Marekani ya waumbua Sitta na Mwakyembe yawasafisha Rostam na Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Marekani ya waumbua Sitta na Mwakyembe yawasafisha Rostam na Lowassa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by issenye, Jun 29, 2011.

 1. i

  issenye JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 1,151
  Likes Received: 992
  Trophy Points: 280
  Na Daniel T. Kamna, Dar es Salaam
  [​IMG]

  WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton, alifanya ziara hapa Tanzania katika shughuli zake mbalimbali nchini alizindua mitambo ya Dowan’s iliyonunuliwa na Marekani na kupewa jina la Symbion.

  Clinton amesifu mitambo hiyo ya Dowan’s ambayo awali ilibezwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, Naibu Waziri wa Ujenzi, Harrison Mwakyembe, viongozi wa vyama vya siasa na wanaharakati. Clinton alipigilia msumari wa mwisho aliposema mitambo ya Dowan’s (Symbion) ni mitambo safi na imetengenezwa kwa teknolojia ya kisasa yenye kujali mazingira.
  Wahenga walisema; heri ya mtu mchawi kuliko mtu muongo, binadamu muongo anaweza kuleta madhara makubwa kwenye jamii, mfano, nchi kwa nchi kuingia kwenye vita, wananchi kukosa imani na serikali yao, pia ndoa za watu kuvunjika. Njia ya muongo ni fupi, amekuja Mmarekani amenunua mitambo hiyo ya Dowan’s, Waziri Sitta na wenzake sasa wamekaa kimyaa.
  Awali ya yote napenda kumpongeza mwanasiasa Kabwe Zitto, aliposimama kidete bungeni bila kujali ametoka upinzani, lakini kwa kujali utaifa wake, alisema mitambo hiyo ya Dowan’s inunuliwe ili kunusuru nchi kuingia gizani, matokeo yake Zitto alishambuliwa na kupewa jina la ‘Kabwe Zitto Fotokopi.’
  Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Madini na Nishati, Shelukindo, Sitta, Mwakyembe, Mbunge wa zamani wa Nzega, Seleli, katika kundi lao wapo 12, hawa wanafaa kupigwa viboko hadharani na kufukuzwa kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutokana na mateso waliyowapa Watanzania wenzao kukosa umeme kwa sababu ya visasi vyao vya kisiasa.
  Wataalamu wa TANESCO wakiongozwa na aliyekuwa Mkurugenzi wao Idrisa Rashid waliitaka Serikali inunue mitambo hiyo ya Dowan’s ambayo ingekuwa mkombozi na kuepusha nchi kuingia katika dhama ya mgawo wa umeme.
  Sasa kiko wapi, fedheha kubwa imewakumba Waziri Sitta na kundi lake pamoja na wanaojiita wanaharakati waliokuwa mstari wa mbele kupinga kuwashwa kwa mitambo ya Dowan’s wamezungumza kwenye makongamano, hata kwenye mitandao ya kompyuta (Internet) wamesambaza maneno ya kukashifu mitambo hiyo ya Dowan’s, Waswahili wamenena aliyepewa na Mola amepewa.
  Ninatamka bayana kwamba Waziri Sitta, Mwakyembe ndio hasa waliosababisha TANESCO na Serikali kuingia katika matatizo makubwa, hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro (ICC) katika hukumu yake ambayo TANESCO wanatakiwa kuilipa Dowan’s Sh bilioni 94 imechangiwa kwa asilimia 100 na Waziri Sitta, Mwakyembe na genge lao kutokana na husda mbaya dhidi ya wanasiasa wenzao.
  Viumbe hawa ni watu wabaya katika jamii, Waziri Sitta anasema eti Serikali haiwezi kununua vitu chakavu, swali kwako Waziri Sitta, je, vichwa vya treni (stemengene), ndege, je zinanunuliwa mpya? Mitambo ya Dowan’s imekataliwa kisiasa tu.
  Ninamuomba Rais wetu mpendwa Rais Jakaya Kikwete, asiwe na kigugumizi katika kutoa uamuzi, mfano kama hii ya Dowan’s. Mtu mwenye akili timamu baada ya ripoti ya wataalamu wa TANESCO kusema mitambo hiyo ya Dowan’s ni mizuri inaweza kukaa miaka 20 bila kufanyiwa ukarabati, tulishangaa Waziri Sitta na kundi lake kupinga kwa nguvu zao zote eti kununuliwa kwa mitambo ya Dowan’s hata kudiriki kusema bora nchi kuingia gizani kuliko kununuliwa kwa mitambo hiyo.
  Tulitegemea Rais kutoa uamuzi wa kununua mitambo hiyo kuliko kuyumbishwa na wanasiasa uchwara ambao hawautakii mema utawala wako Rais Kikwete kupata mafanikio.
  Mwisho wanasiasa wetu wasiingilie wataalamu wetu kwenye fani zao, wenye fani ya uhandisi ya ujenzi wa barabara, umeme n.k. chonde chonde wanasiasa wetu waacheni wataalamu wetu wafanye kazi ambazo wamezisomea, kodi za wananchi ndizo zimewasomesha wataalamu wetu ili kutoa huduma zinazostahili kwa Watanzania.
  Kazi zenu wanasiasa ni kutetea na kuomba msaada serikalini ili wapiga kura wenu wapate maendeleo majimboni kwenu si kuwaingilia wataalamu wetu katika kazi zao. Waziri Sitta, Mwakyembe na kundi lenu msalaba huu wa Dowan’s ni wenu. Hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro (ICC) dhidi ya TANESCO walipe Waziri Sitta na Mwakyembe na kikundi chao ikibidi wafilisiwe mali zao kufidia faini hiyo.
  Zilizobaki zilipwe na Serikali na TANESCO, sheria ni msumeno, Watanzania hawatawasamehe Waziri Sitta, Mwakyembe mpaka pale watakapoungama hadharani kwamba walidaganya umma na kuapotosha Watanzania juu ya mitambo ya Dowan’s kuhusu watu walio waamini kwa uongo wao.
  Mwandishi wa makala haya anapatikana kupitia 0715 309 669 / 0773 309 669.

