Marekani ya waumbua Sitta na Mwakyembe yawasafisha Rostam na Lowassa

Issue sio mitambo bali mikataba ya kifisadi, kila mmoja anajua aina ya mitambo ni ya kisasa.

Kwa sheria yetu ya manunuzi ya umma hatuwezi kununua mitambo mtumba sio kwasababu ya Mwakyembe wala Sitta, ukitaka kumchafua mtu unajipanga kwa hoja na sio hadithi za dhaifu ambazo hata mtoto anaweza kung'amua.
 
Muanzisha mada ana akili fupi kama ya panzi! Hivi, tatizo la umeme Tanzania lilikuwa litatuliwe na Dowans tu? Dont be myopic, think before you write. Ina maana we unaona yaliyofanywa na Richmond na Dowans hapa Tanzania ni sawa? Ah, nimekumbuka, una magamba kichwani, so you cant think. Pole.
 
Namuunga mkono mia kwa mia muandishi wa hiyo makala. Ujinga wetu ndio umetuponza. Leo hii hiyo mitambo inhetusaidia sana. Rashid akajiondoa taratibu baada ya kuona hawasadifiki. Zitto alijisemea kweli akaonekana mbaya. Haya hao waliokuwa wakiipinga Dowans, kikowapi? Fedha wanalipwa na mitambo wameiuza. Sie jee? Bado tuipo kizani. Aliyezowea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.

Mod, hebu tuokoe!

Nimewahi kuomba kwamba ongeza forum ya kids corner ili watu wasije jikuta wakibishana na watoto wadogo wanaochezea keyboards tunapokwenda kazini. Itakuwa vizuri kama mchango ukiwa wa kitoto kama huu uhamishiwe kwenye kids corner.

Siamini kama mtu aliyejipima na kujiamini ku-join JF anaweza kutoa hoja dhaifu kama hii. Ni mchango unanikumbusha enzi ya utoto wangu nikifurahia hata kushikana mkono na mwanasiasa aliyetembelea shule yetu.

Pamoja na mwandishi wa habari inayojadiliwa, kuna sifa gani Bi Clinton akitembelea mitambo? Ni mtakatifu kwamba kaitakasa?
 
Hivi Hillary yeye ni Engineer au anajua nini kuhusu ubora wa mitambo ya kufua umeme.., hii si ndio kumuomba ushauri Kiafya Muuza Butcher
Hakisii, anawashauri waliobobea. Si kama washauri uchwara walioshauri mitambo isiwashwe, isinunuliwe, sasa hivi ushauri wao unamfanya Al Adawi aiuze mitambo bei nzuri kwa kuwa haijatumika sana na hapohapo analipwa na huku mitambo haikutumika. Nani ni mshauri mzuri kwa muono wako?
 
Muanzisha mada ana akili fupi kama ya panzi! Hivi, tatizo la umeme Tanzania lilikuwa litatuliwe na Dowans tu? Dont be myopic, think before you write. Ina maana we unaona yaliyofanywa na Richmond na Dowans hapa Tanzania ni sawa? Ah, nimekumbuka, una magamba kichwani, so you cant think. Pole.
Tatizo la umeme Tanzania lilikuwa litatuliwe na nyerere, mwinyi na mkapa. Hawakuweza. Kikwete ndio pekee anaelivalia njuga kulimaliza hilo tatizo na Dowans ilikuwa emergency measure, iliyopigwa vita na mapunguani wachache kwa kuwa tu walikuwa na mradi wao wa umeme wa upepo. Kiko wapi?
 
Kila amtendeae mwenzake mabaya, hulipwa hapahapa haraka sana. Sitta yuko wapi? Benchi anasikiliza kwa mbali, hana tena ile power aliokuwa nayo, utafikiri kamwagiwa maji ya mtungini, Selelii nae? Anahaha. Mwakyembe, ma halucination mpaka anatia huruma, mara nataka kuuliwa na AlShabaab, mara sijui nini, maskini roho yake hana pakuiweka. Wenzao on the other hand, ndio hivyo, mitambo imenunuliwa kwa raha na kitu kizito kimekuja kuikaguwa, na mifedha ya mitambo kukaa bure wanalipwa. Kuku na Bata kama kawa kwa AlAdawi.
Mzungu kiboko bwana, alikuja al adawi na malemba yake wakamtolea nje lakini kaja lady wa kimarekani watu kimya
 
Hakisii, anawashauri waliobobea. Si kama washauri uchwara walioshauri mitambo isiwashwe, isinunuliwe, sasa hivi ushauri wao unamfanya Al Adawi aiuze mitambo bei nzuri kwa kuwa haijatumika sana na hapohapo analipwa na huku mitambo haikutumika. Nani ni mshauri mzuri kwa muono wako?

Hivi kweli kule Iraq walikuta silaha za maangamizi? Au wakati huo akina Collin Powel walikuwa wanawashauri wasiobobea? Mmh nimeshasahau!
 
Kila amtendeae mwenzake mabaya, hulipwa hapahapa haraka sana. Sitta yuko wapi? Benchi anasikiliza kwa mbali, hana tena ile power aliokuwa nayo, utafikiri kamwagiwa maji ya mtungini, Selelii nae? Anahaha. Mwakyembe, ma halucination mpaka anatia huruma, mara nataka kuuliwa na AlShabaab, mara sijui nini, maskini roho yake hana pakuiweka.

Wenzao on the other hand, ndio hivyo, mitambo imenunuliwa kwa raha na kitu kizito kimekuja kuikaguwa, na mifedha ya mitambo kukaa bure wanalipwa. Kuku na Bata kama kawa kwa AlAdawi.

Oyaaaa hapa lazima umwage pumba! Ile post ya Mwanakijiji ni mwiba kama huioni
 
Taarifa ya Wizara ya Nishati
"...Tunapenda kuwakumbusha wananchi kwamba isingekuwa mdororo wa kiuchumi duniani ulioathiri utekelezaji wa mradi wa Mnazi Bay (MW 300) na kuchelewa utekelezaji wa mradi wa Kiwira (MW 200), mambo ambayo yalitokea bila kutarajiwa, tatizo la umeme nchini leo hii lisingekuwepo, maana miradi hii ingekuwa imetuondoa kwenye utegemezi wa umeme wa maji wa zaidi ya asilimia 50...."

Umeme Forum: TAARIFA KWA UMMA

Sijaona ktk press release hii eti kuna mgao sababu hatukununua mitambo ya Dowans. At least this Press Release makes sense than most of us who still have Dowans/Richmond hangover!
 
Back
Top Bottom