ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,418
- 9,599
Marekani imechukua tena taji lake kwa kua na kompyuta ya kasi zaidi Duniani kwa kuipiku China.
Taji hilo lilikua likishikiliwa na China tangu mwaka 2013 kwa kuipiku Marekani kwa kua na Kompyuta yenye Kasi zaidi Duniani iliyoitwa Taihulight.
Supercomputer hiyo ya Sasa ya Marekani kwa jina 'Summit' ndio yenye Kasi kwa Sasa Duniani ikiizidi uwezo ile ya China kwa asilimia 60 ikiwa na uwezo wa kuchakata mahesabu 200 quadrillion kwa sekunde (ambayo ni sawa Trillion 200,000 kwa sekunde). Taihulight (ya Uchina) ilikua na uwezo wa kuchakata mahesabu 93 quadrillion kwa sekunde.
Kompyuta hiyo yenye ukubwa sawa na viwanja viwili vya tennis inatajwa kua ni nzito zaidi ya Ndege ya abiria ikiwa na uzito wa Tani 340,imeundwa kwa seva( servers) 4608 huku ikiwa na memori kubwa zaidi ya Petabytes 10 hutumia magaloni zaidi 4000 kwa dakika kuipooza ili isipate joto sana.
Supercomputer hiyo imegharimu kiasi Cha Dola milioni Mia mbili kuitengeneza ($200 millions)
Kompyuta hiyo yenye Kasi zaidi Duniani inaarifiwa kwamba itasaidia kwenye research mbalimbali kama za magonjwa hasa Cancer,nk,Pia na Mambo yahusuyo Jeshi.nk
US beats China to build world's fastest supercomputer that's one million times faster than a laptop | Daily Mail Online