Marekani: Wabakaji kuanza kutolewa nguvu za kiume

miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
1,961
Points
2,000
miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
1,961 2,000

Jimbo la Alabama nchini Marekani limepitisha muswada wa sheria inayowalazimu baadhi ya watu waliopatikana na hatia ya kuwabaka watoto, waondolewe nguvu za kiume kupitia njia ya kemikali.

Chini ya sheria hiyo, wale watakaobainika kuwa na hatia ya kosa la kuwabaka watoto wenye umri chini ya miaka 13 watalazimika kuanza kupata dawa za kuwapunguzia uwezo wa kufanya tendo la ndoa huku wenye hatia watatakiwa kulipia matibabu kabla ya kuachiliwa kwa msamaha.

Hadi sasa kuna majimbo saba , yakiwemo Louisiana na Florida, yenye sheria ya kuwaondolea nguvu za kiume kwa wale wote wanaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto wadogo.

Aidha, Muswada wa sheria hiyo ulitiwa saini na Gavana wa jimbo la Alabama nchini humo, Kay Ivey Jumatatu, huku akisema hii itakuwa ni hatua nzuri ya kuelekea kuwalinda watoto katika jimbo la Alabama.

Hatua hiyo awali ilipendekezwa na Mbunge wa chama cha Republican, Steve Hurst ambapo alisema kuwa amekuwa akiathirika sana kwa kusikia matukio mbalimbali na kusikiliza ushahidi kutoka kwa mashirika yanayowalea watoto kuhusu namna watoto wadogo wanavyobakwa.

Hata hivyo, Muswada huo umekosolewa vikali na Muungano wa mashirika yanayopigania uhuru wa raia katika jimbo la Alabama, huku Mkurugenzi Mkuu wa Muungano huo, Randall Marshall akisema haijawa wazi kwamba ni kweli zina athari yoyote na ikiwa imethibitishwa kimatibabu.
 
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
10,256
Points
2,000
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
10,256 2,000
... kwanini wasiwatoe makende badala ya "kuwapunguzia" nguvu za kiume?
 
1gb

1gb

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2013
Messages
1,301
Points
1,500
1gb

1gb

JF-Expert Member
Joined Jun 30, 2013
1,301 1,500
Ushoga unaongezwa kwa akili na juhudi kubwa mno.
Huenda hiyo kemikali isiathiri mikuyenge tu,bali ikawa inanyevuanyevua mpk huko nyuma ya uchi wa mbele.
 
kidadari

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
5,035
Points
2,000
kidadari

kidadari

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
5,035 2,000
Kuna kila dalili hizo kemikali huwa zinaprlekwa nchi masikini ili kupunguza kasi ya kuzaliana
 
P

pye Chang shen

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2016
Messages
3,994
Points
2,000
P

pye Chang shen

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2016
3,994 2,000
Nguvu zenyewe zipo?
 
GODZILLA

GODZILLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2014
Messages
2,062
Points
2,000
GODZILLA

GODZILLA

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2014
2,062 2,000
Ngoja tuone waswahili watakuja na conspiracy theories zipi kuhusu hili!
 
J

J.wawatu

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Messages
227
Points
500
J

J.wawatu

JF-Expert Member
Joined Dec 20, 2013
227 500
Kwa hisani ya watu wa marekani!
 
B

bantulile

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2012
Messages
1,549
Points
1,250
B

bantulile

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2012
1,549 1,250
Ushoga unaongezwa kwa akili na juhudi kubwa mno.
Huenda hiyo kemikali isiathiri mikuyenge tu,bali ikawa inanyevuanyevua mpk huko nyuma ya uchi wa mbele.
Kwa hiyo mtu akiiba akatwe mikono atobolewe na macho
Akiiba chakula aondolewe utumbo
Akiiba kwa kalamu atolewe ubongo
Sheria ya ajabu hii
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
26,031
Points
2,000
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
26,031 2,000
Yani wanawatoa uwezo wa kusimamisha...

Mwenye tabia yake aachi, wataendelea kuwabaka na vifaa vya kufanyia...


Cc: mahondaw
 

Forum statistics

Threads 1,307,084
Members 502,332
Posts 31,601,095
Top