#COVID19 Marekani: Waliochanjwa wahimizwa kuendelea kuvaa barakoa

Dong Jin

JF-Expert Member
Jun 4, 2018
754
1,442
Mamlaka ya udhibiti na kuzuia magonjwa Marekani CDC imetangaza amri mpya kuwa watu wote walio choma chanjo ya kuzuia Corona waanze tena kuvaa barakoa katika mikusanyiko ya ndani.

Amri hii inakuja miezi kadhaa tangu mamlaka hiyo ilipotoa ruksa kwa wote walio chanjwa kuto vaa barakoa.

Maamuzi ya CDC kutaka waliochanjwa kuvaa barakoa yametokana na kuongezeka kwa watu wenye maambukizi ya Corona katika miji kadhaa nchini humo ikiwemo Florida na Missouri vilevile kutokana na kuongezeka kwa ripoti ya maambukizi ya virusi hatari zaidi aina ya Delta kwa watu ambao wamekwisha pata chanjo zote mbili.

Mamlaka hiyo imeongeza kuwa kila mtu anapaswa kuvaa barakoa na kuweka msisitizo kwa Walimu, wafanyakazi, wanafunzi na wageni katika shule zote bila kujali wamechanjwa au bado.

Source: BBC Swahili
 
This is the bullshit that is making some people question the whole vaccination thing!

Mwishowe watasema iwepo lockdown nyingine.
 
Hiki ndio kinasababisha nisichanjwe.

Nimechanjwa lakini bado natakiwa kuchukua tahadhari zote kama mtu ambae hajachanjwa, sasa chanjo ya nini?

Mbaya zaidi, nimechanja bado uwezekano wa mimi kuambukizwa na kuambukiza tena covid ni zaidi ya 90% na hatari zaidi bado naweza kufa kwa covid huku nimechanjwa, sasa chanjo ya kazi gani?

Chanjo ikae mbali na mimi na familia yangu kabisa.
 
Kuna mambo mengi sana hayapo clear kuhusiana na hizi chanjo... Waliosema tujiridhishe kabla ya kutumia waliona mbali
 
Mamlaka ya udhibiti na kuzuia magonjwa Marekani CDC imetangaza amri mpya kuwa watu wote walio choma chanjo ya kuzuia Corona waanze tena kuvaa barakoa katika mikusanyiko ya ndani.

Amri hii inakuja miezi kadhaa tangu mamlaka hiyo ilipotoa ruksa kwa wote walio chanjwa kuto vaa barakoa.

Maamuzi ya CDC kutaka waliochanjwa kuvaa barakoa yametokana na kuongezeka kwa watu wenye maambukizi ya Corona katika miji kadhaa nchini humo ikiwemo Florida na Missouri vilevile kutokana na kuongezeka kwa ripoti ya maambukizi ya virusi hatari zaidi aina ya Delta kwa watu ambao wamekwisha pata chanjo zote mbili.

Mamlaka hiyo imeongeza kuwa kila mtu anapaswa kuvaa barakoa na kuweka msisitizo kwa Walimu, wafanyakazi, wanafunzi na wageni katika shule zote bila kujali wamechanjwa au bado.

Source: BBC Swahili
Sasa hapa unataka tuupate ujumbe gani hasa?ila ushauri wangu wa bure kwako nenda kapate chanjo,pia ufahamu kuwa hata kwenye tiba ya malaria ni mara kadhaa dawa zilizozoeleka zimeshindwa kufanya kazi kikamilifu na zikatengenezwa dawa aina nyingine,hivyo hatakwa corona halitakuwa jambo geni.
 
we jamaa acha kutudanganya, dawa gani ya malarha ishawahi kuja km chanjo?
 
Sisi wengine tulishaona usanii huu wa CDC toka corona inaanza, tumegoma kuchanja... liwalo na liwe.
 
Vizuri sana! Kujikinga ni muhimu zaidi maana chanjo haizuii maambukizi, bali inachochea tu uzalishaji wa kingamwili.
 
Back
Top Bottom