  Source: Mtanzania
   
 2. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #2
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mwanzo nilidhani habari hii ni very sensitive, nilipoona source mwenyewe nimechoka.
  Duh, ama kweli lakuvunda halina ubani
   
 3. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hajui unaloongea huyo muandishi,

  Kifupi RICHMONDULI ilikua ni kampuni
  • ISIYOKUA NA UTAALAM, UJUZI WALA UZOEFU WA KUZALISHA UMEME POPOTE DUNIANI
  • ISIYOKUA NA MTAJI WALA FEDHA KWA MRADI MKUBWA KAMA ULE
  • ISIYOKUA NA MTAMBO HATA MMOJA WA KUFUA UMEME WAKATI WANAOMBA TENDER
  • HUWEZI FANANISHA NA SYMBION SABABU TOFAUTI NI KAMA USIKU NA MCHANA, SYMBION WANACHOUZA NI UMEME KWA TANESCO
  Kwa kifupi kampuni ya RICHMONDULI ilipewa kazi kwa UFISADI na KIFISADI.
   
 4. K

  Kahinda JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2011
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 849
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 60
  Hillary Clinton siye anayepata adhaa ya giza hapa Tanzania. Kama hoja hii ingeendana na tatizo kuwa limetatuliwa watanzania tungeona mantiki yake.
  Kinachoonekana sasa hivi ni uozo ulioko serikalini ambao ni mzigo kwa walipa kodi.

