Marekani na Urusi zawasilisha maazimio yanayokinzana kuhusu Venezuela

Display Name

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
423
451
Marekani na Urusi zimewasilisha maazimio yanayokinzana kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya kisiasa nchini Venezuela.

Marekani inamtaka rais Nicolas Maduro kukubali kufayika kwa Uchaguzi mpya wa urais haraka iwezekanavyo, lakini pia kuhusu misaada ya kibinadamu kuingia nchini humo.

Hata hivyo, Marekani haijasema inataka uchaguzi huo ufanyike lini, wakati huu ikiitaka jumuiya ya Kimataifa kumuunga mkono kiongozi wa upinzani Juan Guido kama kiongozi wa Venezuela.

Hata hivyo, Urusi nayo inataka katika azimio lake, mataifa ya nje yaache kuingilia siasa za ndani ya Venezuela na rais Nicolas Maduro, atambuliwe kuwa rais halali wa nchi hiyo.

Kwa namna ya mambo yalivyo, Marekani na Urusi zinatarajiwa kutumia kura zao za veto, kuzuia maazimio hayo.

Katika hatu nyingine, kiongozi wa upinzani ameonya dhidi ya serikali ya rais Maduro kukataa kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia nchini humo, wakati uo huo Maduro akionya kuwachukua hatua kali wale watakaojaribu kuleta vurugu katika nchi yake.

Sw.rf

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom