Marekani: Serikali ya Tanzania iweke wazi chanzo Kifo cha aliyedhaniwa kuwa na Ebola

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,373
Waziri wa mambo ya Afya wa Marekani ameitaka serikali ya Tanzania kuweka wazi matokeo ya Kimaabara juu ya Kifo cha mwanamke aliedhaniwa kufa kwa ugonjwa unaodhaniwa kufanana na Ebola.

Alex Azar,akizungumza na wanahabari nchi Uganda amesema wanafuatilia suala hili kwa karibu na ni vizuri serikali ya Tanzania kuweka uwazi kwakua ni muhimu katika mapambano ya ugonjwa huu.

Aidha amesema juhudi zimafanywa kuhakikisha Tanzania inatimiza matakwa ya kimataifa ya shirika la afya duniani(WHO) kulinda afya za watanzania na watu wa ukanda mzima.

Serikali ya Tanzania ilitangaza Siku chache zilizopita kwamba hakuna ugonjwa wa Ebola nchini.

Chanzo:VOA Swahili
IMG_20190919_195046.jpeg

====

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile jana amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa masuala ya kupambana na magonjwa kutoka Marekani Bw. Robert Redfield.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ofisi ndogo za wizara Jijini Dar Es Salaam yamelenga kuona namna gani nchi hizo mbili zinavyoweza kushirikiana katika kupambana na magonjwa hususani ya kuambukiza na milipuko.

Bwana Redfield amesema ziara yake nchini imekuja mara baada ya kutembelea nchi za Kongo DRC, Rwanda na Uganda ambazo zilikwishapata mlipuko wa ugonjwa Ebola na alitaka kujua Tanzania imejidhatiti vipi kukabiliana na ugonjwa huo usiingie nchini.

Kwa upande wake Naibu Waziri Dkt. Ndugulile amemuhakikishia Mkurugenzi huyo kuwa Tanzania imekuwa ikiwa mikakati ya utayari wa kukabiliana na Ebola hususani mipakani kwa kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wahudumu wa afya na pia imepeleka vifaa vya uchunguzi vinavyotumika kupima joto la mwili kwa watu wote wanaopita mipakani na kama atashukiwa kuwa na virusi basi kuna vituo maalum vya afya vilivyotengwa kwa ajili ya kutoa matibabu.

Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Muhammad Kambi na Kaimu Mkurugenzi wa Kinga Dkt. Janeth Mghamba kimeondoka na azimio la Serikali ya Tanzania na Marekani kuendelea kushirikiana katika kupambana na kudhibiti magonjwa kupitia program za Global Health Security.

Soma pia > WHO lalalamika ukosefu wa ushirikiano kutoka Tanzania kuhusu uwezekano wa uwepo wa visa vya Ebola
 
Waziri wa mambo ya Afya wa Marekani ameitaka serikali ya Tanzania kuweka wazi matokeo ya Kimaabara juu ya Kifo cha mwanamke aliedhaniwa kufa kwa ugonjwa unaodhaniwa kufanana na Ebola.
Alex Azar,akizungumza na wanahabari nchi Uganda amesema wanafuatilia suala hili kwa karibu na ni vizuri serikali ya Tanzania kuweka uwazi kwakua ni muhimu katika mapambano ya ugonjwa huu.
Aidha amesema juhudi zimafanywa kuhakikisha Tanzania inatimiza matakwa ya kimataifa ya shirika la afya duniani(WHO) kulinda afya za watanzania na watu wa ukanda mzima.
Serikali ya Tanzania ilitangaza Siku chache zilizopita kwamba hakuna ugonjwa wa Ebola nchini.
Chanzo:VOA SwahiliView attachment 1211849
HAYA MABEBERU KWA KWELI NI YA AJABU SANA YAANI YANALAZIMISHA KWA NGUVU ZOTE TUKUBALI,KWAMBA KUNA EBOLA, ha ha ha..../
Yanashindwa kuelewa endapo ingilikuwa ni ebola ingesha out break katika eneo husika kwa kasi sana.kiasi kusinge weza kuwapo na siri yoyote..!
 
Wamalizane kwanza na Iran ndio waje kutuchokoza sie

Wamuulize Idi Amini Uganda tulimfanya nini

Wamuulize M Reno tulimfanya nini kule Mozambique kama wamesahau wamuulize Kaburu tulimfanyaje kule Soweto

1965 tulivunja uhusiano na Uingereza kwa Ungese ungese kama huu kwa Ndugu yetu Mugabe v

Mikwala muhimu hata kama Mnyonge
 
Na Ndio concern ya Marekani na WHO kwamba kama kulikuwa na uvumi kwamba mtu kafariki kwa Ebola na baadae vipimo vikafanyika kujua ukweli,majibu yawekwe hadharani huyo mtu alikufa na nini?

Na hatari ya huu ugonjwa sio kwa watanzania tu ni ukanda mzima huu unaotuzunguka
Basi inawezakuwa tunaficha kweli na mwisho kifo kituimbue na wakati huo itakuwa ni kwa maelf.
Kama mtu alikufa na kudhaniwa huo ugonjwa,lazima sample zimechukuliwa na kucinguzwa,majibu yakoje?Tusiangalie utalii kwenye majanga yatakayotupinguza.
 
Back
Top Bottom