Marekani yaelemewa na janga la Corona, yapewa msaada na Misri

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Misri imetuma nchini Marekani ndege iliyosheheni vifaa na zana za kitiba za kukabiliana na virusi vya Corona, wakati huu ambapo nchi hiyo inayotajwa kuwa dola kubwa na lenye uwezo zaidi duniani linaendelea kulemewa na janga ugonjwa wa Covid-19.

Serikali ya Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri ambayo imekuwa ikifanya jitihada za kuwa na uhusiano mzuri na utawala wa Rais Donald Trump ilituma ndege hiyo iliyobeba misaada ya kitiba nchini Marekani jana Jumanne. Barakoa au maski 200 000 ni sehemu ya msaada huo.

Taarifa ya video iliyotumwa na ofisi ya Sisi imeonyesha shehena hizo za misaada zenye ujumbe ulioandikwa kwa lugha za Kiingereza na Kiarabu unaosema "Kutoka kwa watu wa Misri kwenda kwa watu wa Marekani".

Mwanasiasa Dutch Ruppersberger ambaye anaongoza kundi la wabunge wa Bunge la Wawakilishi la Marekani kutetea uhusianowa nchi hiyo na Misri amesema ndege hiyo ya misaada kutoka Misri imetua katika uwanja wa kijeshi wa Dutch Ruppersberger, nje kidogo ya mji mkuu Washington.

Kwa mujibu wa takwimu za leo za Chuo Kikuu cha Johns Hopkins, idadi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona nchini humo imefikia 819,000 huku zaidi ya 45,000 miongoni mwao wakifariki dunia kwa virusi hivyo.

Kwa sasa Marekani inashika nafasi ya kwanza duniani kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu walioambukizwa virusi vya corona na vilevile kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya wahanga wa virusi hivyo.

Serikali ya Rais Donald Trump inalaumiwa kwa kuchukua hatua za kupima virusi vya vya corona kwa kuchelewa, na kutokana na kuwa na idadi kubwa ya malaki ya waathirika wa virusi hivyo, sasa nchi hiyo inasumbuliwa na uhaba wa vifaa na zana za kitiba za kukabiliana na janga hilo.
 
Back
Top Bottom