Marekani, watu 50 wana utajiri kuliko wa nusu ya Wamarekani

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Sanders: Dhulma isiyoelezeka Marekani, watu 50 wana utajiri kuliko wa nusu ya Wamarekani

Mar 27, 2021 02:33 UTC

Bernie Sanders, seneta wa chama cha tawala cha Democratic cha Marekani amelalamikia vikali dhulma iliyochupa mipaka inayotawala nchini humo na kusema kuwa, mali za matajiri 50 wakuu wa Marekani, leo hii ni nyingi zaidi kuliko karibu nusu ya wananchi wote wa nchi hiyo.

Sanders ameandika hayo katika mtandano wa kijamii wa Twitter na kusema, niacheni nirudie kulisemea hili, kwani jambo hili halikubaliki hata kidogo. Matajiri 50 wakuu wa nchi yetu wana utajiri mwingi zaidi kuliko wa karibu Wamarekani milioni 165. Hii ni aibu ya kimaadili.

Hivi karibuni pia seneta huyo wa jimbo la Vermont la kaskazini mashariki mwa Marekani alimlaumu Elon Musk, muasisi wa shirika kubwa la teknolojia na utafiti wa anga za mbali lijulikanalo kwa jina la SpaceX na kumtaka aelekeze nguvu zake katika kuwasaidia wakazi wa ardhini badala ya kushikilia ndoto yake ya safari za anga za mbali, wakati mamilioni kwa mamilioni ya wakazi wa ardhini hawana hata nyumba wala chakula cha siku, wakiwemo wananchi wengi wa Marekani kwenyewe.



Kwa mujibu wa vielelezo vya mabilionea wa Marekani vilivyotolewa na taasisi kubwa ya teknolojia ya Bloomberg, Elon Musk mwasisi na mmiliki wa shirika kubwa la SpaceX peke yake ana utajiri wa dola bilioni 174 hivi sasa akiwa ni tajiri mkubwa zaidi wa pili, kote ulimwenguni.

Hivi karibuni, bilionea huyo wa Marekani aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa anafanya juhudi za kukusanya fedha zinazohitajika za kuwezesha watu kuishi katika sayari kadhaa tofauti na kugundua siri zilizojificha za sayari za mbali. Tangazo hilo amelitoa wakati ambapo Wamarekani wengi hawana hata chakula na mahala pa kuishi.


My take: wanasahau kwamba Marekani ni capitalist nation!!!
 
Watu hawawezi kulingana kimaisha hilo liko hivyo tu hata nyumbani kwenu.

Chukulia watu kumi kila mmoja apewe milioni kumi baada ya mwaka mmoja kuna wengine watakuwa hawana hata shilingi moja na wengine watakuwa na mara mbili au tatu zaidi.

Kuna mambo mengine hayaelezi tuyaache hivyo hivyo.
 
Huyo jamaa ana akili za hovyo sana, mimi kuwa na utajiri sawa na nusu ya watu wengine kosa langu nini.

Socialism takataka kweli.
 
Back
Top Bottom