  Kama kuna kipindi nchi imekosa viongozi ni sasa, na hii imesababishwa na ubabaishaji wizi wa kura na watu walioko madarakani kung'ang'ania nafasi zao kwa lengo la kulinda maslahi yao, na kuendeleza ubadhilifu. ni aibu kwa baba kujiita baba wakati wanae wana lala njaa, labda tutapata fundisho la kulinda na kuchunga kura zetu wakati wa uchaguzi ili kukwepa kubambikiwa viongozi wasio kuwa na uwezo.

  Hakuna jinsi Rais na waziri mkuu na watendaji wote wa serikali hii wanavyoweza kujitetea, tunazidi kuona kashfa za kuweka mawaziri hotelini kwa gharama za wananchi na afadhali kama waziri mwenyewe angekuwa anauwezo wa kazi, wananchi wamekuwa na wanaendelea kuuawa na watendaji walio chini ya waziri ambaye tunamghalimia mamilioni kwa siku hotelini kwa kazi asiyofanya.

  Mkuu wa nchi kila siku anatumia mamilioni safarini huku hajui kinachoendelea nyumbani. Huu kama siyo usanii ni kitu gani? tulimlaani sana Mkapa
  wa ufisadi ambao ulisababishwa na yeye mwenyewe na serikali yake, lakini leo hii angalao tuna kumbukumbu yake kwa barabara alizo tuachia hivi Kikwete tutamkumbuka kwa lipi? na je haoni aibu?.

  Leo hii Anna Makinda anaedesha bunge kama bunge la CCM hili siyo bunge la CCM wala CDM, hili ni bunge letu wananchi. kosa letu na wala nisiseme kosa letu tatizo ni kwamba baadhi ya wabunge wanajua dhika kwamba hawakuchaguliwa na wananchi aidha waliingia kwa wizi kwa lengo fulani ndo maana hawapo bungeni kuwakilisha wananchi bali kuwakilisha walio wapeleka bungeni.

  Watanzania ukombozi wetu utakuja tu pale serikali itakapo kuwa ya wananchi na wa kwa ajili ya wananchi. Hilo halipatikani kama hatudai katiba huru ya wananchi Watanzania. Katiba itakayotupatia Tume huru ya uchaguzi" siku zote hainingii akilini timu iingie uwanjani ikiwa na refa na washika vibendera wake kisha timu inayoshindana nayo ishinde itakuwa muujiza". Hivyo ndivyo Lewis makame na vipendere vyake walivyofanya kwenye uchaguzi huu, sasa matokeo yake tunayaona kiongozi hana uwezo mambo ya memshinda lakini hataki kukubali. Hawzi kumlaumu mtu yeyote anatakiwa ajilaumu kwa kuunda serikali ya kishikaji. Uongozi haugawiwi kama bakshishi wala kwa uswahiba, sasa tunaelekea kwenye mchafuko wa nchi

  Tunaomba baadhi ya waandishi uchwara wasituletee pumba hivi leo hatusomi magazeti kama pale mwanzo ambapo tulikuwa tukisoma tu maadamu umesoma. Huyu mwandishi wa makala hii ameandika nadhani mfulahisha mmiliki wa gazeti hili ambaye nadhani tunamfahamu wote.
   
 5. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  amewaumbua vipi? acha ushabiki wewe.
   
 6. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ukiona hivi gamba litaka kuvuka kweli.tusubiri tu!
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Namuunga mkono mia kwa mia muandishi wa hiyo makala. Ujinga wetu ndio umetuponza. Leo hii hiyo mitambo inhetusaidia sana. Rashid akajiondoa taratibu baada ya kuona hawasadifiki. Zitto alijisemea kweli akaonekana mbaya. Haya hao waliokuwa wakiipinga Dowans, kikowapi? Fedha wanalipwa na mitambo wameiuza. Sie jee? Bado tuipo kizani. Aliyezowea vya kunyonga vya kuchinja haviwezi.
   
