Marekani na China kushirikiana dhidi ya Korea Kaskazini

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
16,618
30,575
160401041513_xi_obama_washington_976x549_getty.jpg
Mkutano wa dunia kuhusu Nuklia

Korea kaskazini imekuwa gumzo wakati wa mkutano wa dunia juu ya usalama wa nyuklia unaofanyika mjini Washngton.

Baada ya kukutana na Rais Xi Jinping wa China, Rais Barack Obama amesema wote wanawajibu wa kulifanya eneo hilo la rasi ya Korea kuwa eneo huru lisilo na nyuklia na kuiweka vikwazo zaidi dhidi ya Pyongyang.

Hali ya wasiwasi imetanda juu ya jaribio la Korea kaskazini kuendelea silaha za nyuklia na majaribio yake ya teknolojia ya makombora.

Awali Rais Obama alikutana na viongozi wa Japan na Korea kusini kuweka msimamo wa pamoja juu ya suala la usalama katika rasi hiyo ya Korea.

Pamoja na kwamba nchi ya pili kwa nuklia duniani Urusi haijahudhuria mkutano huo, Rais Obama alifanya mazungumzo na Rais Xi Jinping of China ambapo amesema yeye pamoja na Rais XI wamekubaliana kuondoa nuklia katika eneo la rasi ya Korea na kutekeleza vikwazo vipya vilivyopitishwa na Umoja wa Matiafa kwa lengo la kuipa shinikizo jipya Korea Kaskazini.

Kwa upande wake Rais Xi amesema China inataka kuongeza mawasiliano na kuratibu jambo hilo ambapo nchi zote mbili zimekubaliana kukutana kila mwaka kuzungumzia masuala ya usalama wa nyuklia.

Wamesema pia watafanya kazi kwa pamoja kuzuia malighafi za kutengeneza nuklia na kuratibu juhudi za kuzuia malighafi hizo kuangukia mikononi mwa magaidi.

Hata hivyo kasoro moja katika mkutano huo ni kutokuwepo kwa Rais Vladimir Putin. Urusi na Marekani wanamiliki karibu asilimia 90 ya silaha za nyuklia hivyo Mosco kukataa kuhudhuria mkutano huo unaweza kufanya makubaliano yatakayofikia isiyatekeleze.

Chanzo: BBC
 
moscow kwa kutafuta umaarufu wa kijinga hawajambo, ndo maana china na marekani nchi kubwa uchumi mkubwa, russia nchi kubwa uchumi kiduchu
 
Sexer acha maneno, njoo na figures za uchumi mduchu wa russia sio maneno tu.
 
Sexer acha maneno, njoo na figures za uchumi mduchu wa russia sio maneno tu.
US $17.41 trillion
CHINA 10.35 trillion
RUSSIA 2.05 trillion
kiuchumi cha russia kinaingia mara 5 kwa mchina na karibia mara 9 kwa limarekani
 
hiyo pyoyang inaonekana ina siraha za hatari sana angekua wa kawaida wangekavamia maana vikao haviishi kuingia hapana ni kupunguza uingizaji wa virutubisho vya nyuklia..mbona iran walimsechi huyo dogo tusimbeze anatisha pia..
 
Marekani anajitia uanaume,amguse msela tushuhudie mwisho wa dunia,anajifanya kuweka vikwazo,unamuwekea vikwazo mtu asiyetegemea kitu kutoka kwako si ujuha huyo,Korea Kaskazini ni dunia tofauti na hili wana dunia yao wale, #TEAM #SOCIALISM #TEAM #RUSSIA #TEAM #KOREA............Pumbavu zenu Marekani na vibaraka wenu na wafuasi wenu wooooooote
 
Endelea kujipa moyo, eti wana dunia yao, ipi hiyo? wewe hujui chochote kuhusu Korea kaskazini, hujui ukoo wa huyo rais Kim Jong Un, Kwa Taarifa yako huo ni ukoo wa vichaa, Siku Korea kaskazini ikianza kupigwa mtaanza kulia humu Kama kawaida yenu, oooh Marekani anapenda kuonea nchi ndogo, kipindi kile Saddam anajifanya kidume mlikuwa mnampa kichwa hivi hivi, alipochapwa na kupinduliwa, mkaanza kulia tena, nyie ndo pumbavu zenu.
 
