#COVID19 Marekani: Rais Biden ataka kutolewa Dola 100 kwa kila atakayepata chanjo ya COVID-19

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Biden kutoa dola 100 kwa kila atakapigwa chanjo ya COVID-19

100x2399= 239,900

hii ni kweli?

====

Rais wa Marekani Joe Biden amesema kila mwananchi atakaekubali kupigwa chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 atalipwa dola 100. Marekani ni nchi yenye chanjo za kutosha, na idadi kubwa ya watu wanaopinga kuchanjwa.

Rais wa Marekani Joe Biden amewashauri viongozi wa majimbo na miji yote nchini humo kuwalipa wakazi wao dola 100 ili wapigwe chanjo dhidi ya ugonjwa wa COVID-19.

Aidha ameweka sheria mpya zinazohitaji wafanyakazi wote wa serikali kuonyesha uthibitisho wa kupigwa chanjo au kulazimika kupimwa ugonjwa huo mara kwa mara, kuvaa barakoa pamoja na kuwekewa vikwazo vya kusafiri.

Hatua hizo za hivi karibuni ni miongoni mwa juhudi za Biden kujaribu kuwahamasisha Wamarekani wenye kupiga chanjo, huku aina mpya ya virusi vya corona iitwayo Delta ikiwa inaenea kote nchini humo, hasa miongoni mwa watu ambao bado hawakuchanjwa.

Marekani inashika mkia miongoni mwa nchi zilizoendelea kwa viwango vya watu waliochanjwa, licha ya kuwa na chanjo za kutosha zinazotolewa bure. Juhudi za Ikulu ya Marekaniza kuhamasisha wananchi kuchanjwa zimegonga ukuta, hasa kutokana na vuguvugu kubwa linalopinga chanjo hiyo, habari za uwongo zinazosambazwa kuhusu chanjo pamoja na migawanyiko ya kisiasa.

Uamuzi wa Biden kuhitaji mamilioni ya wafanyikazi wa serikali na makandarasi kuonyesha uthibitisho wa kupigwa chanjo unaonyesha kuwa Ikulu imeamua kuchukua msimamo mkali zaidi huku virusi hivyo vya aina ya Delta vikiwa vinazidi kuenea.

Biden amewaambia waandishi wa habari wa Ikulu, kwamba watu wengi sana wanafariki dunia au wanapoteza watu wanaowapenda.

Kulingana na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), takribani watu milioni 163.8 nchini Marekani ndiyo waliochanjwa dozi kamili ya chanjo kati ya idadi ya watu milioni 330.

Serikali ndiye mwajiri mkubwa zaidi nchini Marekani, na hatua ya Biden inaweza kuwa mfano wa kuigwa na makampuni binafsi ya kibiashara na taasisi nyingine wakiwa wanajitayarisha kurudisha wafanyakazi maofisini.

Wafanyakazi wa serikali ambao watashindwa kuonyesha uthibitisho wa kuchanjwa watalazimika kupimwa ugonjwa wa COVID-19 kila wiki au mara mbili kwa wiki pamoja na kuwekewa vikwazo vya kusafiri.

Wizara ya Fedha imesema serikali za majimbo zitatumia dola bilioni 350 zilizotengwa kwa ajili ya kupambana na corona kuwalipa wananchi dola 100 kila atakaekubali kupigwa chanjo ya kuwakinga na ugonjwa huo wa COVID-19.

Biden amesema anafahamu kuwa wale ambao tayari wameshachanjwa hawatofurahichwa na umauzi huo, lakini amelazimika kuchukua hatua hiyo ili kuwalinda Wamarekani wote.
 
🗣Ukuti ukuutii 🗣wa naniii wa na niii 🗣tumpeleke hospitali asije akawa kichaa🎶🎶 yesa yesa yeeee🎶
 
Jamaa katangaza hongo ya dola 100 za marekani ili raia wa Marekani wakubali kuchanjwa. Kwa taarifa tu ni kwamba zaidi ya asilimia 50 ya wamarekani wamekataa kabisa chanjo ya aina yoyote. Kuna watu wasiojielewa wanadhani upinzani wa chanjo upo Tanzania tu, la hasha! Sasa kuona hivyo Rais Biden ameamua kutangaza dau la hongo ya dola 100 kwa kila atakayeshawishika kuchanjwa! Kama Marekani inawashawishi raia wake kwa hongo ili wachanjwe, kwa nini tusiamini piaa kuwa Marekani inawashawishi kwa hongo viongozi wa nchi nyingine ili wakubali kupokea chanjo na kuwashawishi raia wao kuchanjwa!! Tofauti tu ni kuwa kwa marekani anayechanjwa ndiye anayepewa dola 100. Huku kwa wenzangu na mimi kwa nini tusiamini kuwa viongozi watapewa dola 100 kwa kila mtu atakayechanjwa? Zikiingia chanjo milioni moja, kwa nini tusiamini watahongwa kwa dola milioni mia moja ($100,000,000)? Kama huko kwao wanahonga kitu gani kitawazuia huku wasihonge? Mungu amewafunua peupe! Fungua link hapa chini usome uhayawani huo!
 
Tuchanjwe ama tusichanjwe , Kesho mapema Sana kanisa la ufufuo na uzima , wahi parking ni chache ....!!! Yanayokuja mbeleni , hakuna kupata huduma za Afya , banks na ofisi za Uma kama hujachanjwa , hakuna kusafri nje ya nchi kama hujachanjwa , hakuna kupeleka bidhaa sokoni kama hujachanjwa , wataoruhusiwa kukusanyika kwenye mikutano ya kidini ni wale waliochanjwa , stay tuned
 
Hawa viongozi wa mataifa mbalimbali wanajua kabisa madhara ya chanjo lakini kwa hongo wanayopokea wanaamua kufumba macho na kusema liwalo na liwe na wao wanafanyika chambo kwa kuwa wa kwanza kuchomwa chanjo bandia (siyo chanjo yenyewe), ili watu washawishike waingie chaka kichwa kichwa!! Haushangai, viongozi wakichanjwa mkono haupati sumaku ya kunasa vitu vya chuma kama sarafu. Duniani kote wanaochanja mwanzoni ni viongozi, lakini hakuna hata kiongozi mmoja duniani aliyeathirika na chanjo ya corona, lakini watu wa kawaida ndio wanaokufa na kulalamikia athari za chanjo!. Angalia usanii wanaofanya hapa:
 
Back
Top Bottom