 8. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huyu aliyeandika (Daniel Kamna) si yule jamaa wa Simba ambaye ni mission town? Kama ni yeye nashangaa sana gazeti lenye hadhi kama Mtanzania linaweza kutumia habari yake. Huyu ni mtu anayeishi mjini kwa kulamba miguu ya mafisadi. Kazi yake kubwa ni kuanzisha fitna kwenye klabu ya Simba ili apate mavuno, na sasa amehamia kwa mafisadi. Shame on you Kamna/Mtanzania!
   
 9. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,143
  Trophy Points: 280
  Kila amtendeae mwenzake mabaya, hulipwa hapahapa haraka sana. Sitta yuko wapi? Benchi anasikiliza kwa mbali, hana tena ile power aliokuwa nayo, utafikiri kamwagiwa maji ya mtungini, Selelii nae? Anahaha. Mwakyembe, ma halucination mpaka anatia huruma, mara nataka kuuliwa na AlShabaab, mara sijui nini, maskini roho yake hana pakuiweka.

  Wenzao on the other hand, ndio hivyo, mitambo imenunuliwa kwa raha na kitu kizito kimekuja kuikaguwa, na mifedha ya mitambo kukaa bure wanalipwa. Kuku na Bata kama kawa kwa AlAdawi.
   
 10. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Ningeshangaa kama usingechangia?
  Sijui unalipwa shilingi ngapi kwa kuwatetea maagamba!
   
 11. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Hivi Hillary yeye ni Engineer au anajua nini kuhusu ubora wa mitambo ya kufua umeme.., hii si ndio kumuomba ushauri Kiafya Muuza Butcher
   
 12. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Ni mabaya yapi hayo waliyotenda???, mimi hapa naona tunao-pay the price ni sisi wananchi kwa kuwa Gizani na sio Sitta wala Mwakyembe
   
 13. Mhadzabe

  Mhadzabe JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2011
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 1,648
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Kuoshana na kuchafuana tu, hakuna la maana hapo! Kwani kwa kununua hiyo mitambo anayodai ni bora imemaliza tatizo la Umeme nchini? Napata shaka na mwandishi wa habari hii juu ya uelewa wake wa Sheria ya manunuzi na matumizi ya umma. Mwandishi anajitanabaisha kama mtu mwenye chuki, hasira, gubu, wivu na upendeleo juu ya mawaziri alowataja huku akipigia chapuo waajiri wake (RA and Co). Sitastaajabu muda si muda atakuja na habari kuwa watuhumiwa wa ufisadi wamesafishwa na MUNGU! Hivyo hawahusiki na matatizo yetu ya leo na hata ya kesho!
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Who are Americans to give verdict on our mafisadi? Their country's foreign policy is always guided by permanent interests, not permanent friends.
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hizi ni harakati za EL za kufanya Zuma type 'bounce back' baada ya kutoka Nigeria. Tutayasikia na kusoma mengi na ya ajabu sana kutokana na harakati hizo.
   
 16. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #16
  Jun 29, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  So what are you trying to convey to this distinguished forum ...ooh ok let me put it this way what is your objective?
   
 17. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #17
  Jun 29, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  We maza mbona unachonga sana? JK mwenyewe alidai kwamba haijui Dowans/Symbion, sasa wewe umeijulia wapi?
   
 18. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2011
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  wewe unalipwa ngapi na unalipwa na ngni?
   
 19. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #19
  Jun 29, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,882
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu kwangu mimi sidhani kama haya ni matatizo, kinachonitatiza ni kuwa RICHMOND kwa mara ya kwanza ilipokelewa kwa mikono miwili na Sita akiwa uwekezaji!! baadae akaja kuipiga chini kwa sababu ulizozitoa.

  Kwa kifupi nchi yetu usiwaamini sana wanasiasa wanaweza kukufanya uonekane mjinga sana, huku wakilinda interest zao!!
   
 20. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Husifikiri US wanaweza kununuwa uchafu wa CCM bure! lengo lao ni kuikowa CCM hisife maana wameshaona mbali, wanajuwa bila CCM hawawezi kupata madini ya Bure hapa Tanzania.
   
Loading...