We ndo hujui chochote kuhusu Korea kaskazin,ila mumeo Marekani anajua ndo maana haleti fyokofyoko....jinga we
 
US $17.41 trillion
CHINA 10.35 trillion
RUSSIA 2.05 trillion
kiuchumi cha russia kinaingia mara 5 kwa mchina na karibia mara 9 kwa limarekani
inasaidia nini serikali kuw na maela yote hayo,uchumi wa china ni mkubw lakin wananchi wa urusi wanaish maish mazur kuliko china.kam uchumi tu Nigeria ndo inaongoz kuw na uchumi mkubw africa,je maish ya nigeria na Tanzania yapi mazuri?
 
anzisha mada heading uandike hiv, 'uchumi mkubwa wa nchi unasaidiaje wananchi wake ukilinganisha na uchumi mdogo'
 
moscow kwa kutafuta umaarufu wa kijinga hawajambo, ndo maana china na marekani nchi kubwa uchumi mkubwa, russia nchi kubwa uchumi kiduchu
Mpaka Leo bado watafute maarufu ? Kuna sababu nyingine muhimu wala sio hiyo yako ya ngumbalu..
 
Endelea kujipa moyo, eti wana dunia yao, ipi hiyo? wewe hujui chochote kuhusu Korea kaskazini, hujui ukoo wa huyo rais Kim Jong Un, Kwa Taarifa yako huo ni ukoo wa vichaa, Siku Korea kaskazini ikianza kupigwa mtaanza kulia humu Kama kawaida yenu, oooh Marekani anapenda kuonea nchi ndogo, kipindi kile Saddam anajifanya kidume mlikuwa mnampa kichwa hivi hivi, alipochapwa na kupinduliwa, mkaanza kulia tena, nyie ndo pumbavu zenu.
Mkuu mzozo wa USA na North korea umeanza siku nyingi sna,kuliko hata ule wa libya mbona hadi leo USA hajampiga huyo north korea
 
inasaidia nini serikali kuw na maela yote hayo,uchumi wa china ni mkubw lakin wananchi wa urusi wanaish maish mazur kuliko china.kam uchumi tu Nigeria ndo inaongoz kuw na uchumi mkubw africa,je maish ya nigeria na Tanzania yapi mazuri?

Mkuu si rahisi hawa watu wakakuelewa, hizi ni nchi tofauti zenye mifumo ya kiuchumi tofauti, living standards tofauti, priorities tofauti nk - uwezi kuwa na a blanket standards kwa Wachina, Warusi na Wamarekani - mfano nenda Merikani tembelea raia wa kawaida mjini na kwenye Rular areas, sasa linganisha na wenzao wa Urusi - nani wanaishi maisha bora na yenye uhakika wa mlo wa kila siku na matibabu ya bure mpaka mwisho wa siku yako ya kuishi hapa Duniani, je, baina ya nchi hizo mbili ni hipi yenye ku guarantee maisha bora kwa kila raia?

Haya tuje kwenye viwanda na upatikanaji wa mali ghafi zinazo hitajika kwenye viwanda, kati ya nchi hizo mbili ni hipi cost of production hiko chini (simaanishi viwango) sasa unategemea end products zinauzwa kwa bei gani.

Ninacho taka kusema hapa ni kwamba namba kuwa hefy doesn't tell you everything - hapo ndipo watu wengi upotoka kwa kuanza kudhalau Mataifa ya watu wengine, yaani waswahili wanakuwa overly vocal na kukasirika kuliko wazaliwa/raia wa huko, kama hawajui what is inside the hood msianze kuponda ponda nchi za watu.
 
moscow kwa kutafuta umaarufu wa kijinga hawajambo, ndo maana china na marekani nchi kubwa uchumi mkubwa, russia nchi kubwa uchumi kiduchu
Hujui siasa ya Dunia kijana unawaamini sana USA na China kwa taarifa yako Ulaya wakikohoa tu jamaa anawanyima gesi uone wanavyotaabika, USA hana ubavu Wa kupigana na Urusi hadi asaidiwe na wasaidizi naona wanaiogopa Russia
 
Mkuu mzozo wa USA na North korea umeanza siku nyingi sna,kuliko hata ule wa libya mbona hadi leo USA hajampiga huyo north korea

Wanajua Wakorea si lelemama, si uliona Libya walingia bila ya kubisha hodi, sasa waijaribu Korea ya Kasikazini waone itachukua masaa mangapi Korea kusini kutekwa na infrastructure zao zote kuharibiwa.

Korea Kaskazini hawatajali hasara walisha jitayarisha kwa siku nyingi jinsi ya ku deal na uvamizi wa Kimarekani na washirika wake - wako tayari kufa mamillioni lakini watahakikisha Wamerika wanapata fundisho.

Jamaa hao wana umoja sana, propaganda za MSM ndio ziko mstari wa mbele kuwa demonise kwa kutangaza habari mbaya masaa yote kuhusu Taifa hilo.
 
Back
Top Bottom