Amani ya dunia haiwezi kusimamiwa na Waarabu au Korea Kaskazini.Korea yenyewe ni ndogo kama wilaya ya Bagamoyo, katibu kata wa Tanzania akienda huko Korea nina imani atakuwa raisi bora kuliko huyu mvuta bange ambae anataka kuangamiza watu wake.
Imeisoma vzr ramani ya dunia mkuu eti NK Ni Kama bagamoyo....
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom