Marekani na Taliban kusaini makubaliano ya amani

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri wa nchi za kigeni wa Marekani Mike Pompeo anasema makubaliano ya siku saba ya kusitisha uhasama baina ya Marekani na Taliban yataanza kutekelezwa usiku wa leo ingawa hajasema yataanza muda gani hasa.

Hatua hiyo itakuwa mwanzo wa kutiwa saini makubaliano ya amani kati ya taliban na Marekani mnamo Februari ishirini na tisa hafla itakayofanywa huko Doha Qatar. Baada ya hapo Marekani itaanza mchakato wa kuviondoa vikosi vyake kutoka Afghanistan.

Pompeo anasema makubaliano hayo ya amani yatapelekea kupatikana kwa usitishwaji wa kudumu wa mapigano. Jumuiya kujihami ya NATO pamoja na Urusi wote wameunga mkono hatua hiyo ya kihistoria.

Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema suala hilo litafungua nafasi ya kupatikana kwa amani ya kudumu Afghanistan.
 
Huenda Wataliban wakawa sehemu ya serikali mpya ya Afghanistan baada ya mapambano ya miaka karibu 20.
 
Back
Top Bottom