figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,491
- 54,884
Mkutano wa 18 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa CITES (CITES COP 18) umeanza tarehe 17 Agosti 2019, Geneva, nchini Uswisi. Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaongozwa na Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangala, Waziri wa Maliasili na Utalii na unajumuisha wajumbe toka Idara ya Wanyamapori Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyapori (TAWA), Hifadhi za Taifa (TANAPA), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) na Idara ya Misitu na Mali Asili Zisizorejesheka ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Akiwa nchini Uswisi, Mhe. Kigwangala na ujumbe wake walitembea Ubalozi wa Tanzania nchini Uswisi na kuonesha mikakati iliyopo ya kutangaza utalii wa Tanzania na nafasi ya ubalozi katika kutekeleza azma hiyo. Wakiwa katika mkutano unaoendela wa CITES Tanzania imeshirki katika kutetea hoja mbalimbali zenye maslahi kwa nchi na imetumia fursa ya kuwa mwenyekiti wa SADC katika kuunga mkono hoja za nchi wanachama wa SADC zenye maslahi kwa Tanzania na jumuiya hiyo.
Ujumbe wa Tanzania umeshiriki katika mjadala wa agenda 20 ikiwemo agenda sita za kimkakati za uhifadhi wa simba, chui, tembo, Faru, Ushirikishwaji wa Jamii, makakati wa usimamizi wa wanyamapori jamii ya paka katika uhifadhi na umewezesha kutokupitishwa kwa maazimio ambayo yangeathiri ustawi wa uwindaji wa wa kitalii kwa wanyama hao na hivyo kuathiri mapato na uhifadhi hapa nchini. Mijadala mingine ambayo Tanzania imeendelea kutoa mchango wake ni pamoja tafsiri halisi kuhusu maeneo mahususi ya kuhamishia wanyamapori (appropriate and acceptable destination), andiko la mapitio ya ujumla ya Mkataba wa CITES, utambuzi wa nyara, uhifadhi wa viumbe bahari nk.
Aidha, Mhe. Kigwangala pamoja na ujumbe wake wamekutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Rob Wallace, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Marekani anayesimamia Masuala ya Uhifadhi wa Wanyamapori na Uvuvi na Hifadhi za Taifa (Assistant Secretary for Fish, Wildlife and Parks). Masuala yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na uhifadhi wa wanyamapori na umuhimu wa kujenga uwezo kwa taasisi za uhifadhi hapa nchini, kuboresha ushirikiano uliopo kati ya Serikali hizi mbili pamoja na zuio la uingizwaji wa nyara za simba na tembo nchini Marekani kutoka Tanzania.
Kufuatia kikao hicho Serikali ya Marekani imefafanua kuwa hakuna isipokuwa maombi ya uingizwaji wa nyara hizo hufanyiwa tathmini kwa kila ombi na hivyo haiwezi kuathiri uwindaji wa kitalii. Serikali ya Marekani imeomba kupewa taarifa muhimu kuhusu uwindaji wa simba na tembo ili kurahisisha utoaji wa vibali vya kuingiza nyara hizo nchini Marekani.
Vilevile kikao hicho kati ya Tanzania na Marekani kimeazimia kufanyika kwa mkutano wa wataalam kutoka Tanzania na Marekani kuhusu utekelezaji wa Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Marekani yaliyosainiwa mwaka 2006 na kufanyiwa mapitio mwaka 2012 pamoja na kuandaliwa kwa andiko “concept note” kuhusu maeneo mapya ya ushirikiano kati ya Tanzania na serikali ya marekani kwenye uhifadhi.
Mhe. Kigwangala na ujumbe wake vilevile wamefanya mazungumzo ujumbe wa Safari Club International (SCI) kuhusu namna bora ya kuboresha tasnia ya uwindaji wa kitalii. SCI wameahidi kuisaidi Tanzania katika sensa ya Simba na Chui, kutangaza uwindaji wa kitalii kwa kutoa banda maalum kwa Tanzania wakati wa maonesho ya uwindaji wa kitalii (Safari Club Convention – Reno, Marekani).
Aidha, Mhe. Kigwangala na ujumbe wake wanatarajia kukutana na Ujumbe wa Umoja wa Ulaya unaoshiriki Mkutano wa CITES tarehe 20 Agosti 2019 kujadili masuala ya uhifadhi pamoja na maeneo ya kimkakati ya ushirikiano kati ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya.
MY TAKE:
Kwanini Tanzania iombe kibari cha kusafirisha Tembo wakati kwetu hiyo biashara anakatazwa?
Tuseme Viongozi waliopo Madarakani Wanauza wanyama Kisiri siri?
Watu kila siku wanafungwa kwa kumatwa na Nyara za Serikali saa nyingine Serikali inachoma pembe za Tembo.
Kwanini leo aombe kibari cha kusafirisha nyara hii ya Serikali?