MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Nilidhani sisi kazi yetu ni kuiga tu masuala ya Marekani kumbe hata Marekani wanaweza kuiga masuala yetu.
Sisi toka mfumo wa vyama vingi uanze nchini mwaka 1992, washindi wa pili wa nafasi ya Urais wa Tanzania hawajawahi kukubali matokeo na kwa maana hiyo, hawajawahi kumkubali Rais wa Tanzania.
Kitendo hiki husababisha kuwepo na maandamano ambayo husababisha uharibifu wa mali za wananchi na serikali.
Hili somo limeanza kuwaingia vizuri Wamarekani ambao kwa sasa wameanza kuiga siasa zetu!
Wanachama na wapenzi wa Chama cha Democratic wakiongozwa na vyombo vya habari vilivyosaidia mgombea wa chama cha Democratic wamegoma kukubali kuwa walishindwa kwenye uchaguzi mkuu na kwa maana hiyo wamekataa hata kumtambua Rais Trump.
Wanachofanya kwa sasa ni kufanya maandamano ambayo yameendelea kusababisha uharibifu wa mali za wananchi na serikali.
Ninaamini kuna wabunge wa upinzani nchini Marekani wataingia bungeni kuisimamia serikali ya Trump ambayo wanatuambia hawaitambui kama ilivyo kwa wabunge wa upinzani nchini wanaoingia bungeni kuisimamia serikali wanayotuambia hawaitambui.
Hili ni jambo la kujivunia kuona tumeweza kuwafundisha Wamarekani siasa ambazo hawakuwahi kuzifahamu!
Big up Tanzania!
Baadhi ya viongozi na wabunge wa chama cha Democratic waliokataa kumtambua Trump kama Rais wa Marekani.
Polisi wakipambana na waandamanaji ambao ni wanachama na wapenzi wa chama cha Democratic ambao wanaamini Rais Trump hakushinda uchaguzi mkuu kwa haki.