Marekani: Ujenzi wa jiwe la amri 10 za Mungu wapingwa

Wahindu je?! Na wale wanaoabudu mizimu?! Na atheists je..?! NINASEMA ULE NI UBAGUZI..!
THERE IS NO SEPARATION OF RELIGION AND STATE!
Ivi hao Wahindi na Atheists huwa wanapenda

Kuiba
Kuzini
Kuuwa
Kusema uwongo
Kutoheshimu wazazi
Kutamani mke wa wenzao nk.

Mambo ambayo yamekatazwa katika Amri kumi.

Ivi katiba ya huko marekani inaruhusu hayo mambo ?.

Wao wanazitii amri zipi ?

Hebu tujuze mkuu.
 
Amri kumi za Mungu ndizo zinazotumika mahakamani kutuhukumu. Na hata sharia za kiislam zimechenjuliwa toka kwenye kwenye amri kumi.
 
Nilijua tu wanaofanya upuuzi huo lazima wawe Republicans, maana ndo wanajifanya wanamjua sana Mungu.
 
Amri kumi za Mungu ndizo zinazotumika mahakamani kutuhukumu. Na hata sharia za kiislam zimechenjuliwa toka kwenye kwenye amri kumi.

Usisahau kuwa katika amri kuu za Mungu za kikristo kuna moja inayosisitiza kuwa wewe au mtumwa ( kijakazi) wako msifanye kazi siku ya saba ila muitumie hiyo siku kumtakasa Mungu.Ni mahakama gani duniani inayoitumia amri hiyo kuhukumu watu?
 
But still 9 commandments out of 10 are used by mahakama.
 
Usisahau kuwa katika amri kuu za Mungu za kikristo kuna moja inayosisitiza kuwa wewe au mtumwa ( kijakazi) wako msifanye kazi siku ya saba ila muitumie hiyo siku kumtakasa Mungu.Ni mahakama gani duniani inayoitumia amri hiyo kuhukumu watu?
8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, kwa hiyo Bwana akaibariki siku ya Sabato akaitakasa.
Kutoka 20 : 11

Kwahiyo hao hawataki kupumzika siku ya Jumamosi ?

Weekend yao wanataka iwe siku gani ?

Mbona karibu dunia nzima watu wanapumzika Jumamosi na Jumapili.

Au wanataka kupumzika Jumatano?

Katiba ya Marekani inatambua siku za Jumamosi na Jumapili ni (weekend) siku za mapunziko.

Au hawataki kupumzika kabisa ?
 
Back
Top Bottom